Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Rais Samia: Nimeagiza tozo ya mafuta irudishwe, asema nauli na bei za bidhaa vitapanda. Sababu ni vita ya Urusi

Sasa sijui wanamuogopa mama au lah

Enz za jpm walisema mkal waliogopa kumshauri lakn alikuwa mkal pale bidhaa zilipopanda Bei au kuadimika tunakumbuka upungufu wa sukari na hatua alizochukua

Mwez mfungo upo jiran bidhaa zinapanda ndugu zetu waislamu mnaona kinachotaka kutokea

Mama kauli zake hazina afya katika uchumi wetu hasa mwananchi wa kawaida

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma hapo kupanda nauli nikaogopa! Mimi nakwambia vita vya Russia vimetumika kama Funika Kombe mwanaharamu apite! Huenda mambo ni magumu.
 
Huyu bibi bora arudi Zanzibar hajui shs 100 ni kubwa sana kwenye mafuta na tunaoumia ni sisi, yeye anapewa bure kila kitu ndiyo maana anaona siyo kitu, hafai kabisa kuwa kiongozi.
Mkuu usilalamike acheni aupige mwingi na kuifungua nchi.


🤭 Safi sana hiki kinachoendelea.
 
Mama ana kazi ya kuomba mambo yatizamwe tena sio amri, ombi linaweza kubaliwa au lisikubaliwe. Mwanamke lake jiko sio madaraka makubwa.
 
Kwa kauli yake tu ni Kama tayari kawaambia wafanya biashara waongeze gharama za bidhaa, ulimi ni kiungo kidogo sana lakin inaweza kuleta mpasuko mkubwa katika jamii/taifa Kama utakua hauna busara ya kutumia ulimi wako vizuri, pengine ni labda kwakua anauhakika gharama za maisha zikipanda haathiriki yeye ndo maana hajali kuusu sisi wazee wa mlo mmoja kwa siku ambao kula mchana tumeshaona ni Kama anasa
 
Raisi wa ajabu kuwahi kutokea, badala ya kuturhisishia maisha yeye anazidi kuyabana, aige hata huko ulaya anakoenda kutembea bas
 
Dhumuni lakurudisha iyo tozo nikufikia bajeti yao nasiyo kutengeneza unafuu kwa wananchi
Waliyopo kwenye mamlaka wanatizama tuu matumbo na mifuko yao sababu wanazo fedha zakukidhi hayo mahitaji
Eti wananchi waambiwe ukweliii, ni mangapi hawasemi ukwelii
 
Leo Rais Samia amepokea ripoti ya CAG Ikulu Dodoma na kuongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la mafuta. Rais Samia amesema waziri husika aliondoa tozo ya Tsh 100 kwenye lita ya mafuta bila kuangalia upana wake ikiwemo tayari ilikuwemo kwenye bajeti ambayo ilipitishwa na Bunge hivyo Rais ameagiza irejeshwe.

Rais Samia ametaka wananchi kuambiwa ukweli kwamba nauli zitapanda na usafirishaji wa bidhaa umepanda, gharama ambazo zitaingizwa kwenye bei za vitu.

Kuhusu bei ya mafuta ya kula ameomba tathmini ya tozo iliyowekwa kwenye mafuta yanayotoka nje ili kulinda viwanda vya ndani itazamwe tena kwani viwanda hivyo vya ndani havizalishi.

========

Rais Samia: Bei zimepanda kwa bidhaa nyingi tunazoagiza kutoka nje lakini kuna upandaji wa bei za mafuta, mafuta yamekuwa yakipanda nadhani kutoka mwaka jana katikati ya mwaka.

Tukachukua hatua ya kupunguza tozo ndani ya mafuta kwa mara ya kwanza ili kushusha bei ya mafuta kwa wananchi lakini mafuta yameendelea kupanda.

Kipindi hiki cha pili mafuta yamepanda kwa 156 kwa lita, waziri akaona nikitoa shilingi mia yapande kwa shilingi 56 nitaleta unafuu ndani ya nchi lakini kwa bahati mbaya hakuangalia kwa upana zaidi ile ilikuwa tayari iko kwenye bajeti iliyopitishwa na bunge kwahiyo kulikuwa na utata kidogo, tumekaa kama Serikali tumerekebisha.

Ile shilingi iliyotoka, nimeagiza irudishwe na tathmini tuliyofanya hata kama ile shilingi tungeitoa, kwa mwenendo wa upandaji wa mafuta duniani, bado isingekuwa na impact ila tungejikosesha kile ambacho tunakifanya, kwahiyo tumeamua shilingi irudishwe.

Wabunge wenye maeneo yenu, mawaziri mnaosimamia sekta waambieni wananchi ukweli, vita ya Russia na Ukraine imepandisha sana bei ya mafuta na mafuta yanapopanda ndio kila kitu kinapanda.

Nauli zitapanda, usafirishaji wa bidhaa zitapanda. Sasa hivi kutoa kontena China ya bidhaa kuleta Tanzania walikuwa wanalipa kontena ya ft 40 dola 1500, sasa hivi ni dola 8,000-9,000. Hii inaenda kuingia kwenye bidhaa anazozileta kwahiyo waambieni wananchi ukweli, wasikae tu kulaumu Serikali haisemi kitu.

MAFUTA YA KULA
Rais Samia:
Nakumbuka nilikuagiza waziri wa fedha kwamba katika bajeti yetu tunayoimaliza tuliingiza kitu katika mafuta ya kula nadhani na ya nyuma yake ili kulinda viwanda vya ndani nadhani kwenye uzalishaji lakini pamoja na kuongeza hiyo kitu kuzuia mafuta ya nje yasije, viwanda vya ndani ndio vimefungwa kabisa hata huo uzalishaji wenyewe, kwahiyo naomba litizameni tena.

Kama haitusaidii ondoeni ili mafuta ya nje yaingie angalau hata kama bei itakuwa kubwa lakini wananchi wana mafuta ya kutumia. Sasa mmezuia ya nje hayaingii, ndani hayazalishwi, wananchi wanapiga kelele bila shaka mafuta yatapanda bei kwa kiasi kikubwa, nendeni katazameni vipengele vitakavyoleta unafuu kwa wananchi.

=> Kwa mfano kwenye bei ya mafuta Afrika Mashariki na kati Tanzania ndio ina bei ya chini kabisa ya mafuta lakini wenye sekta hawasemi, wamekaa tu wanajifungia.

PIA, Soma=> Rais Samia aagiza tozo za mafuta kupunguzwa
Nimemsikia leo kwenye hotuba yake wakati anapokea ripoti ya CAG. kasema serikali haina coordination kwahiyo ka prove mwenyewe kuwa hakuna huo muunganiko ina maana hakukubaliana na waziri wake kuondoa hiyo tozo ya mafuta.wote wanakurupuka tu kutafuta umaarufu.
 
1540+100+ ongezeko la mwezi huu...tutarajie maumivu mwezi April.
 
Mkuu hii nchi acha tu. Kinachozidi kunisikitisha ni hii hapa chini ivi ni kweli kipindi cha Magu umeme ulikuwa unakatika kwenye Bwawa la Nyerere na kusababishia serikali hasara hiyo. Wacha nicheke tu ila inauma sana.

Hii inadhiirisha wazi kuwa Magufuli alikuwa kiongozi Bora kuwahi kutoka Tanzania na hata Africa. Sasa wanaangalia jinsi ya kumdhoofisha na kuwapandikiza wananchi chuki dhidi ya MagufuliView attachment 2169386
Ukaguzi wa 2021/ 2022 CAG anatuletea habari za 2020.

Huyu CAG anataka kumfurahisha tu Rais wa sasa hana weledi kabisa.

Ni mtu anayekosa busara kabisa.
 
Wakati wenzetu wanapambana kutatua changamoto za uchumi zilizosababishwa na vita ya Ukraine huku kwetu Mapaka yanatutangazia kuwa maisha yatakuwa magumu kutokana na vita hiyo.Nitaendelea kuimba kuwa Tanzania inaongozwa na vibaka.
AARD4K.jpeg

CIXr.jpeg
 
Akili kubwa Eng. James Mbatia aliongea haya watu wakambeza alisema mafuta yatapanda zaidi na zaidi.
 
Ndugu zangu,

Kama ni kweli Januari Makamba alifanya maamuzi kwa utashi wake binafsi kama waziri kukiuka maamuzi ya Bunge na kufuta tozo ya shilingi 100 kwenye mafuta ya petroli na kwa sababu Rais Samia kasema "waziri hakuangalia kwa mapana yake"

Ni afya kwa Waziri Makamba akakaa pembeni la sivyo Bunge limuwajibishe.
nikweli ila hatuna utamaduni huo, nambaya zaidi wanaamini hakuna zaidi yawao.
 
Back
Top Bottom