Rais Samia bado anapotoshwa, hajapata washauri wenye weledi

What if mkopo una specific items ambazo wanataka utekelezeje ndio wanakopesha?..

Otherwise.,uko sahihi
 
What if mkopo una specific items ambazo wanataka utekelezeje ndio wanakopesha?..

Otherwise.,uko sahihi
Mkopo wa kupangiwa matumizi huo sio mkopo

mkopo unatakiwa kwenda wewe uombe si una resources za kuweka dhamana?

sasa Kama umeaminiwa utalipa why upangiwe matumizi?
 
Kama huo mkopo unaouzingumzia ni huu wa sh. 1.3 trilioni basi hujui lolote na bora ungekaa kimya.

Kumbuka malengo ya mkopo huu ni mampamba kwa mujibu wa wakopeshaji ni kupambana na ugonjwa wa korona (afya) na si kufanya miradi ya kimkakati kama unavyotaka wewe.

Kilichofanywa na serikali ni "kujiongeza" kwa maana badala ya kuzitumia kwenye afya peke yake ikaamua kutumia kwenye huduma nyingine za kijamii yaani elimu na maji. Kifupi ni kwamba serikali imeweza kuishawishi Benki ya Dunia kwa hoja kwamba kuboresha huduma za maji na miundombinu kwenye sekta ya elimu ni namna nyingine ya kupambana na korona.

Sasa jiulize unnawezaje kupambana na korona kwa kuboresha barabara na kukenga bwawa labumeme?
 
Mkopo wa kupangiwa matumizi huo sio mkopo

mkopo unatakiwa kwenda wewe uombe si una resources za kuweka dhamana?

sasa Kama umeaminiwa utalipa why upangiwe matumizi?
Hapo ndio sina hakika...

Haya mambo hadi uwe na taarifa then u can judge..
 
Kama huo mkopo unaouzungumzia ni huu wa sh. 1.3 trilioni basi hujui lolote na bora ungekaa kimya tu.

Kumbuka malengo ya mkopo huu kwa mujibu wa wakopeshaji ni kupambana na ugonjwa wa korona (huduma ya afya) na si kufanya miradi ya kimkakati kama unavyotaka wewe.

Kilichofanywa na serikali ni "kujiongeza" kwa maana badala ya kuzitumia pesa hizi kwenye afya peke yake ikaamua kutumia kwenye huduma nyingine za kijamii yaani elimu na maji. Kiufupi ni kwamba serikali imeweza kuishawishi Benki ya Dunia kwa hoja kwamba kuboresha huduma za maji na miundombinu kwenye sekta ya elimu ni namna nyingine ya kupambana na korona.

Sasa jiulize unawezaje kupambana na korona kwa kuboresha barabara au kujenga bwawa la umeme?
 
Soma vzr economics baba , mabeberu hawabahatishi wanapotaka lao, umembana kweli kweli amebaki kuongea ongea mambo mepesi
 
watalaamu hao hao waliweka tozo kubwa ya simu,ikapita mbaka bungeni. tukalalamika wakapunguza
Nawaza sipati jibu, kuhusu matumizi ya Tozo za miamala ya simu na benki yaliyolengwa kuborisha huduma za elimu, afya na barabara za vijijini, iwapo mkopo wa UVIKO-19 umeelekezwa huko pia!!

Ije 2025 vijijini bado hali ya huduma hizo itakuwa bado ni kama ya jana, TITAELEWANA
 
Kwani timu gaidi wanasemaje? Ngoja wafunguliwe Ufipa.
 
Kwahiyo wewe ndio unajua kuliko wataalamu wote serikalini ????

Wabongo bana.

Sio kuwa anajua kuliko hao washauri wa Rais bali ni akili ya kawaida tu kuwa kununua ndege nyingine mpya wakati hizo zilizopo hazitumiki kwa kupata faida kwani hazina routes na fierce competition kwenye Aviation industry ni kukosa weledi ambao unawazidishia wananchi machungu ya kutozwa kodi nyingi kufidia hasara zitokanazo na ATCL kujiendesha kizembe!
Viongozi wasome ushauri unaotolewa bure na wananchi kwenye mitandaoni ya jamii na kufanyia kazi ushauri wa busara wanaopewa bure!
 
Hii haitusaidii kama hatutaweza kuendeleza uchumi wetu kwa mipango endelevu....
 
K
Huu utawala kuna watu watakunywa sumu ama kujinyonga kwa wivu...
Kwa hiyo mwonekano was DAI la katiba mpya Kwa watanzania limesha Anza kuchakachuliwa na wanakijani, wanafiki na wapigania maslahi binafsi na SI watanzania watetezi halisi wa mahitaji ya watanzania wanao itaka katiba mupya kwa maslahi mapana ya taifa pendwa Tanzania.
 
Kushauri chama kisichokuwa na akili nako ni kazi. Chama kinashauriwa tawala kwa haki bila ubaguzi, hakisikiii, kinashauriwa usitegemee TISS na Polisi kupata USHINDI, hakisikiii, kinaambiwa sanduku la kura liheshimiwe litoe VIONGOZI waliochaguliwa na wapiga kura, hakisikiii ndo kwanza kinaingiza mabegi ya kura bandia! Chama kisichokuwa na akili ni ngumu sana kushauriwa.
 
Human development. Kusomesha watu unaona ni jambo rahisi? Watoto wasome chini ya miti waathirike kisaikolojia? Afya za watu...? Ni mlolongo. Huu uzi ni mwepesi kumjadili Rais ama ufutwe au mlete hoja aiondoe kidemokrasia.😀😀
 
Mabavicha bhana!..

Kwa Magufuli mlikuwa mnasema anajiamulia tu kidikteta ila kwa mama anashauriwa vibaya!
 
Kulikuwa hakuna ulazima wa kukopa ndio point yangu!!!

Kama wamepewa bure sawa lakini Kama Ni mkopo umepewa halafu utalipa halafu unapangiwa masharti Basi wewe ndio tatizo!!!
 
Wewe Ni moja ya wachumia tumbo hapa jf ulimtuka Sana Magufuli kununua ndege cash ukawa unasema Ni mwizi leo unatetea Tena Samia kununua ndege cash.

Una njaa ya tumbo umepewa chai wewe itakuwa!!
Na Wala sijabadilika bado msimamo wangu uko pale pale kuhusu Magufuli. Ila usinilazimishe nim criticize Rais SSH anapofanya mema. Siishi kwa kukariri kama wewe
 
Kulikuwa hakuna ulazima wa kukopa ndio point yangu!!!

Kama wamepewa bure sawa lakini Kama Ni mkopo umepewa halafu utalipa halafu unapangiwa masharti Basi wewe ndio tatizo!!!
Unachanganya mambo Mkuu! Hivi huoni kwenye mada yako umeshauri namna "sahihi" ya kutumia mkopo huo ni kujenga bwawa la umeme, barabara au SGR?

Lakini unadhani mkopo wa kutumia kwenye hiyo miradi unayoshauri unaweza kuwa wa "masharti nafuu" kama huu uliopatikana? Au unataka kutuambia mbali na miradi ya ujenzi wa miundombinu uliyoitaja nchi yetu haihitaji mikopo kwa ajili ya miradi kwenye sekta nyingine?
 
Unaposema hashauriwi vizuri una maana yeye mwenyewe hana uwezo hadi ategemee ushauri tu ?
 
Soma vzr economics baba , mabeberu hawabahatishi wanapotaka lao, umembana kweli kweli amebaki kuongea ongea mambo mep

Na Wala sijabadilika bado msimamo wangu uko pale pale kuhusu Magufuli. Ila usinilazimishe nim criticize Rais SSH anapofanya mema. Siishi kwa kukariri kama wewe
VIP kununua ndege cash unakubaliana naye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…