Rais Samia: Haiwezekani jeshi lifanye mauaji na lijichunguze lenyewe

Rais Samia: Haiwezekani jeshi lifanye mauaji na lijichunguze lenyewe


Rais Samia Suluhu Hassan amezungumzia mauaji yaliyotokea Mtwara ambapo maafisa wa Jeshi la Polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamisi ambapo Jeshi limeunda kamati kuchunguza tukio hilo.

Rais amesema haiwezekani Jeshi kutuhumiwa kisha liunde kamati ya kujichunguza lenyewe, hivyo amesema amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aunde kamati nyingine kuchunguza tukio hilo.

Amesema taarifa ya kamati ya polisi inayochunguza tukio hilo, italinganisha na taarifa ya kamati huru itakayoundwa na Waziri Mkuu.

Ameyasema hayo akiwa njiani akielekea Mwanza.

=======

Pia soma:
Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (25/01/2022)

Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022 (26/01/2022)


Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi (25/01/2022)

Kwa hili naunga mkono hoja 100%
 
Muarobaini wa haya matendo ovu ya Polisi ni kuundwa chombo nje ya jeshi la Polisi ambacho kazi yake itakuwa kuoversee utendaji wa jeshi!
Napongeza hatua hiyo ya Rais lakini tuangalie mbali zaidi!Malalamiko ni mengi dhidi ya jeshi la Polisi,Sasa zitaundwa tume ngapi?
Kabisa, kazi ya usalama wa Taifa ni nini?
 
N muda rafiki wa IPG kustaafu kwa amani
 
Amechemka. raia hawezi kuchumguza polisi Ila polisi anaweza kumchunguza raia. Hata ukitumia vyombo vingine vya ulinzi watacompromise tu report kutokana na mutual respect and relationship waliyonayo.
 
Kweli mambo yanakwenda kasi sana na kamanda Ziro bado yupo tu madarakani, tutaona mengi sana mwaka huu, ila hawa watu si marafiki jamani hata kule kuiba naniliu zile za kwenye masanduku baadfa ya miaka mitano wanashirikianaga?
 
Kwani polisi wanaripoti kwa waziri mkuu,? Mh. Rais Ana nia nzuri lakini kakosea njia sahihi ya kushughulikia hili suala.

Asante Mh. Rais kwa maamuzi hayo, japo unamtupia waziri mkuu kazi zisizomhusu.
Tuanzie hapa kazi za Waziri Mkuu ni zipi?Na kazi zipi haruhusiwi kufanya katika mgawanyo wa kazi zake?
 
Panapofuka moshi ndipo panapowaka moto...wenye mashaka na uzalendo wa Madame President wajipange Upya kumchafua
Sometimes, "zilongwa mbali, zitendwa mbali". Hivyo si kila asemacho mtu ndicho atendacho, tusubiri tuone. Isiwe yale ya Aquilina Aquilini.
 
Yulee alianzia juu kwenda chini,
Mama ameanzia chini anawafuata huko huko juu, hongera sana mama asiyekukubali mchawi,
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kuunda Kamati hizo ambazo hazitaleta matokeo pale ambapo wananchi wamesahau hakusaidii! Jeshi la Polisi lifumuliwe na kuundwa upya kama baadhi ya wadau walivyokwishapendekeza muda mrefu.
 
Panapofuka moshi ndipo panapowaka moto...wenye mashaka na uzalendo wa Madame President wajipange Upya kumchafua
Siku hizi urais imekuwa kazi rahisi sana. Yani kwa sasa kazi ya Rais ni kuteuwa,kutengua,kutoa salamu za rambirambi kama kuna msiba na kuwatesa wapinzani. Mambo ya mfumuko wa bei,sijui mbolea, ajira,watu kuuwawa na kupotea hiyo kamwambie Bibi ako wala si kazi ya Rais tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye Amemsikiliza mtumishi wa Mungu Askofu Bagonza maana aliyazungumza haya jwenye Big ajenda ya Nyanda... Kudos SSH na Kudos Askofu... sasa ni wakati muafaka ianzishwe independent poice complaint commission ya kudumu itayohungunza vitendo vyote vya kutojali haki za binadamu wanavyo lalamikiwa polisi... SSH tengeneza legacy sasa---kazi na iendelee
 
Amechemka. raia hawezi kuchumguza polisi Ila polisi anaweza kumchunguza raia. Hata ukitumia vyombo vingine vya ulinzi watacompromise tu report kutokana na mutual respect and relationship waliyonayo.
Hakuna kitu kama hicho subiri tukimaliza.
 
Aliposema "Msinichukulie kwa jinsia yangu" kina ndugai walicheka na kugomba meza

Sasa tunamtaka IGP, watamuelewa tu mama yetu a.k.a biushungi ama bibi tozo kutoka kule visiwa vyenye marashi ya karafuu
 
Back
Top Bottom