Acha uchawa wako , hiyo clip iko very clear hiyo tafsisri yako ni ya kichachawa! Samia anawaambia waende kula lakini wasivimbiwe , sasa huko sio kuhalalisha upigaji?
Hawa watu wake nao wanafuata nyendo za yeye mama, anapowateua wakina RIDHWANI kutokana na ukaribu wake na baba yake na kuwaacha wenye uwezo kuliko yeye anadhani hao mawaziri nao hawawezi kufanya hivyo yeye anavyofanya? Kiongozi anatakiwa aoneshe mfano.
Magufuli alipiga marufuku watendaji kufanya safari za nje kiholela na yeye akaonesha Mfano wa kutokuwa mzururaji!! Kikwete alikuwa mtu wa kwenda kubembea na watendaji wake nao wakawa wanapishana Airport nao wakifuata nyayo zake!!! Utakalofanya wewe Samia ndio wafuasi Wako watafanya pia!! Badala ya kupiga mayowe unatakiwa uongoze kwa kuonesha Mfano. Unatakiwa uwe RAIS wa vitendo na Maneno machache! " UKUBWA WA PUA SIO WINGI WA MAKAMASI."