Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Rais Samia: Nikijua wewe ni dhidi yangu(Serikali) siwezi kukushirikisha. Utatumia sheria zote za Kimataifa, nitatumia za ndani kuku-bar

Wataalam ndiyo injini ya kuleta maendeleo katika nchi.
Wataalam hawatakiwi kujipendekeza na kuwalamba nyayo wanasiasa.
Mtaalam anapotoa maoni au kukosoa lazima asikilizwe siyo kumchukia au kumuita adui.
Hajakataa kazi yao kikatiba ila ni ukweli Tanganyika law walianza kuonekana kama sehemu ya wanaharakati kujificha sote tunajuwa.
 
Duh...!, kwa kauli kama hizi, kiukweli kabisa kuna vitu, ili twende salama, Mama lazima asaidiwe, kwa kuelimishwa kuwa ushirikishwa sio hisani, sio favor, sio option, sio choice, ushirikishwaji ni haki, duty and responsibility, yaani ni wajibu!, kama ulivyo utii kwa mamlaka!. Unaweza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua majirani, ukiisha jikuta unaishi na jirani fulani, ni lazima ushirikiane nae ndipo muishi vizuri.
Sasa leo ndio nimeanza kuielewa hii TLS ya Hosea!.
Duh....!.
Haya...
P
TLS imesingiziwa huu ujumbe uwafikie woote wenye ndoto za Urais 2025 ndani ya ccm na nje ya ccm.

Anasema atatumia sheria za ndani ukweli ni kuwa hapo kwenye sheria weka neno( Dola) kuwashughulikia wanaompinga.

Hii kauli ya leo ni zaidi ya hayati.

Sijui kama alitamka kwa kukusudia au amechokoza nyuki ili aone wapi watawashwa.
 
Ndiye aliyejenga mfumo mbovu tulionao. Bila ya mfumo huu tungekuwa mbali sana

Ni kweli tuzungumzie mgao wa umeme na maji wa sasa, unaotokana na teuzi za kujuana bila ufanisi na kuwajibishana, muda wa Nyerere umeshapita hana anachoweza kubadili sasa ila sisi tuliobaki ndio wajibu wetu hasa hasa Mama samia. Nyerere pamoja na uwezo wa kidikteta aliokuwa nao hakukubali hata kujengewa nyumba ya kisasa kifupi hakuwa fisadi tofauti na sasa.
 
Nyerere hayupo zaidi ya miaka ishirini,kwanini mnashindwa kuuvunja mfumo unaoita mbovu ulioasisiwa na Nyerere?
Mnashindwa hata kujenga matundu ya choo..mkiulizwa oh shida Nyerere..nonsense!
Mfumo uliojengwa na Nyerere unawanufaisha vigogo. Hauvunjiki.
 
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake

Kwa mfano Tanzania, miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo frankly speaking ilikuwa siyo chama cha Wanasheria, kilikuwa chama cha Wanaharakati na mapambano yao yalikuwa ni dhidi ya Serikali.

Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo! Mpaka unioneshe kwamba am here to support you, I'm here to serve a country, I'm here kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu.

Nikikuona una sura hiyo nitakushirikisha, nikikuona una sura ya uadui nami sitaweza kukushirikisha. Utatumia Sheria zote za Kimataifa, zoooote na mimi nitatumia zangu za ndani ya nchi kuku-bar usishiriki kwangu.

Safi Sana Ni kuwachana live hivi hivi ili kila mtu afanye kile alichochagua.
 
Kiranga

She is still far better than Magufuli..
At least utamtukana utaenda kulala bila wasiwasi....

Hakuna Ben Saanane kupotea
Wala Roma kutekwa wala Maxence Melo kushinda mahakamani...
Nenda tandika uliza unyama waliofanyiwa so called panya road, kwenu mpaka waue public figure ndio mshtuke, tukiuwa wachumia tumbo ni sawa. Huo ni unafiki..
 
Mfumo uliojengwa na Nyerere unawanufaisha vigogo. Hauvunjiki.
Swala la kutokuvunjika kwa mfumo sio kweli, kama ulitengenezwa na watu hao hao watu wanaweza kuuvunja(labda uniambie hawajaamua), endapo wenye dhamana wakiaamua. Hivyo sioni sababu ya kumlaumu Nyerere kwa jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu, sasa kwa kuanzia inabidi kupata katiba mpya. Itakayo mpunguzia madaraka rais na kumuwajibisha tofauti na ilivyo sasa.
 
Hoja ilikuwa nini mpaka kusema hayo!?

Halafu kazi mojawapo ya rais ni kuleta utengamano katika nchi hata kama unapata upinzani kiasi gani kauli za utata kama hizi angeshauriwa aziepuke maana hizo ndiyo zilizomfanya mwendazake kuchukiwa
Ameongea fact,, tatizo wengi hawapendi kusikia ukweli mchungu,, huezi kushirikiana na mtu anaekuhujumu, never
 
Back
Top Bottom