Rais Samia leo kafanya kosa kubwa sana. Huwa hatukunjui makucha kwa waliotukosea

Rais Samia leo kafanya kosa kubwa sana. Huwa hatukunjui makucha kwa waliotukosea

Kwa hali ilivyo Spika Ndugai akiendelea kuwa na Uspika kwa masaa mengine 48 atakuwa hasomi alama za nyakati.. Mkuu wa nchi akishakosa imani na wewe unapaswa kujiuzulu..
Asipojiuzulu atalazimishwa kujiuzulu.. Hadhi ya Rais wa nchi ni muhimu kuliko maisha ya mtu..😎
Ampishe SSH aendelee na kazi..
Huu ni wakati wa SSH ' to put her house in order'.. katika uongozi wa nchi hakuna kitu muhimu kama 'Loyalty'..
Yule anatoka muhimili mwingine....
bara bara anayoweza kuipata kumuwajibisha ni kupitia chama maana yy ni mwenyekiti wake
 
Yule anatoka muhimili mwingine....
bara bara anayoweza kuipata kumuwajibisha ni kupitia chama maana yy ni mwenyekiti wake
Mkuu ras jeff kapita Rais ana madaraka makubwa sana .. anaweza kuwatumia wazee ndani ya chama kumshinikiza kutumia busara kujiuzulu ili kumraisishia kazi Rais.. pia Taasisi ya Urais inaweza kutumia 'misuli' yake kumshinikiza ajiluzulu .. hivyo kwa vyovyote inawezekana..
Hakuna kitu kinaitwa mhimili mwingine au kujitegemea mhimili.. Rais ni sehemu ya Bunge kikatiba ijapokuwa si mbunge lakini ndiyo anayeendesha mambo..
 
Leo Samia amefanya kosa kubwa sana kwa kitendo chake cha kujibu mashambulizi kwa Ndugai.

Hii mbungi ya Ndugai ndo ilikuwa chance kubwa ya mama kuwajua maadui zake kwa kirefu.

Mama angepaswa kuwa soft kabisa kwa siku ya leo. Na ingependeza kama angeanza kumshukuru kwa dhati Ndugai kwa kuomba msamaha.

Imagine kama angeongea haya maneno leo "Namshukuru sana kaka yangu Ndugai kwa kuonesha ukomavu na kurekebisha kauli yako ili tuendelee kujenga taifa la umoja na mshikamano"

Hivyo ndivyo mama angepaswa kusikika leo. Diplomatically and soft tone. Hii ingemfanya hata Ndugai aone kama amesamehewa kirahisi.

Hiyo maana yake ni kumpa adui false signal, halafu sasa akishajaa kwenye comfort zone, ndio unafanya severe atacks.

Kwa case kama hii, Samia amgeweza kuwa soft sana kama nilivyosema hapo mwanzo halafu baada ya kama wiki mbili au tatu mambo yakishapoa, ndio anafanya fujo za kuvunja baraza la mawaziri ikifuatiwa na taratibu za Ndugai kuvuliwa u spika.

Sasa kwa hii move ya kukunjua makucha asubuhi na mapema, maana yake ni kama ametangaza vita wazi wazi na kambi ya kina Ndugai kitu ambacho kwangu mimi tayari ni udhaifu kwa sababu sasa Ndugai ni kama naye hawezi kutulia tu hivi abondwe, lazima atataka kujibu mashambulizi na kurejesha nguvu yake hata ingekuwa mimi.
Babu kwa nguvu na aliyonayo Mwenyekiti wa chama na Rais wa nchi hii hata uchakalike vipi atakubonda tu labda Mungu mwenyewe aingilie kati.
 
Hicho kitu hakiwezekani kabisa.. Rais ndiyo Mwenyekiti wa Chama na ndiye anayeongoza Kamati Kuu hivyo hapo hana lake..
Sio rahisi hivo mkuu... Hiyo move inawezekana ki maandishi ila utekelezaji wake sio rahisi.

Kwa mfano katiba inasema at least 2/3 ya wabunge wakubaliane, what if isipopatikana? What next? Maana yake Ndugai atabaki spika, then what?

Yaani mwisho wa siku huu mziki ni mzito
 
Mkuu ras jeff kapita Rais ana madaraka makubwa sana .. anaweza kuwatumia wazee ndani ya chama kumshinikiza kutumia busara kujiuzulu ili kumraisishia kazi Rais.. pia Taasisi ya Urais inaweza kutumia 'misuli' yake kumshinikiza ajiluzulu .. hivyo kwa vyovyote inawezekana..
Hakuna kitu kinaitwa mhimili mwingine au kujitegemea mhimili.. Rais ni sehemu ya Bunge kikatiba ijapokuwa si mbunge lakini ndiyo anayeendesha mambo..
Ndugai hawezi jiuzulu aisee.. Take it from me. Yaani uwarahisishie kazi?
 
uko sawa but kila mtu ana mbinu zake kwe kudeal na mamb km haya
Anyway, ila kumbuka tu huwa kuna General na Specific rules.. Mara nyingi ili huwe kwenye safe side, tumia General rules ambayo viongozi wengi huwa wanatumia..
 
Spika mwenye integrity hawezi kukubali kufanywa mtumishi wa Mwenyekiti wa chama chake. Na Mwenyekiti hawezi kumfukuza kwenye chama bila ushirikiano wa wenzake. Hiyo si rahisi kwa mtu anaejulikana kwa uadilifu wake. Ila kama ulijiweka ki utumishi utumishi hivi basi utaondoka maana wenzako itakuwa rahisi kuwashawishi wakutose. Aidha, Spika mtenda haki anakuwa anakubalika sana kwa raia ambao hawatafurahi kuona anaonewa kwa sababu ya msimamo wake. Bahati mbaya Spika wa sasa alijiweka kama mtumishi na hiyo ndio inayomponza.

Amandla...
Nakubaliana na wewe mkuu
 
aanzishe chama CCM igawanyike, ila sidhani kama atapata wafuasi....sema Ndugai hakujenga marafiki, alijenga ubabe kumuegemea Magufuli
Jamaa ana ubabe, hata hapa sidhani kama atakubali kushindwa kirahisi.. muda utaongea
 
Nakubali haujui hasa ukubwa wake. Wako wakijani wengi tu mchana ni kondoo usiku ni koboko.
Mama awe mwangalifu na asiogope kufanya lililo la haki.
Ni kweli wapinzani somehow ni positive kwa Samia ilhali kuna kijani wengi wako negative kwake.
Tatizo la mama alikuwa anajua threats ni Mbowe na Chadema. Ametumia nguvu nyingi sana ku deal na Mbowe akasahau mtumbwi wake umatoboka matundu
 
Mkuu hii point ya kimkakati wa ki'c.i.a.....[emoji16][emoji16]
Hahahahahaa.. strategy za ku deal na maadui unaokula nao..

Ndo mana unaambiwa, muogope sana mtu anayekuchekea. Wengine huwa ni chambo cha kukufanyia ubaya wa kutisha..
 
Back
Top Bottom