Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Chakula cha Usiku na Timu ya Yanga kwa ajili ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Juni, 2023.



Rais wa TFF Wallace Karia akitoa salamu za Shirikisho hilo amemshukuru Rais kwa mwaliko wa leo.

View attachment 2647144
Wallace Karia, Rais wa TFF
Ameipongeza timu ya Yanga kwa nafasi waliyofikia kwa kucheza fainali na kushinda mchezo wa mwisho hivyo kuiletea heshima Nchi.

Ushindi wa Yanga umeleta deni kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ambayo itacheza huko Algeria ili kufuzu michuano ya AFCON.

Shirikisho la Mpira litahakikisha mwakani timu zote 4 zinazoshiriki kimataifa zitafanya vizuri zaidi ikiwezekana kuchukua kombe.

Rais wa Yanga Eng. Hersi amemshukuru Rais kwa motisha aliyotoa, ilisababisha wavuke hatua ya mtoano, na kuongoza kwenye hatua ya makundi.

Hamasa ya Rais iliwapa hamasa vijana hao na kwa mara ya kwanza klabu kutoka Tanzania imevaa medali ya CAFCC.

View attachment 2647143
Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga
Eng. Hersi amesema Medali waliyovaa Rais Samia anastahili kuliko mtu mwingine yeyote. Vijana wa Yanga walipigana vita kubwa nchini Algeria, mchezo uligubikwa na kila aina ya vioja. Pamoja na hayo, vijana wa Yanga waliweza kushinda.

Amemuahidi Rais Samia kuendelea kuongeza idadi ya Makombe kwenye utawala wake na kwamba timu ya Yanga itakuwa ya kwanza kuleta kombe la Afrika Tanzania.

Ili kujenga uwanja wake, Hersi amemuomba Rais Samia kuwaongezea sehemu ya ardhi ya mtaa wa jangwani ili uwanja uwe mkubwa.

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema Rais Samia amesaidia sana kuleta hamasa. Jumla ya magoli 26 yamefungwa na Tsh. 190 Milioni imetolewa kama motisha.

View attachment 2647155
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma
Amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege, ni motisha na hamasa iliyotoa maana kuwa Serikali ilikuwa pamoja na timu ya Yanga.

Amewashukuru pia viongozi wa Yanga kwa kuendeleza maono ya waasisi wa klabu hiyo hivyo wanastahili heshima.

Utani wa jadi ni suala lenye manufaa makubwa sana katika kukuza michezo. Simba wanakataa mafanikio ya Yanga sababu ya utani wa jadi lakini moyoni wanayatambua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza timu nzima na upngozi wa Yanga wa kuitoa kimasomaso Tanzania.

Amemtambulisha Rubani Neema kwa kuileta ndege kubwa ya mizigo na kuifikisha salama kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwanzoni mwa mashindano lilikuwa ni suala la timu binafsi lakini baada ya kufika hatua ya juu zaidi, Timu ya Yanga ililiwa inasimama kwa niaba ya Taifa.

Kufika fainali kwa Yanga kumerejesha heshima ya Tanzania, sasa nchi imerudi kwenye ramani ya michezo. Haikuwa rahisi kwa kuwa nchi nyingi zilitoa timu zao, sio jambo jepesi.

Amewaomba Viongozi na wadhamini wa Yanga kuendelea kutoa ari, motisha na hamasa kwa vijana kwa kuongeza maslahi yao.

Amesema mwaka 1993 timu ya simba ilifika pia hatua hii ya juu zaidi, sasa kinachotakiwa ni matayarisho na hamasa.

Timu yoyote itakayokuwa inawakilisha taifa kimataifa itakuwa timu ya kitaifa. Mambo ya utani wa jadi yaishie humu ndani maana mafanikio yanapotokea yatakuja Tanzania. Utaifa uwe mbele kuliko mengine.

View attachment 2647188
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Tanzania inadhamiria kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027 pamoja na Uganda na Kenya hivyo ujenzi wa viwanja na kurekebisha vilivyopo uendelee.

Amewataka wafanyabiashara wa Sekta binafsi kuwekeza zaidi kwenye michezo kwani ni ajira, pia kwa kuwa Serikali imewaachia wafanye biashara kwa uhuru wanapaswa kurudisha kwa jamii.

Rais amesema huwa anafuatilia sana mashindano ya ndondo, mashindano yanayoibua vipaji vya timu ya taifa. Waandaaji wa mashindano hayo atawashika mkono ili waendelee kuibua vipaji hivyo kwa kuwa samaki hukunjwa akiwa bado mbichi.

Amevitaka vilabu kujipanga zaidi mwakani ili kombe hilo lije Afrika.

Pia, ameeleza kuwa hafurahii ugomvi ulipo kati ya Yanga na Feitoto na amewataka viongozi wa klabu hiyo kuumaliza mzozo huo.
Waliokuwa wanasema Yanga ni ya kwanza kufika fainali Mama amewapa jibu safi kuwa Simba ilishafika hapo miaka 30 iliyopita!
 
Habari Wana Yanga Wenzangu, kiufupi na Mimi ni Yanga Die Hard
Sa hivi SAA Mbili Usiku wapo wanapiga Soga na Samia, wakitoka hapo wamechoka, wanaenda kuoga, wanaenda Airport hiyo lazima itakuwa at least SAA Sita usiku. Wanaruka na Ndege. Watafika wamechoka, kesho mechi na Mbeya City, Ijumaa na Prison, Jumatatu na Azam. Hili Fatique la kulazimishana tukutane Tanga Jumatatu.
Hiyo Jumatatu Azam watatupiga kama Ngoma. Nipo nimekaa Pale, tukishinda mniite Umbwa!!
Inabidi wagawe kikosi, wakina zawadi mauya na wenzake wala mkeka wenzake wakamalizie izo mechi mkoani kikosi cha kwanza kibaki dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya fainali na azam.
 
Iliyo niuma ni hiyo milioni mia moja tisini za motisha kwenye sekta ya burudani , lakini walio kwenye sekta ya huduma za jamii hawapewi hata mia zaidi ya kutukanwa na wakina mpwayungu wa jamii forums.

One day tutakutana kwenye kwenye ile bandari ya milele asubuhi ile ya milele kwenye haki iliyo haki kweli.
 
Ndiyo shida ya kupokea vya watu mara kanunua goli mara katoa ndege hatimae anaanza kuwaambia nini cha kufanya.
Wenzako wanasema siasa na michezo ni kitu chausahihi😂😂😂. Hawajui kwanini FIFA walipiga marufuku hivi vitu, ngoja tufunzwe na ulimwengu kwanza😂😂
 
Una utapia mlo wewe endelea kuchezea poka za wazungu... Bata Waheed.
Nchi isiyo na mafanikio yoyote yale yaliyo ya maana, kwenye nyanja yoyote ile, inaona timu kufikia fainali ya kakombe kaliko obscure duniani kuwa ni mafanikio?

Pity the fools.
 
hapa dogo kapata ahueni ila tungemtoa mavvi...KWA HIVI ITABIDI YANGA WAMWACHE BILA MIA YA KUVUNJA MKATABA akazuzrure huko anapopataka
Tuko pamoja, uongozi wa Yanga umuache huru Feitoto bila hata kuchukuwa mia yake halafu warudi kwa Rais kumpa mrejesho ombi lake limetekelezwa, bado ombi la Yanga halafu ndio mtaona mama atafanya nini.

Tujifunze kula na vipofu.
 
Hawajali chochote kuhusu nchi its is all about power, hapo mbinu ni kuwateka washabiki wote wa Yanga ili wampiganie na kumtetea, anajaribu kila awezalo abakie, kama mnakumbuka alipoingia na kuona mambo magumu alikuja na machief akataka kuleta mambo waliotumia Wakoloni akitaka kufufua uchief ili wampiganie kikabila ikabumu sasa kaingia kwenye mpira mwisho wa siku its all about power na haina uhusiano wowote na football wakishindwa kila kitu watahamia kwenye Uislamu ni swala la muda tu, na huo ndio utakuwa mwisho wa Tanzania, wanaingiza hii nchi shimoni kwa uroho wa madaraka, …
Hizo ndiyo strategies za siasa sasa siyo zile ambazo Magufuli alikuwa ananunua wabunge wa upinzania kisha kurudia uchaguzi. Au kuua wapinzania
 
Tuko pamoja, uongozi wa Yanga umuache huru Feitoto bila hata kuchukuwa mia yake halafu warudi kwa Rais kumpa mrejesho ombi lake limetekelezwa, bado ombi la Yanga halafu ndio mtaona mama atafanya nini.

Tujifunze kula na vipofu.

Umeona mbali sana mkuu
 
Back
Top Bottom