Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Naona siku hizi wanasaccos wote mmehamia CCM yaani ni raha sana kweli Hayati Magufuli aliposema Saccos itakufa ikifika 2020 yametimia.
Mkuu haki mengine badae, si mlitaka mkandia mama nyie wafuasi wa mwendazake , mlipo ona twamkingia kifua mkaanza eti twajipendekeza ,CHADEMA HAIJAWAI JIPENDEKEZA KWA MTU ,


Mfano nyie ccm mna mbwai, Mama mkimzingua alafu akasema 2025 angombee pitia CHADEMA , si chama kinakufa kibudu

Sikia chadema organization yake ccm Cha mtoto Sana ,elewa hilo ,
 
Cha msingi mkuu ,asije toroka chato to Kagera to Mtukula then Unganda KARIBU ila bado akipuyanga mpaka Kanyigo anaweza fika Uganda kirahisi mno KWA njia za panya pitia ziwa Victoria, pale zipo mitumbwi ya ingine ni rahis Sana that's ifikapo maeneo yale mali Kama vitenge nk TOKA Ug rahis Sana pata

Kama alitenda wema atulie,Rais SSH alisema wema wa mtu hufuata popote aendako, so nimetoa angalizo KWA vyombo vyetu vya ulinzi
BAVICHA siku akili zenu zitakaporudi ndo mtaelewa game inayochezwa .kaeni mjenge chama chenu 2025 sio mbali nyie hangaikeni na Mambo ya Chama tawala .
 
BAVICHA siku akili zenu zitakaporudi ndo mtaelewa game inayochezwa .kaeni mjenge chama chenu 2025 sio mbali nyie hangaikeni na Mambo ya Chama tawala .
Tulisha kubaliana Rais wa Jamhuri ya muungano wa tz ni mmoja , ambae anawajibu wa kutenda haki KWA watu wote bila kujali dini,chama, kabila pindi hawapo madarakani,

Elewa ndio aliopo madarakani katokana na chama Cha ccm ,ila KWA mda huu ni wa watanzania wote , Msilete habari za mwendazake hapa aliamini ccm KWa kua ndo chama chake basi Wana haki kuliko wengine bila kujua awapo pale ameaapa kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano Wala sio ilani ya CCM , na katiba ndio inayotambua Jamhuri ya Muungano wa Tz na watu wake na vitu vyote vilivyomo ikiwemo sisimizi,


Bahati mbaya mkamjaza upepo , akasahau kiapo chake ,akazalisha watu wa kuabudu na kusifia, mfano kabudi, GWAJIMA waziri, Sabaya , MACKONDA , Msiba, na wewe mwenyewe ikiwemo ,nje ya wengine kibao ,wakina kangi lugola,


Mungu akasema umetukuzwa Sana hata kuliko mie nilie kuumba , nakuchukua Sasa na maulinzi YAKO ya kidunia yakiwemo mabunduki ,msafara mkubwa zaidi ya ule wa YESU na na wanafunzi wake, maana YESU hakuwai tumia Chopa au helkopter ,japo alipaa KWA uwezo wa Mungu.

Akamchukua maana yeye ni fundi na alpha na Omega, Sasa mmebaki angaika hamjui wapi mshike ,MWAFAA nawambia
 
Tungesamehana tu tukatafuta katiba mpya na tume huru ili kutengeneza mfumo bora ( justice)

Tunasahau mifumo yetu ya utawala ndio inafanya watu wajisahau na kutena uovu kama huu.

Visasi havijawai kuleta amani na umoja.

Nelson Mandela angefanya visasi sijui kama angekuwa anakumbukwa kwa mazuri leo.
Nafikiri sio suala la visasi. Hapa ni suala la jinai alizotenda. Kama ikithibitika kuwa alihusika kwa namna moja au nyingine lazima awajibike. Hana kinga yoyote kisheria ya kuzuia asishughulikiwe
 
Leo nimemuona Makonda akiwa Chato kutembelea Kaburi la Magufuli.

Katika ziara hiyo, Makonda eti alisimamishwa na wananchi wa Chato na kuzungumza nao. Na katika maigizo hayo,Makonda amelia sana.

Juzi niliona gazeti moja limeandika kuwa jalada la uchunguzi wa utekwaji wa mfanyabiashara maarufu Mo limepelekwa kwa DPP.

Naamini baada ya kukamatwa kwa Sabaya kwa kuwa maovu ya Makonda yanafanana na ya Sabaya, amenusa kitu. Hivyo ameamua kuanzisha harakati za kutafuta huruma za watanzania hasa wasiojua drama zake ili kuitisha Serikali isimchukulie hatua kama alivyofanyiwa Sabaya.

Sisi wengine tunajua Makonda ana hasira mno na utawala wa mama Samia baada ya kuachwa kwenye teuzi zote zilizofanywa. Yeye pamoja na wanazi wengine wa Magufuli waliokuwa wanafaidika na utawala wake wa kikatili na kidikteta wameanzisha kundi linaloishambulia Serikali ya Rais Samia katika mitandao ya kijamii. Kule FB wanatumia ID ya veronica france.

Kama kundi hili halitadhibitiwa mapema, litaisumbua sana Serikali ya mama Samia.
Angewalilia na Aliwateka na kuwaua Makonda mnafiki sana
 
Masela wa Segerea wanamsubiri m.at.ako ya taifa ....
 
Pamoja na kwamba hakuna asiyejua kua huyu kijana aliongoza makundi ya unyang'anyi,kupiga,kuteka na kuharibu mali za watu wazi wazi kwa kutumia mamlaka yake alipokua RC wa Dar es salaam mpaka kufikia nchi ya Marekani kumwekea vikwazo kutokusafiri nchini humu baada ya taarifa zao za Intelligence Angecy kubaini kua ni mhusika wa matukio yote. Pamoja na uhalifu huu wote, Makonda hawezi kuguswa na mtu.

Sababu kuu ni kwamba aliguswa yeye wanaweza kuguswa watu wengine wazito sana. Matukio ya Makonda ni zaidi ya Sabaya, Kwa mchamungu yeyote atakubali ana nami kua Makonda alipaswa kua jela wakati huu. Makonda anatajwa kua na Utajiri mkubwa kwa kazi yake ya ukuu wa Mkoa tu pengine kuliko Ma-RC wote wa Tanzania.

Kitu kiingine ni Mama kutamka bayana kua ndiye aliyemtabiria kua Makamu wa Rais, Je, Mama anaweza kumuundia Kamati ya kumchunguza Makonda? Mama anaweza kuweka maslahi ya kitaifa mbele kuliko kuangalia uso wa mtu?
 
Fanya maisha mkuu huku juu nawenyewe vitaumana kadri wawezavyo.
 
Kitu kiingine ni Mama kutamka bayana kua ndiye aliyemtabiria kua Makamu wa Rais, Je, Mama anaweza kumuundia Kamati ya kumchunguza Makonda? Mama anaweza kuweka maslahi ya kitaifa mbele kuliko kuangalia uso wa mtu?
Hapo sio rahisi nachoamini huyu jamaa atateseka na kuweweseka kwa aliyoyafanya na wala hatafurahia Mali ya utapeli aliyoipora kwa taifa hili,majivuno,kiburi,yote ni mizizi ya dhambi arudishe tuu ndio atakua free lasivyo yumo gerezani kama wafungwa wengine
 
Back
Top Bottom