Rais Samia mbona hakubali tatizo nini?

Rais Samia mbona hakubali tatizo nini?

Kwa upande wangu awamu hii imenikera katika Tozo...makato naona makubwa imefikia hatua ukiingia muamala chini ya laki sitoi nitaitumia kwa mambo madogo Hadi iishe
Ni matokeo ya matatizo ya Jiwe,
 
Hotuba zake tu hawezi kujieleza rejea mahojiano Kati yake na kikeke anapanic sana kujenga hoja ni tatizo sana, hata maamuzi mengi inaonekana Kuna watu nyuma yake mzigo wa Tozo ni kwere

jombaa mfumuko wa bei uliopo siyo wa mchezo mchezo na tena mfumuko ulianza kabla hata ya vita kwakauli yake amesama "Na bado kila kitu kitaendelea kupanda" sasa umsikilize mtu wa namna hiyo wa kazi gani si utapata dhambi ya kumtukana kimoyo moyo tu.
Juz aliitisha kikao Cha dharura usiku eti kujadili upandaji wa mafuta lakin kikao chenyewe kaita kuwaambia haohao walio shindwa eti watafute ufumbuzi yeye Hana anacho changia chochote kimawazo/ kimaamuzi
 
Achana nao hao.Wengi wa wanaoonesha chuki kwa SSH ni masikini.Hawa walikuwa wanafurahia matajiri,wafanyabiashara na watumishi wa umma kuumizwa na kufanyiwa dhulma.Kwa akili zao nyembamba walidhani hayo makundi yakifanyiwa udhalimu ndiyo watalingana nao kuuishi ufukara.Akili za kimasikini kama mpendwa wao jiwe!Tell them to go to hell!
Are u serious? Wengi ni maskini wasiomkubali, hivyo kwako ni sawa kukubalika na matajiri achukiwe na maskini!!! Jenga hoja kama GT, Je Kwa wastani, kati ya maskini na matajiri wengi ni kundi Gani? TANZANIA Kuna matajiri wangapi, TAFSIRI ya maskini na TAJIRI ni ipi? Unvyowaza vigezo vip Ukiwa navyo unakuwa maskini au TAJIRI?
 
Methali kama "aliye juu mngoje chini" zimetufanya tuwe na roho za kichawi. Jirani yako akiwa tajiri unatamani afilisike badala ya kutamani ufike alipo
 
Are u serious? Wengi ni maskini wasiomkubali, hivyo kwako ni sawa kukubalika na matajiri achukiwe na maskini!!! Jenga hoja kama GT, Je Kwa wastani, kati ya maskini na matajiri wengi ni kundi Gani? TANZANIA Kuna matajiri wangapi, TAFSIRI ya maskini na TAJIRI ni ipi? Unvyowaza vigezo vip Ukiwa navyo unakuwa maskini au TAJIRI?
Umeanza lini kunichagulia la kuwaza na kuandika?
 
Kwanini watu hawasemi ukweli kuwa Samia hakubaliki Bali wanapiga propaganda tu?

Kuanzia masokoni, vijiwe vya kahawa,mitaani ,maofisini mama hakubaliki ,shida Ni nin jaman?

Juzi tukiwa ofisini karibu staff members Kama 15 ,ikawashwa redio ,mama alikuwa anahutubia ,sijui Ni Tabora hiyo, aisee staff walikuja juu ,redio izimwe ,Hakuna anachoongea Cha maana ,Walidai hivo,

Huku wakisema Wamemis sana Hotuba za Jpm ,

Hii hali niliichukulia kawaida,lkn nenda hata masokoni, mfano Mabibo sokon, manzese, nenda machinjion vingunguti, Mama anazungumzwa vibaya, anaonekana anafeli sana

Wananchi wengi wanaamini maendeleo yanaenda kwa mwendo wa Kobe,

Wanaamini wez wamerudi serikalin,

Wanaamini Jpm alikuwa mtetez wao,

Wanaamini Kuna kund limemuondoa mwendazake

Kiukweli hata wewe ulipo hapo Kama mpo 10, jaribu ufanye utafiti,uone Ni namna gan mama anakubalika ,

Utaleta majibu hapa ,

Ninachojiuliza huyu mama kwann hakubaliki ,je sio presidential material?

Au Hana maono na nchi hii Kama alivyokuwa Jpm?

Ukiangalia jins Jpm alivyotuvusha kwenye Corona , unaona KABISA angekuwa huyu mama tungekuwa wapi?

Kuna mtu huwa ananiambia msimamo wa chanjo kwa watanzania ndio Iman ya Watu kwa Jpm ,

Hadi Sasa propaganda za chanjo zimefeli , huku majority wakiendelea kuamini falsafa za Jpm ,ambazo hata Korea wameanza kuzitumia

Swali kwann huyu mama hata Hotuba zake zinapuuzwa ,?

Kipind Cha JPM watu had kwenye bodaboda wanatega masikio ,waone mwamba ataongelea mradi gan mpya, mwizi gan atatumbuliwa,

Huyu mama Hotuba zake zinapuuzwa ,kwasasa watu wapo tayari kumsikiliza haji manara na sio raisi,tatizo nn?
toa ushahidi usitopoke
 
Unachokisema ni kweli. Kundi kubwa halimkubali. Walio karibu naye hawampi yote ili kilinda vibarua vyao.

Tatizo la Samia ni kuwa hana agenda yeyote inayovutia watu kwakua hakujiandaa kuwa Rais na watu hawakumchagua kutokana na agenda yake hivyo inakua vigumu kweli kumkubali na mambo yake.

Atatumia nguvu sana kukubalika.
 
Kwanini watu hawasemi ukweli kuwa Samia hakubaliki Bali wanapiga propaganda tu?

Kuanzia masokoni, vijiwe vya kahawa,mitaani ,maofisini mama hakubaliki ,shida ni nini jamani?

Juzi tukiwa ofisini karibu staff members Kama 15 ,ikawashwa redio ,mama alikuwa anahutubia ,sijui ni Tabora hiyo, aisee staff walikuja juu ,redio izimwe ,Hakuna anachoongea cha maana ,Walidai hivo,

Huku wakisema Wamemmiss sana Hotuba za JPM ,

Hii hali niliichukulia kawaida,lkn nenda hata masokoni, mfano Mabibo sokoni, Manzese, nenda machinjion Vingunguti, Mama anazungumzwa vibaya, anaonekana anafeli sana

Wananchi wengi wanaamini maendeleo yanaenda kwa mwendo wa Kobe,

Wanaamini wezi wamerudi serikalini,

Wanaamini Jpm alikuwa mtetezi wao,

Wanaamini Kuna kundi limemuondoa mwendazake

Kiukweli hata wewe ulipo hapo Kama mpo 10, jaribu ufanye utafiti,uone Ni namna gan mama anakubalika ,

Utaleta majibu hapa ,

Ninachojiuliza huyu mama kwann hakubaliki ,je sio presidential material?

Au Hana maono na nchi hii Kama alivyokuwa Jpm?

Ukiangalia jins Jpm alivyotuvusha kwenye Corona , unaona KABISA angekuwa huyu mama tungekuwa wapi?

Kuna mtu huwa ananiambia msimamo wa chanjo kwa watanzania ndio Iman ya Watu kwa Jpm ,

Hadi Sasa propaganda za chanjo zimefeli , huku majority wakiendelea kuamini falsafa za Jpm ,ambazo hata Korea wameanza kuzitumia

Swali kwann huyu mama hata Hotuba zake zinapuuzwa ,?

Kipind Cha JPM watu had kwenye bodaboda wanatega masikio ,waone mwamba ataongelea mradi gan mpya, mwizi gan atatumbuliwa,

Huyu mama Hotuba zake zinapuuzwa ,kwasasa watu wapo tayari kumsikiliza haji manara na sio raisi,tatizo nn?
 
Binafsi nilichokiona watu bado wanaamini katika RAIS MWANAUME. Ila kwenye kufanya kazi vizuri MAMA SAMIA yuko Far better than MAGUFULI. NAMKUBALI KINOMA NOMA JPM ila mama Samia anatumia Busara, Hekima, nidhamu na Utu katika kuongoza. Kama huyu mama angekuwa Rais mara baada ya KIKWETE amini nakwambia hii nchi ingekuwa mbali mno, kwanye Sekta nyingi sana, Ajira, Biashara, Uvuvi, Kilimo nk.

Thank You Hon. Pres. Samia.

Watu wamezoea vitisho.
You have said it better
 
wabongo wekeni wazi tu msizunguke! Mama ni president material kinoma, ana akili kubwa sio local bali global, hotuba zake ni nzuri na za kisomi na anaenda na agenda za nchi kwa wakati , anajenga nchi kwa kasi, ni msomi na mzoefu wa mashirika ya kimataifa, miradi ya Mwendazake ameisimamia inasonga kama kawa japo hatujui itaisha lini ila wasiomkubali bimkubwa tatizo ni

1. Mama ni mwanamke anaeongoza nchi yenye mfumo dume ulioota mizizi! baba ni kichwa cha familia ndio utamaduni wetu. wanaume inawachoma sana kuongozwa na mwanamke ila hawasemi hadharani
2.Mama ni muislam wakati inadhaniwa ilikuwa zamu ya wakristo kuongoza baada ya JK ila Mwendazake akakatika kama mshumaa ghafla bin vuu mtu kajengewa karo.
3.Mama ni Mzanzibari na wabara wengi hawaamini weledi toka visiwani kuongoza nchi
4.Mama sio Rais aliechaguliwa kupitia sanduku la kura zenye ushindani wa vyama vingi hasa kupitia mpambano na Tindu Leso na Miwani Makengeza bin Mbowe
5. Watu wanachukia waliotengeneza katiba kuwa Makamu ni Rais bila uchaguzi boss wake akiaga dunia kwa njia ya kawaida au kusafirishwa kuzimu
6. Mwendazake alikuwa na kauli za kibabe sasa Mama kuna siku alisema ukinikuna nakupuliza ukizingua nakuzingua na kukuparura kauli hizi zilitafsiriwa ni mpole na watu wanataka Rais awe mkali kwenye kauli na vitendo wakiamini wizi umezidi serikalini!
 
CCM itapata shida sana ikiwa itaamua kumsimamisha SSH kwenye uchaguzi 2025 (nadhani watamshauri apumzike), ukweli ni kwamba hakubaliki, sio kwasababu hafanyi kazi bali ni wananchi hawamwelewi tu na hata wanaojaribu kumpaka mafuta huku jukwaani wanalijua vizuri hilo.

Itawalazimu waibe kura kwa kiwango ambacho hawajawahi kufanya tangu uhuru wa Tanzania na kwenye viti vya ubunge upinzani utazoa sana viti.

NB: Sidhani kama CCM watafanya kosa la kumsimamisha SHH, nafikiri atashauriwa aache kugombea kwa masilahi mapana ya chama
 
Kipindi Cha jiwe hata hiki alichokiandika alikuwa anajiuliza mara mbili aandike au aache kwa hofu ya kujulikana na kutekwa,

Leo hapa anaharisha bila hofu yoyote.
Watu wamesahau haraka sana, jinsi walivyokuwa wakiishi kwa hofu ya kutekwa na kupotezwa.
Tukumbuke rais naye ni binadamu, hajakamilika kwa mambo yote. Tujifunze pia kuvumilia mapungufu ya wengine.
Laikini pia kwa hulka ya binadamu, hata Mungu akitupatia malaika atuongoze, bado tutamlaumu na kumkosoa vikali.
 
wabongo wekeni wazi tu msizunguke! Mama ni president material kinoma, ana akili kubwa sio local bali global, hotuba zake ni nzuri na za kisomi na anaenda na agenda za nchi kwa wakati , anajenga nchi kwa kasi, ni msomi na mzoefu wa mashirika ya kimataifa, miradi ya Mwendazake ameisimamia inasonga kama kawa japo hatujui itaisha lini ila wasiomkubali bimkubwa tatizo ni

1. Mama ni mwanamke anaeongoza nchi yenye mfumo dume ulioota mizizi! baba ni kichwa cha familia ndio utamaduni wetu. wanaume inawachoma sana kuongozwa na mwanamke ila hawasemi hadharani
2.Mama ni muislam wakati inadhaniwa ilikuwa zamu ya wakristo kuongoza baada ya JK ila Mwendazake akakatika kama mshumaa ghafla bin vuu mtu kajengewa karo.
3.Mama ni Mzanzibari na wabara wengi hawaamini weledi toka visiwani kuongoza nchi
4.Mama sio Rais aliechaguliwa kupitia sanduku la kura zenye ushindani wa vyama vingi hasa kupitia mpambano na Tindu Leso na Miwani Makengeza bin Mbowe
5. Watu wanachukia waliotengeneza katiba kuwa Makamu ni Rais bila uchaguzi boss wake akiaga dunia kwa njia ya kawaida au kusafirishwa kuzimu
6. Mwendazake alikuwa na kauli za kibabe sasa Mama kuna siku alisema ukinikuna nakupuliza ukizingua nakuzingua na kukuparura kauli hizi zilitafsiriwa ni mpole na watu wanataka Rais awe mkali kwenye kauli na vitendo wakiamini wizi umezidi serikalini!
Jiwe alikuwa mkali, lakini bado watu walikuwa wanaiba. Wasichokijua watu ni kwamba mama siyo mkali wa kauli ila kwa vitendo. Kuna baadhi wamesha anza kuonja joto lake la ukali wa vitendo. Inaonekana Wabongo wengi wanapenda kiongozi anayepayuka/ anayetoa vitisho hovyo hadharani!
 
staff ya wapi hiyo? Ni bora huyu mama mara mia japo anapuyanga kuliko Jiwe.

Uhuru tu wa kufanya mambo yangu bila hofu ya kutekwa inatosha, mama dhibiti vibaka tu na hawa panya road kura tutakupa
Hujaelewa kwanini watu hawamuelewi huyu mama, hao panya road waliyorudi tena katika kipindi chake ni moja ya vitu ambavyo huwafanya watu kutomuelewa huyo mama.

Kuna mambo mengi ya hovyo yamerudi na madili haramu yamerejea, sasa mama ameshindwa nini kusahisha makosa ya mtangulizi wake bila kurudisha makosa aliyoyashughulikia mtangulizi wake?

Leo unasikia wauza unga wamerudi kwenye biashara zao kama mwanzo maana kuna kipindi waliacha, sasa unajiuliza hawa wauza unga nao walikuwa wanaonewa na Magufuli au vp? Mara utasikia jamaa fulani alifulia maana alicha kupiga deal zake haramu kipindi cha Magufuli ila sasa karejea, unabaki unajiuliza hupati jibu.
 
Kipindi Cha jiwe hata hiki alichokiandika alikuwa anajiuliza mara mbili aandike au aache kwa hofu ya kujulikana na kutekwa,

Leo hapa anaharisha bila hofu yoyote.
Magufuli asingetaka malaika wafunge mitandao kama ingekuwa watu hawatumii mitandao kumkosoa kwa kuogopa.
 
Samia anacheza vzr, lakin ni kutokukubalika TU kwa watu wachache ambao hawini kua mwendazake kafa, tusiishi kwa mazoea, Kwan hata akifanya mangapi Bado watasema TU kua anajipendekeza.
Hata Jiwe alikuwa hakubaliki na wote kuna ambao walikuwa wanamchukia ila tofauti kwa huyu mama ni kwamba haelewiki, hata kama anafanya mazuri ila ubaya wake ni kwamba utawala wake ndipo mambo mengi ya hovyo yanarudi kwa kasi vitu ambavyo vilidhibitiwa kama sio kupungua.

Nidhamu imeshuka kwa watumishi na ukiuliza unaambiwa kipindi cha Magu kulikuwa na nidhamu ya uoga ila yeye hadi sasa hatuoni hatua anazochukua kuweka nidhamu isiyo ya uoga, deal haramu zinarejea na hata uharifu badala ya kuzidi kupungua unarudi ule wa mwanzo.
 
Back
Top Bottom