#Kuhusu #hotuba ya #Rais #leo;
1. Ametumia #muda mwingi kuzungumzia Chadema kuliko kilichompeleka kwenye mkutano. As the result Chadema imekua agenda kubwa kuliko mkutano wenyewe. Hapa Chadema 3, Msajili 0.
2. #Hana taarifa sahihi jamii inavyomchukulia. Aache kukumbatia "chawa" atumie vyombo vyake kujua hali halisi ilivyo mtaani. Ni tofauti kabisa na anavyojiaminisha. Watu wamemkinai mno.
3. Anadai #kuunda kikosi cha kufuatilia maoni #mtandaoni na kuyafanyia kazi. Awamu ya 5 kilikuwepo kikosi kama hicho na wakosoaji walipotea, kukamatwa na wengine kuumizwa. Je anataka kuturudisha zama hizo za giza?
4. #Anadai anapenda kukosolewa, lakini ukimsikiliza dhamiri inakataa. Angekua anapenda kukosolewa leo TEC wangealikwa. Kanisa lenye nusu ya Wakristo wote nchini linakosaje mwaliko?
5. #Chawa wamemwaminisha wanaomkosoa wanamtukana. Hawezi kutofautisha ukosoaji na matusi. Kupinga mkataba wa bandari sio matusi. Kutetea Wamasai wa Ngorongoro sio matusi. Kudai Katiba mpya sio matusi. Wapuuze wanaokuaminisha hivyo.
6. Anasema #uhuru wa #maoni una mipaka, lakini anaamini yeye ndio mwenye kipimo cha kuweka hiyo mipaka. Wanaotoa maoni yasiyomfurahisha anadhani wanatumia uhuru wao vibaya [emoji1787].
7. Waliomwambia #JPM kwamba Katiba ni kitabu kisichoweza kuleta maendeleo, ndio haohao wanaomwambia Samia kuwa Katiba ni kitabu tu, kinaweza kuwepo na kisifuatwe. Ni aibu kiongozi aliyeapa kulinda Katiba kutamka maneno haya hadharani.
8. #Watanzania wanataka #Katibampya sio elimu ya Katiba. Katiba ni vile jamii inavyotaka kujiongoza yenyewe. Watanzania wanajua wanataka waongozwe vipi. Walishatoa maoni yao Tume ya Warioba. Hawahitaji kufundishwa tena kuhusu hilo.
9. #Mabalozi walioalikwa leo kuna jinsi wamebadili mtizamo wao kwa Rais Samia. Wengi wamekua "disappointed" na hotuba yake. Ni hotuba mbovu zaidi tangu aingie madarakani.
10. #Tusubirie zile ramli za #Polisi kwamba "Taarifa za kiitelijensia zinaonesha uvunjifu wa amani, hivyo mkutano wenu umezuiwa"
Kwa kifupi Mama ameturudisha zama za "jiwe"
Sent using
Jamii Forums mobile app