Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

KKwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Chakula cha Usiku na Timu ya Yanga kwa ajili ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Juni, 2023.



Rais wa TFF Wallace Karia akitoa salamu za Shirikisho hilo amemshukuru Rais kwa mwaliko wa leo.

View attachment 2647144
Wallace Karia, Rais wa TFF
Ameipongeza timu ya Yanga kwa nafasi waliyofikia kwa kucheza fainali na kushinda mchezo wa mwisho hivyo kuiletea heshima Nchi.

Ushindi wa Yanga umeleta deni kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ambayo itacheza huko Algeria ili kufuzu michuano ya AFCON.

Shirikisho la Mpira litahakikisha mwakani timu zote 4 zinazoshiriki kimataifa zitafanya vizuri zaidi ikiwezekana kuchukua kombe.

Rais wa Yanga Eng. Hersi amemshukuru Rais kwa motisha aliyotoa, ilisababisha wavuke hatua ya mtoano, na kuongoza kwenye hatua ya makundi.

Hamasa ya Rais iliwapa hamasa vijana hao na kwa mara ya kwanza klabu kutoka Tanzania imevaa medali ya CAFCC.

View attachment 2647143
Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga
Eng. Hersi amesema Medali waliyovaa Rais Samia anastahili kuliko mtu mwingine yeyote. Vijana wa Yanga walipigana vita kubwa nchini Algeria, mchezo uligubikwa na kila aina ya vioja. Pamoja na hayo, vijana wa Yanga waliweza kushinda.

Amemuahidi Rais Samia kuendelea kuongeza idadi ya Makombe kwenye utawala wake na kwamba timu ya Yanga itakuwa ya kwanza kuleta kombe la Afrika Tanzania.

Ili kujenga uwanja wake, Hersi amemuomba Rais Samia kuwaongezea sehemu ya ardhi ya mtaa wa jangwani ili uwanja uwe mkubwa.

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema Rais Samia amesaidia sana kuleta hamasa. Jumla ya magoli 26 yamefungwa na Tsh. 190 Milioni imetolewa kama motisha.

View attachment 2647155
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma
Amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege, ni motisha na hamasa iliyotoa maana kuwa Serikali ilikuwa pamoja na timu ya Yanga.

Amewashukuru pia viongozi wa Yanga kwa kuendeleza maono ya waasisi wa klabu hiyo hivyo wanastahili heshima.

Utani wa jadi ni suala lenye manufaa makubwa sana katika kukuza michezo. Simba wanakataa mafanikio ya Yanga sababu ya utani wa jadi lakini moyoni wanayatambua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza timu nzima na upngozi wa Yanga wa kuitoa kimasomaso Tanzania.

Amemtambulisha Rubani Neema kwa kuileta ndege kubwa ya mizigo na kuifikisha salama kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwanzoni mwa mashindano lilikuwa ni suala la timu binafsi lakini baada ya kufika hatua ya juu zaidi, Timu ya Yanga ililiwa inasimama kwa niaba ya Taifa.

Kufika fainali kwa Yanga kumerejesha heshima ya Tanzania, sasa nchi imerudi kwenye ramani ya michezo. Haikuwa rahisi kwa kuwa nchi nyingi zilitoa timu zao, sio jambo jepesi.

Amewaomba Viongozi na wadhamini wa Yanga kuendelea kutoa ari, motisha na hamasa kwa vijana kwa kuongeza maslahi yao.

Amesema mwaka 1993 timu ya simba ilifika pia hatua hii ya juu zaidi, sasa kinachotakiwa ni matayarisho na hamasa.

Timu yoyote itakayokuwa inawakilisha taifa kimataifa itakuwa timu ya kitaifa. Mambo ya utani wa jadi yaishie humu ndani maana mafanikio yanapotokea yatakuja Tanzania. Utaifa uwe mbele kuliko mengine.

View attachment 2647188
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Tanzania inadhamiria kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027 pamoja na Uganda na Kenya hivyo ujenzi wa viwanja na kurekebisha vilivyopo uendelee.

Amewataka wafanyabiashara wa Sekta binafsi kuwekeza zaidi kwenye michezo kwani ni ajira, pia kwa kuwa Serikali imewaachia wafanye biashara kwa uhuru wanapaswa kurudisha kwa jamii.

Rais amesema huwa anafuatilia sana mashindano ya ndondo, mashindano yanayoibua vipaji vya timu ya taifa. Waandaaji wa mashindano hayo atawashika mkono ili waendelee kuibua vipaji hivyo kwa kuwa samaki hukunjwa akiwa bado mbichi.

Amevitaka vilabu kujipanga zaidi mwakani ili kombe hilo lije Afrika.

Pia, ameeleza kuwa hafurahii ugomvi ulipo kati ya Yanga na Feitoto na amewataka viongozi wa klabu hiyo kuumaliza mzozo huo.

Huyu ana Uzanzibari sana, anataka fei ahurumiwe kwakuwa ni Mzanzibari. Tusirudie kuwapa hawa wabaguzi uongozi wa nchi,

Hili.likikubalika fifa lazima itufungie kwa kuingiza siasa kwenye mpira
 
Aya Sasa simnasema Mnafata sheria Mara mna utaratibu haya Sasa tuone. Mkikataa maombi ya Rais walahi nyie ni mbinguni moja Kwa moja manina. [emoji23][emoji23][emoji23]

Ukijipendekeza na kuingia kwenye korido za wanasiasa lazima yatakugharimu tuu. Tuone Sasa kama hamtafa matakwa ya huyu mama [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], shida mnakuwa machawa mpaka mnakera na bado [emoji38][emoji38]
Screenshot_20230605-202140.jpg
 
Hili umelisemea sana lakini watu hawakutaka kuelewa sababu ya ushabiki.Sasa tuone kama Yanga bado watataka kumwambia Fei team inayomtaka ije mezani baada ya maelekezo ya leo .Hapa linakwisha kwa 112M walizozikataa na dogo anasepa zake kiulaini.
Hatma ya fei Toto ,iko kwa mtu mmoja tu,wala sio Rais,uyo akiweka ngumu ,dogo ataendelea kufurukuta
 
Kumg'ang'ania Fei ni ujinga sababu:

Akishinda kesi mnamlipa, Akishindwa kesi either atawalipa kidogo na kama hana uwezo wa kuwalipa labda kufungiwa soka.

Sasa kwanini asipigwe faini akaachwa? Kwa Club hakuna manufaa yoyote kumshikilia ila kama ni kiongozi anataka kuonyesha umwamba wake kwa Fei sawa, auonyeshe tuuone.
Mwingine akilianzisha kama Fei .. mama akiomba tena ? lazima kuwe na nidhamu, yakiendekezwa haya mambo kuna hatari kwenye vilabu vyetu
 
Rais Samia ameitega Yanga ametowa ombi kwa uongozi wa Yanga kuhusu sakata la Fei Toto liishe.

Ikumbukwe Yanga imemuomba Rais maombi ambayo yana thamani zaidi ya Feitoto.

Na tukubali ukweli hivi kuna kiburi gani mwenye jeuri ya kukataa ombi la Rais? tena Rais muungwana kama Samia?

Pia tufahamu nje ya Mtanzania hawa ni Wazanzibar, mama ameomba ombi kistaarabu na kiungwana uongozi wa Yanga umuheshimu mama ikiwezekana kesho aachwe huru aende anapotaka bila kuchukuwa hata mia lakini Karma itamfuata hukohuko aendako.

Cc: Pascal Mayalla
hapa dogo kapata ahueni ila tungemtoa mavvi...KWA HIVI ITABIDI YANGA WAMWACHE BILA MIA YA KUVUNJA MKATABA akazuzrure huko anapopataka
 
Kwaiyo kwenye kuunganisha na siasa inaingizwa [emoji23][emoji23][emoji23], wasomi wa ajabu nchi hii. Umeshawahi kusikia vilabu vikiambatanishwa na siasa, mfano rahisi angalia nchi ambazo mpira umeendelea yaani uingereza na hispania. King Charles na alikuwa anapishwa lakini hukusikia ligi za mpira au vilabu vya mpira vikitaja hata kidogo hilo jambo bali ilihairishwa ratiba ili kupisha zoezi ila siasa haikutumika hata kidogo kwenye mpira siku hiyo ila uku 3rd world country tunajua kuchanganya mpira na siasa, aisee[emoji23][emoji23][emoji23]. Mtafungiwa na FIFA, aisee.
Si uende huko Uingereza ukaishi ambako King Charles hawezi kutaja timu anayoshabikia!! Sisi tuache hivyo hivyo, timu hizi 2 huwezi kuzitenganisha na historia ya Tanzania
 
Back
Top Bottom