Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Sasa sijui wanamuogopa mama au lah

Enz za jpm walisema mkal waliogopa kumshauri lakn alikuwa mkal pale bidhaa zilipopanda Bei au kuadimika tunakumbuka upungufu wa sukari na hatua alizochukua

Mwez mfungo upo jiran bidhaa zinapanda ndugu zetu waislamu mnaona kinachotaka kutokea

Mama kauli zake hazina afya katika uchumi wetu hasa mwananchi wa kawaida

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma hapo kupanda nauli nikaogopa! Mimi nakwambia vita vya Russia vimetumika kama Funika Kombe mwanaharamu apite! Huenda mambo ni magumu.
 
Huyu bibi bora arudi Zanzibar hajui shs 100 ni kubwa sana kwenye mafuta na tunaoumia ni sisi, yeye anapewa bure kila kitu ndiyo maana anaona siyo kitu, hafai kabisa kuwa kiongozi.
Mkuu usilalamike acheni aupige mwingi na kuifungua nchi.


🤭 Safi sana hiki kinachoendelea.
 
Mama ana kazi ya kuomba mambo yatizamwe tena sio amri, ombi linaweza kubaliwa au lisikubaliwe. Mwanamke lake jiko sio madaraka makubwa.
 
Kwa kauli yake tu ni Kama tayari kawaambia wafanya biashara waongeze gharama za bidhaa, ulimi ni kiungo kidogo sana lakin inaweza kuleta mpasuko mkubwa katika jamii/taifa Kama utakua hauna busara ya kutumia ulimi wako vizuri, pengine ni labda kwakua anauhakika gharama za maisha zikipanda haathiriki yeye ndo maana hajali kuusu sisi wazee wa mlo mmoja kwa siku ambao kula mchana tumeshaona ni Kama anasa
 
Raisi wa ajabu kuwahi kutokea, badala ya kuturhisishia maisha yeye anazidi kuyabana, aige hata huko ulaya anakoenda kutembea bas
 
Dhumuni lakurudisha iyo tozo nikufikia bajeti yao nasiyo kutengeneza unafuu kwa wananchi
Waliyopo kwenye mamlaka wanatizama tuu matumbo na mifuko yao sababu wanazo fedha zakukidhi hayo mahitaji
Eti wananchi waambiwe ukweliii, ni mangapi hawasemi ukwelii
 
Nimemsikia leo kwenye hotuba yake wakati anapokea ripoti ya CAG. kasema serikali haina coordination kwahiyo ka prove mwenyewe kuwa hakuna huo muunganiko ina maana hakukubaliana na waziri wake kuondoa hiyo tozo ya mafuta.wote wanakurupuka tu kutafuta umaarufu.
 
1540+100+ ongezeko la mwezi huu...tutarajie maumivu mwezi April.
 
Ukaguzi wa 2021/ 2022 CAG anatuletea habari za 2020.

Huyu CAG anataka kumfurahisha tu Rais wa sasa hana weledi kabisa.

Ni mtu anayekosa busara kabisa.
 
Wakati wenzetu wanapambana kutatua changamoto za uchumi zilizosababishwa na vita ya Ukraine huku kwetu Mapaka yanatutangazia kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na vita hiyo.Nitaendelea kuimba kuwa Tanzania inaongozwa na vibaka.

 
Akili kubwa Eng. James Mbatia aliongea haya watu wakambeza alisema mafuta yatapanda zaidi na zaidi.
 
nikweli ila hatuna utamaduni huo, nambaya zaidi wanaamini hakuna zaidi yawao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…