Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Rais Samia ameitega Yanga ametowa ombi kwa uongozi wa Yanga kuhusu sakata la Fei Toto liishe.

Ikumbukwe Yanga imemuomba Rais maombi ambayo yana thamani zaidi ya Feitoto.

Na tukubali ukweli hivi kuna kiburi gani mwenye jeuri ya kukataa ombi la Rais? tena Rais muungwana kama Samia?

Pia tufahamu nje ya Mtanzania hawa ni Wazanzibar, mama ameomba ombi kistaarabu na kiungwana uongozi wa Yanga umuheshimu mama ikiwezekana kesho aachwe huru aende anapotaka bila kuchukuwa hata mia lakini Karma itamfuata hukohuko aendako.

Cc: Pascal Mayalla
Siasa zinaingizwa kwenye soka,tunapoelekea sio kuzuri,mtu anatakiwa afuate sheria na taratibu za kazi na termination of contract na sio maombi ya Rais,Rais anakuwaje juu ya sheria,Africa tunamambo ya kishamba sana,siku jambazi litaua hadharani na litaachiwa huru kwa ombi la Rais.
 
Ah hamna kumuachia bure labda wampe nafasi ya mwisho ya kuvunja mkataba kwa kufata taratibu .
Serikali haihusiki na hili swala pia lazima sheria ziheshimiwe.
Serikali haiusiki vipi na ndio wamiliki halisi wa Yanga?
 
Kauli ya Raisi kwa third world ni amri. Tutarajie by next week kama sio kesho Fei Toto ni mchezaji huru.

Yanga wanaweza kuikubali ile 120 M kuvunja mkataba, au kumtoa bure kabisa.
 
Ah hamna kumuachia bure labda wampe nafasi ya mwisho ya kuvunja mkataba kwa kufata taratibu .
Serikali haihusiki na hili swala pia lazima sheria ziheshimiwe.
Anatakiwa alipe fidia kwa hasara/ fidia aliyoisababishi club,Tanzania sijui kwa Nini Sheria hazifuatwi,itafika kipindi mtu anafanya kosa akikamatwa anamlilia Rais ,ilo jina la mama linamwendea vibaya
 
Siasa zinaingizwa kwenye soka,tunapoelekea sio kuzuri,mtu anatakiwa afuate sheria na taratibu za kazi na termination of contract na sio maombi ya Rais,Rais anakuwaje juu ya sheria,Africa tunamambo ya kishamba sana,siku jambazi litaua hadharani na litaachiwa huru kwa ombi la Rais.
Rais yupo juu ya sheria hujui unachokiandika.

Magufuli aliwasamehe wabakaji Babu Seya na wanaye waliokuwa wamefungwa kifungo cha maisha.
 
Umeandika ukweli ombi la Rais wa nchi hua ni amri hapo upende usipende lazima watekeleze tena bila kudai hata mia mbovu
Rais hana ubavu wa kuingilia sheria za mpira,ndio maana kwenye nchi nyingine serikali ikiingilia maswala ya mpira huwaga inapigwa bani na FIFA. Labda Yanga waamue kutosimama na sheria za FIFA, FIFA ni domain nyingine ambayo rais wa nchi hana nayo sauti.
 
We umeshiba mihogo unasema linalokujia tu.
Kama serikali inatoa ndege mnakubali na hamsemi inawaingilia,Rais akitoa ushauri ndio kuingiliwa huko?
Inawezekana mpira unaufuatilia ukubwani, serikali hairuhusiwi kuingilia maswala ya kisheria ya mpira wa miguu kwa mujibu wa sheria za FIFA, ipo hivyo ina itabaki kuwa hivyo kwa mujibu wa FIFA hata kama kichwa chako ukikitia ugumu kuelewa.
 
Nchi isiyo na mafanikio yoyote yale yaliyo ya maana, kwenye nyanja yoyote ile, inaona timu kufikia fainali ya kakombe kaliko obscure duniani kuwa ni mafanikio?

Pity the fools.
Aisee...kwa nini wabongo ili msisitize kitu lazima mtumie english jamani🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nchi isiyo na mafanikio yoyote yale yaliyo ya maana, kwenye nyanja yoyote ile, inaona timu kufikia fainali ya kakombe kaliko obscure duniani kuwa ni mafanikio?

Pity the fools.
Bora wewe umeongea pengine unaweza kusikilizwa.

Hata CAF wakisikia kuna harambee imefanyika tena ikiongozwa na Raisi kwa ajili ya kufurahia fainali watatuona watanzania wote ni mambwiga kwa sababu ya upuuzi wa watu wachache

Mourinho kwenye final dhidi ya Roma uliona jinsi alivyotupa medali chini kwa ghadhabu

Huku bongo mambo ni tofauti, Yanga wenye vikamba vya medali wanafuraha zaidi kuliko hata USM ALGER waliobeba kombe.
 
Back
Top Bottom