Rais Samia leo kafanya kosa kubwa sana. Huwa hatukunjui makucha kwa waliotukosea

uko sawa but kila mtu ana mbinu zake kwe kudeal na mamb km haya
 
Apindue tu meza ili minyukano ianze mapema, vita ni vita muraaa..........
 
Nimependa rais alivyofanya, huyo mgogo ana shida sana. Ni mbabe ni mkatili kupita kiasi, hivi umeshasahau "What goes around comes around? Ndugai anayo mapungufu mengi sana, Uongo wake kuwa hiyo video imetengenezwa imemtokea puani...Mzandiki, ameumiza wengi sana.
 
Siasa ni kazi kubwa sana. Nadhani hajui kabisa siasa. Hoja inajibiwa kwa hoja na siyo kushambulia wala kutishana
 
Mtego upo kwa kisu cha mwenyekiti😅 lazma kipite na shingo ya Sabufa kwa kumuondoa chamani
 
Tz bado sana, marekani spika wa bunge aliichana hotuba ya raisi waziwazi kisa tu hawafanani kimitazamo huku spika anaomba msamaha hadi huruma
Huku sio marekani mzee😅 unaweza onesha umwamba raisi akatulia zake na wapambe wakakutia sumu bila kuelewa unadefedi kiroho safi
 
Tz bado sana, marekani spika wa bunge aliichana hotuba ya raisi waziwazi kisa tu hawafanani kimitazamo huku spika anaomba msamaha hadi huruma
Huku sio marekani mzee😅 unaweza onesha umwamba raisi akatulia zake na wapambe wakakutia sumu bila kuelewa unadefedi kiroho Safi au unavuliwa vyeo chamani unatimuliwa kwenye system na kuwa mtu wa kawaida tu kama 7YA
 
Familia moja wakigombana shika jembe ukalime
 
Mkuu hii point ya kimkakati wa ki'c.i.a.....[emoji16][emoji16]
 
Mama ilikua kama muda mfupi katoka sikiliza taarabu ametembeza mipasho ya kutosha.

Ila CCM ni wanafiki, nimesikia wakaanza kuimba tuna imani na mama samia, oya x2 , Samia kweli x2 ahahah ahha. Mipasho ilivyokolea
Kama umemsikia baada ya wimbo huo alivyosema, "wimbo huo unatukumbusha mbali sisi wanaccm wakongwe"!
Jee unajuwa ni wapi? Ni kuwa wimbo huo uliimbwa na halmashauri kuu kwenye mgogoro wa kumtema Lowassa na wakaimba "tunaimani na Lowassa".
Mama anajua unafiki wa ccm na hao wenyeviti wake, wanaweza imba hivi na kesho wanafanya vile
 

Ahahah nilisikia hii kitu
 
Siasa zetu ni za kufuata mkumbo au upepo na kujikomba. Mama kusema hadharani ndiyo njia nzuri ya kushinda kwa sababu wote wamesikia na watashambulia kweli kweli.
 
Fukuto huko ndani ni kali sana
Nakubali haujui hasa ukubwa wake. Wako wakijani wengi tu mchana ni kondoo usiku ni koboko.
Mama awe mwangalifu na asiogope kufanya lililo la haki.
Ni kweli wapinzani somehow ni positive kwa Samia ilhali kuna kijani wengi wako negative kwake.
 
aanzishe chama CCM igawanyike, ila sidhani kama atapata wafuasi....sema Ndugai hakujenga marafiki, alijenga ubabe kumuegemea Magufuli
 
Spika mwenye integrity hawezi kukubali kufanywa mtumishi wa Mwenyekiti wa chama chake. Na Mwenyekiti hawezi kumfukuza kwenye chama bila ushirikiano wa wenzake. Hiyo si rahisi kwa mtu anaejulikana kwa uadilifu wake. Ila kama ulijiweka ki utumishi utumishi hivi basi utaondoka maana wenzako itakuwa rahisi kuwashawishi wakutose. Aidha, Spika mtenda haki anakuwa anakubalika sana kwa raia ambao hawatafurahi kuona anaonewa kwa sababu ya msimamo wake. Bahati mbaya Spika wa sasa alijiweka kama mtumishi na hiyo ndio inayomponza.

Amandla...
 
Hata Mimi kwa ushauri rais asingetema nyingi,angenyamaza kimya harafu baada ya mwezi mmoja angeibukia kuvunja baraza la mawaziri na kuipanga safu vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…