Rais Samia: Nilipoingia ofisini tu Mufti alinijia na furushi la migogoro ya mali za BAKWATA, ila tatizo wamelitengeneza wenyewe

Kama maeneo ya BAKWATA, viongozi wanawauzia waislam wenzao matajiri, wanajenga vituo vya mafuta, viongozi wanagawana pesa, wanakuja viongozi wapya wanadai eneo mgogoro Apo tayari mfano huo
Heee makubwa nikajua haya makorokoro yapo KKKT na RC tu kumbe hata waislamu. Ila walivyo na kiherehere cha kushadadia migogoro ya dini za wenzao utasema kwao hapavuji! Unafiki
 
Mbona hata makanisa Yana migogoro lundo?
 
Hao masheikh wa bakwata akili zao ziko kama za baba yao ccm
 
Mbona hata makanisa Yana migogoro lundo?
Ndugu mimi niliuliza kupata uelewa juu ya kile rais wa nchi kasema. Kwa hiyo unakusudia kusema hata wakristo wamempelekea rundo la migogoro ya mali za wakristo ambazo waliosababisha wako humohumo?

Hapa sio malumbano ya kidini ila tunataka kujielimisha juu ya nani aliuza mali za dini kiholela na kwa nini apelekewe rais badala ya kuwatafuta wahalifu humo ndani?
 

Kwa nini tuendelee kuishi yaliyopita? Kwa nini waislam wasubili miujiza ya kutatuliwa matatizo yao? Matatizo yanajulikana waislam wenye uwezo mpo nini kina kwamisha? Nyerere alikosea sawa. Sasa nini kifanyike kusawazisha? Mohammed majibu yako mengi yako kisiasa sana. Najua una ushawishi wa kutosha kwa waislam wa Tanzania ni wakati wa kutumia huo ushawishi wako kupunguza kero nyingi za waislam. Usipofanya wewe na mwenzio atasubilia mwingi nae aanze. Wakati ni sasa wa waislam kupata kilicho bora.
 
Massa,
Niliandika kitabu cha Abdul Sykes baada ya kuona kuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika inayosomeshwa ina upungufu mkubwa sana.

Hii ndiyo sababu leo tumerudi nyuma tunaisoma upya historia ya TANU.

Sijui kwa nini unafikiri kuwa Waislam wanasubiri miujiza.

Nadhani mambo ya miujiza yapo kanisani.

Katika Uislam husikii watu wakiambiwa kuwa viwete watatupa magongo na kutembea.

Katika miaka ya 1970 Organisation of Islamic Conference (OIC) ilitaka kujenga chuo kikuu Tanzania.

Serikali ikakataa kutoa kibali.

OIC ikajenga chuo hicho Mbale, Uganda.

Katika miaka ya mwishoni 1990s Darul Imaan kutoka Saudi Arabia walitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha ikatokea vurugu kubwa Darul Imaan wakafuta mradi.

Hatujapata kusubiri muujiza.

Sijatoa majibu ya kisiasa siku zote naeleza ukweli ninaoujua.

Serikali peke yake ndiyo iliyo na jukumu la kuondoa dhulma hili si jukumu la watu binafsi.

Serikali ndiyo iliyovunja EAMWS.

Serikali ndiyo iliyozuia EAMWS isijenge shule na chuo kikuu.

Serikali ndiyo iliyowazuia kwa miaka mingi Waislam kuunda taasisi zao.

Serikali iliporuhusu Waislam kuunda taasisi zao huru mengi yamefanyika na tunaendelea kufanya.

Serikali imejiweka mbali na taasisi huru za Waislam inatambua BAKWATA kuwa ndiyo wawakilishi wa Waislam wa Tanzania.

Waislam hawashughulishwi na ukweli huu wanahangaishwa na kujiletea maendeleo yao kwa kujenga shule na kufanya mengine yenye tija.

Kwani huzioni shule za Waislam, vituo vya radio na televisheni unadhani BAKWATA ndiyo wanafanya haya?
 
Kama maeneo ya BAKWATA, viongozi wanawauzia waislam wenzao matajiri, wanajenga vituo vya mafuta, viongozi wanagawana pesa, wanakuja viongozi wapya wanadai eneo mgogoro Apo tayari mfano huo
Mfano eneo la bakwata pale mchicha chang'ombe dar es Salaam, walimuuzia tajiri akajenga bandari kavu. Mpaka sasa kuna mgogoro
 

[emoji122][emoji122] kweli watu mnasoma mm nasoma ila
Bado sana nmejiona mtupu.
 

Ndo miujiza yenyewe hiyo ya kusubilia serikali. Kwa nini msiende kudai haki yenu uko serikalini? Una maana ata viongozi wakuu wa serikali waislam nao wanachangia kuhujumu uislam. Sasa mnasita nini kwenda kuongea nao kama walivyofanya maaskofu wakati wa Ben mkapa? Miujiza sio kuona kiwete anatembea. Hata hiyo ya kusubilia serikali iwape haki yenu ni miujiza pia. Kuandika kitabu tu haitoshi kuna kusoma na kutokukielewa au kusoma na kupuuzia. Usiache ujumbe mzuri uliokwenye kitabu chake upotee tu. Ebu fatilia kuona kama viongozi wanaelewa ulichoandika na utekelezaji wake ukoje. Kumbuka tuko kizazi cha insta na tik tok usiku ata kasimu anafatilia yaliyoko insta kuliko matatizo ya waislam.
 
Uwe unasoma na kuelewa, inaelekea somo la ufahamu hukua mzingatiaji au ndani ya bufuru lako Kuna shida
 
Massa,
Mimi si mtu wa mabishano.

Nimekujibu maswali yako lakini naona unarudi kule kule.

Najua hupendezewi na majibu yangu kwani yanakupa picha nyingine ya Waislam si ile uliyoizoea.
 
Ndio walimpelekea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…