Rais Samia nakushauri watose sasa Spika (Tulia) na PM (Majaliwa), sakata la bandari limekumaliza kisiasa!

Rais Samia nakushauri watose sasa Spika (Tulia) na PM (Majaliwa), sakata la bandari limekumaliza kisiasa!

Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.
saa-mia kama saa-mia baada ya kusoma ushauri wako
 
Attachments

  • file-my-nails-https://jamii.app/JFUserGuide-off.gif
    file-my-nails-https://jamii.app/JFUserGuide-off.gif
    942.6 KB · Views: 3
Wewe mleta hoja sikuelewi kabisa... yaani atoswe spika kwa kosa gani?
 
What if hao unaowataja hawakupewa nafasi ya kushauri, waliletewa majibu mezani na kuambiwa iwe hivyo...?
Kwanini waliapa? Unaapaje ukishika Katiba na kitabu kitakatifu kisha, ikija kwenye kuwajibika eti unasema waliletewa, for real?
 
What if hao unaowataja hawakupewa nafasi ya kushauri, waliletewa majibu mezani na kuambiwa iwe hivyo...?
Na wakakaa kimya! basi lazima watolewe kafara kuokoa jahazi, ndivgo kisiasa tunavyoendaga
 
Nia njema huwa inastand out yenyewe. Matendo ya Samia Yana aksi Nia yake .tulimuonya tangu mwanzo kuwa amejizunhushia watu wanaotiliwa Shaka akakomaza shingo so avune alichooanda.
 
Inept...

Au tutumie neno gani zuri?

Au tuseme wanampotosha as she's "inept"

Au tuseme the corrupt system ya ccm...

..au tusemeje
 
Kuna mengi bado yana simmering kama uji uliopo jikoni tukiyafahamu tutalia...Hebu tujiulize mambo ya Gas yameishia wapi? Gas ipo au hakuna? Jee inavunwa hivi sasa? Nani anavuna na inaenda wapi?
 
Hakuna yeyote aliyemwaribia kajiharibia yeye mwenyewe.Mbn wakati wa Magu hii mikataba ilitupiliwa mbali iweje yeye aikubali?Na alishaambiwa kabla kuhusu hii mikataba ya hovyo
Lini mikataba ilijadiliwa tofauti na huu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni mingine ikiletwa mtasema imechakachuliwa.
Walau Nuru ya uwazi inajipenyeza
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.
Mama, mamaaa haya Sasa umeingizwa Chaka raia watanganyika hawakuelewi. Unapoteza badili gia usione nishai
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.
Jamani tuacheni na rais wetu, bado tunatumia pesa na per diem kwa kuendelea kuelimisha mikoani kwa wadanganyika wenzetu, kauli mbiu ya kanda ya ziwa ni mabinti wa kiarabu ni wazuri sana wakija tutachanganya rangi," CCM tupo tuition kanda kwa kanda mkoa kwa mkoa, kaya kwa kaya, mpaka waelewe ibara ya 21 kuwa mkataba una ukomo,

chezea ccm wewe, tumeuza bandari kwa toyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.
Akimtoa tulia ataendelea kula mpunga maisha yake yote. majaliwa atakuwa hana kibarua kwasababu amebakisha miaka 2 tu arudi kwao. ila wote huwa sitamani hata kuwaangalia mara mbili.
 
Ukiangalia kwa jicho la umakini hili suala utagundua kwamba waliomuingiza chaka huyu mama ni wabunge wanaoongozwa na njaa kali na ulafi kushindwa kupingana wao kwa wao sababu sasa hivi mle ndani wapo wao tu so wanaona wakienda tofauti na wengine raisi atawaona wasaliti na atakuwa hawabebi awamu ijayo kumbe sometimes yeye rais alitegemea challenges watakazopeana kwenye mjadala wa hili jambo ndizo zimuongoze

Na hii yote ni kutokana na wanajua hawapendwi na wananchi wao kwa sababu kugombea kwao ubunge haikuwa ili wakawasemee shida zao bali ilikuwa ni chance ya kupata ukwasi
Kuna anayeitwa Jerey Silaa, mbunge feki wa jimbo la Ukonga. Baada ya kushindwa kufanya chochote kwenye jimbo, na kusoma alama kuwa ameshakataliwa na wananchi kwa asilimia zote, ndani na nje ya chama chake, yeye ameamua akazurure nchi nzima kuukingia kifua mkataba haramu wa kuuza nchi.

Huyu bwana ana ufahamu wa kiwango cha chini kabisa. Kama anadhani ubunge unatoka kwa Rais, sisi wanaCCM wa jimbo la Ukonga tutankaanga kwenye mafuta yake mwenyewe. Jimboni kwake kila kitu kimekwama, serikali za mitaa zimekufa, serikali imelitelekeza jimbo, lakini mbunge anajivika ubalozi kutetea wezi na matapeli.
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.
Hayo ni mawazo yako
 
Mruma asingejitambulisha Kama profesa mbele ya vile vitoto vya kizungu. Angesema from foo alipata div foo Kama waziri Fulani aliyepata F ya uraia, F ya hesabu na F ya kiingereza.

Kujitambulisha Kama Prof kumewavua nguo maprof wengi wa kitanzania.

Mruma na dada Joy hawachekani japo mruma anajua ung'eng'e kiasi.
Haahaaa eti japo Mruma anajua ung'eng'e kiasi. Ukweli ni kuwa watanzania wengi wanaojiita wasomi wanajua kiingereza cha ugoko wakati wa mjadala wa amani, lakini wanapokuwa kwenye mazingira ya mgogoro ni aibu ya hatari.

Halafu ukiwakuta hao maprofesa wetu wanafundisha vyuoni wanajifanya wanakijua sana kiingereza, na wanatoa elimu katika mazingira ya kukomoa na jazba, sababu mojawapo ni kwakuwa wana uelewa duni wa hiyo lugha.

Hiyo kesi imetuacha wazi kwenye suala la kupenda kusoma kuanzia wanaojiita wasomi, hadi wasio na elimu kabisa. Mruma alikuwa anajaribu kuongea kwa jazba na kuleta ile jeuri aliyowajaza Magufuli wakati ule. Alichokiongea Mruma ndio nimejua kwanini hatukuambulia chochote kwenye kile kikao cha miezi karibu mitatu ya siri kubwa kuhusu makanikia na madini yetu chini ya Profesa Kabudi.
 
Hakuna yeyote aliyemwaribia kajiharibia yeye mwenyewe.Mbn wakati wa Magu hii mikataba ilitupiliwa mbali iweje yeye aikubali?Na alishaambiwa kabla kuhusu hii mikataba ya hovyo
Hiyo mikataba iliyotupiliwa mbali wakati wa Magufuli si ndio hiyo imefanya Profesa Mruma anaibika huko kwenye mahakama za kimataifa, na kesi tumeshindwa na hivi sasa tunatakiwa kulipa zaidi ya 200b? Hujaona Profesa Mruma anaulizwa na mjukuu wake amebaki kuongea mambo ya ajabu hadi imeishia kuwa aibu?
 
Back
Top Bottom