Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Rais Samia: Sifurahii Mgogoro wa Yanga na Feitoto. Nataka umalizike

Inawezekana mpira unaufuatilia ukubwani, serikali hairuhusiwi kuingilia maswala ya kisheria ya mpira wa miguu kwa mujibu wa sheria za FIFA, ipo hivyo ina itabaki kuwa hivyo kwa mujibu wa FIFA hata kama kichwa chako ukikitia ugumu kuelewa.
Hivi unajuwa kama Sepp Blater alikamatwa na serikali kwa mambo ya mpira?

Wewe jizime data tu waulize kina Michael Wambura amenyooka sasa.
 
Pamojq na kwamba mliiwakilisha nchi kwa kiasi chake na mkapewa zawadi kede kede mpka ndege mkapewa lakini bado club ya Yanga mna fedheha kubwa inawagubika na kuwaumbua . Dhana yangu ni nini Wakati Dr Samia Sulhu Hasanai yuko katika kuponya majeraha na kuondoa migogoro na makovu yaloachwa na mwenda zake kwenye taasisi mashirika na nchi mbalimbali nyinyi hamuyaoni matunda ya Raisi zaidi sana nyinyi ndio mnaku viongozi wapinzani dhidi ya Raisi .

Leo Yanga sports club mmeabisha kama mmeelewa Dr samia suluhu alilolizungumza haiwezekani suala la Katoto kamoja ata kasiko na madhara kwa timu mnalicha mpk raisi analiingilia na kutoa tamko .Uongozi wa yanga hii ni aibu kubwa kwenu maaana kwa sasa hata mkienda kulitolea maamuzi suala la Feisal salumu kwenye club mtaonekana mmefanya sababu ya shinikizo la raisi kuwaambia mlimalizi mlishindwa kumaliza suala hili kabla hata ya raisi kuliingilia?

Maamuzi mtakaoyafanya kwa sasa ni kuonesha dhahiri kua mlishindwa kujismamia mpaka kiongozi wa nchi awaambia hapa mnafanya makosa hili liwaandee Taasisi ,mashirika na watu binafsi wote tekelezeni wajibu wenu sio kila kitu mpka mkuu wa nchi atoe maamuzi kwenye mambo madogomadogo nia aibu inapotokea suala kama la leo kwa yanga Africa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Chakula cha Usiku na Timu ya Yanga kwa ajili ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Juni, 2023.



Rais wa TFF Wallace Karia akitoa salamu za Shirikisho hilo amemshukuru Rais kwa mwaliko wa leo.

View attachment 2647144
Wallace Karia, Rais wa TFF
Ameipongeza timu ya Yanga kwa nafasi waliyofikia kwa kucheza fainali na kushinda mchezo wa mwisho hivyo kuiletea heshima Nchi.

Ushindi wa Yanga umeleta deni kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ambayo itacheza huko Algeria ili kufuzu michuano ya AFCON.

Shirikisho la Mpira litahakikisha mwakani timu zote 4 zinazoshiriki kimataifa zitafanya vizuri zaidi ikiwezekana kuchukua kombe.

Rais wa Yanga Eng. Hersi amemshukuru Rais kwa motisha aliyotoa, ilisababisha wavuke hatua ya mtoano, na kuongoza kwenye hatua ya makundi.

Hamasa ya Rais iliwapa hamasa vijana hao na kwa mara ya kwanza klabu kutoka Tanzania imevaa medali ya CAFCC.

View attachment 2647143
Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga
Eng. Hersi amesema Medali waliyovaa Rais Samia anastahili kuliko mtu mwingine yeyote. Vijana wa Yanga walipigana vita kubwa nchini Algeria, mchezo uligubikwa na kila aina ya vioja. Pamoja na hayo, vijana wa Yanga waliweza kushinda.

Amemuahidi Rais Samia kuendelea kuongeza idadi ya Makombe kwenye utawala wake na kwamba timu ya Yanga itakuwa ya kwanza kuleta kombe la Afrika Tanzania.

Ili kujenga uwanja wake, Hersi amemuomba Rais Samia kuwaongezea sehemu ya ardhi ya mtaa wa jangwani ili uwanja uwe mkubwa.

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema Rais Samia amesaidia sana kuleta hamasa. Jumla ya magoli 26 yamefungwa na Tsh. 190 Milioni imetolewa kama motisha.

View attachment 2647155
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma
Amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege, ni motisha na hamasa iliyotoa maana kuwa Serikali ilikuwa pamoja na timu ya Yanga.

Amewashukuru pia viongozi wa Yanga kwa kuendeleza maono ya waasisi wa klabu hiyo hivyo wanastahili heshima.

Utani wa jadi ni suala lenye manufaa makubwa sana katika kukuza michezo. Simba wanakataa mafanikio ya Yanga sababu ya utani wa jadi lakini moyoni wanayatambua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza timu nzima na upngozi wa Yanga wa kuitoa kimasomaso Tanzania.

Amemtambulisha Rubani Neema kwa kuileta ndege kubwa ya mizigo na kuifikisha salama kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwanzoni mwa mashindano lilikuwa ni suala la timu binafsi lakini baada ya kufika hatua ya juu zaidi, Timu ya Yanga ililiwa inasimama kwa niaba ya Taifa.

Kufika fainali kwa Yanga kumerejesha heshima ya Tanzania, sasa nchi imerudi kwenye ramani ya michezo. Haikuwa rahisi kwa kuwa nchi nyingi zilitoa timu zao, sio jambo jepesi.

Amewaomba Viongozi na wadhamini wa Yanga kuendelea kutoa ari, motisha na hamasa kwa vijana kwa kuongeza maslahi yao.

Amesema mwaka 1993 timu ya simba ilifika pia hatua hii ya juu zaidi, sasa kinachotakiwa ni matayarisho na hamasa.

Timu yoyote itakayokuwa inawakilisha taifa kimataifa itakuwa timu ya kitaifa. Mambo ya utani wa jadi yaishie humu ndani maana mafanikio yanapotokea yatakuja Tanzania. Utaifa uwe mbele kuliko mengine.

View attachment 2647188
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Tanzania inadhamiria kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027 pamoja na Uganda na Kenya hivyo ujenzi wa viwanja na kurekebisha vilivyopo uendelee.

Amewataka wafanyabiashara wa Sekta binafsi kuwekeza zaidi kwenye michezo kwani ni ajira, pia kwa kuwa Serikali imewaachia wafanye biashara kwa uhuru wanapaswa kurudisha kwa jamii.

Rais amesema huwa anafuatilia sana mashindano ya ndondo, mashindano yanayoibua vipaji vya timu ya taifa. Waandaaji wa mashindano hayo atawashika mkono ili waendelee kuibua vipaji hivyo kwa kuwa samaki hukunjwa akiwa bado mbichi.

Amevitaka vilabu kujipanga zaidi mwakani ili kombe hilo lije Afrika.

Pia, ameeleza kuwa hafurahii ugomvi ulipo kati ya Yanga na Feitoto na amewataka viongozi wa klabu hiyo kuumaliza mzozo huo.
Waliokuwa wanasema Yanga ni ya kwanza kufika fainali Mama anewapa jibu safi kuwa Simba ilishafika hapo miaka 30 iliyopita!
 
Habari Wana Yanga Wenzangu, kiufupi na Mimi ni Yanga Die Hard
Sa hivi SAA Mbili Usiku wapo wanapiga Soga na Samia, wakitoka hapo wamechoka, wanaenda kuoga, wanaenda Airport hiyo lazima itakuwa at least SAA Sita usiku. Wanaruka na Ndege. Watafika wamechoka, kesho mechi na Mbeya City, Ijumaa na Prison, Jumatatu na Azam. Hili Fatique la kulazimishana tukutane Tanga Jumatatu.
Hiyo Jumatatu Azam watatupiga kama Ngoma. Nipo nimekaa Pale, tukishinda mniite Umbwa!!
Iko hivi,Leo watalahi,wataondoka kesho asubuhi,na ndege,mkuu wa nchi kawapa ndege ya kuwapeleka mbeya,isiwe na shaka na Hilo mkuu
 
Hata huo Uislamu wenyewe wewe unatumiwa tu lkn wenzako wala siyo Waislamu kihivyo ni jina tu kuwadanganya ingekuwa ni Waislamu kweli wasingeruhusu Ushoga, …
BBC News, Swahili
Ruka hadi maelezo
Yaliyomo
HabariMichezoMakalaAfyaBurudaniVideoVipindi vya Redio
Papa 'aashiria kuunga mkono' ndoa za watu wa jinsia moja
22 Oktoba 2020

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Maelezo ya picha,
Kauli ya Papa Francis inatofautiana msimamo wake wa awali kuhusu haki ya wapenzi wa jinsia moja

Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kwamba anafikiria wapenzi wa jinsia wanastahili kuruhusiwa "kuoana".

Wachambuzi wanasema kauli yake hiyo imeashiria wazi msimamo wake kuhusu uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsia moja, katika makala yaliyoelekezwa na Evgeny Afineevsky.

"Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wana haki ya kuwa na familia,"alisema katika filamu, ambayo ilioneshwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

"Ni watoto wa Mungu nawana haki ya kuwa na familia. Hakuna mtu anayestahili kutengwa ama kufanywa ajihisi mnyonge kwa kuamua kuwa katika uhusiano wa aina hiyo.

"Tunachopaswa kuunda ni sheria ya umoja wa kiraia. ili kuwalinda kisheria."

Ameongeza kwamba "aliunga mkono wazo hilo", akiashiria nyakati alipokuwa Askofu mkuu wa Buenos Aires, akisema japo alipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja katika sheria, aliunga mkono ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja.

Filamu ya Francesco, inayoangazi amaisha na kazi ya Papa Francis, ilioneshwa kama sehemu ya Tamasha la Filamu la Roma.

Unaweza pia kusoma:
Papa 'ahofia' makasisi wapenzi wa jinsia moja
Vatican yapinga dhana ya mapenzi ya jinsia moja
Japo kauli ya Papa kuhusu ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja iliangaziwa, filamu hiyo pia inamuonyesha akiwahimiza wanaume wawili mashoga kuhudhuria kanisa na watoto wao watatu.

Muandishi wa Biografia ya Papa Francis, Austen Ivereigh, ameiambia BBC kwamba "hakushangazwa" na kauli hiyo ya hivi punde.

"Huo ulikuwa msimamo wake alipokuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires," alisema Bw. Ivereigh. "Siku zote alikuwa akipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja. Lakini aliamini kanisa linapaswa kutetea sheria ya kuwalinda wapenzi wa jinsia."

Chini ya mafundisho ya sasa ya Katoliki, uhusiano wa wapenzi wajinsia moja unaangaziwa kama "tabia potofu"

Mwaka 2003, shirika la mafundisho la Vatican, Usharika wa Mafundisho ya Imani, lilisema kwamba "heshima kwa watu wa jinsia moja haiwezi kwa njia yoyote kuidhinisha ya uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja au kutambuliwa kisheria kwa vyama vya wapenzi wa njinsia moja".


Msimamo uliopita wa Papa kuhusu mapenzi ya jinsia moja ulikuwa upi?

Tamko la Papa la hivi karibuni ni msururu wa maoni ambayo ametoa kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja - akiangazia msaada wanaostahili kupewa, lakini hajaidhinsha moja kwa moja mahusiano ya kimapenzi ya aina hiyo.

Mwaka 2013, katika kitabu cha Heaven and Earth, Papa alisema kuwa kusawazisha kisheria mahusiano ya jinsia moja na ndoa za jinsia moja itakuwa "upungufu wa kianthropolojia".

Pia alisema ikiwa wanandoa wa jinsia moja wataruhusiwa kuasili, "watoto huenda wakaathitika ... kwami kila mtu anahitaji kuwa na baba wa kiume na mama wa kike ambao wanaweza kuwasaidia utambulisho wao''.


Maelezo ya video,
"If a person is gay and seeks God and has good will, who am I to judge?"

Mwaka huo huo,alisisitiza msimamo wa Kanisa kwamba vitendo vya ushoga ni dhambi, lakini akasema mwelekeo wa ushoga sio.

"Ikiwa mtu anashiriki mapenzi ya jinsia moja na anamtafuta Mungu kwa nia njema, mimi ni nani nimhukumu?,"aliuliza.

Mwaka 2014 iliripotiwa kuwa Papa Francis aliashiria kuunga mkono ndoa ya wapenzi wa wa jinsia moja katika mahojiano, lakini ofisi yake ya mawasiliano ilikanusha taarifa hizo.

Na mwaka 2018, Papa Francis alisema "ana hofu" kuhusu mapenzi ya jinsia moja miongoni mwa makasisi akiongeza kwamba ni "jambo zito".

Habari kuu
Moja kwa moja“Mackenzie hatatoka gerezani tena, atazeeka huko” - Waziri
Ubelgiji yachunguza kama silaha zake zimetumika kushambulia ardhi ya Urusi
Saa 3 zilizopita
Kati ya washambuliaji hawa watano mmoja kuziba pengo la Benzema Madrid
Saa 4 zilizopita
Gumzo mitandaoni

Kwa nini tunashikwa na homa? na ni wakati gani inapaswa kuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa?
3 Juni 2023

Hakuna suluhu ya Sudan inayoweza kudumu hadi wapiganaji waondoke mji mkuu - jeshi
Saa 8 zilizopita

UFO: Mambo matano yaliyofichliwa katika kikao cha jopo la NASA
2 Juni 2023

Kifahamu Chuo Kikuu cha kwanza na kikongwe zaidi duniani kilichotokana na msikiti
2 Juni 2023

Kwa nini shambulio kubwa na la nguvu lililotangazwa na jeshi la Ukraine dhidi ya Urusi halijaanza mpaka sasa?
2 Juni 2023

Vita vya Ukraine: Zifahamu rasilimali 5 zilizopokwa na Urusi huko Ukraine mpaka sasa
1 Juni 2023

Pande mbili za mji mkuu wa Somalia Mogadishu
31 Mei 2023

Fahamu fukwe bora za bahari duniani mwaka 2023
31 Mei 2023

Miradi ya utajiri wa haraka: Hizi ni ishara tano kwamba unatapeliwa
30 Mei 2023
Iliyosomwa zaidi
BBC News, Swahili
Kwanini unaweza kuiamini BBC News
Sheria ya matumizi
Kuhusu BBC
Sera ya faragha
Cookies
Wasiliana na BBC
Do not share or sell my info
© 2023 BBC. BBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje. Soma kuhusu mtazamo wetu wa viambatanishi vya nje
 
Pamojq na kwamba mliiwakilisha nchi kwa kiasi chake na mkapewa zawadi kede kede mpka ndege mkapewa lakini bado club ya Yanga mna fedheha kubwa inawagubika na kuwaumbua . Dhana yangu ni nini Wakati Dr Samia Sulhu Hasanai yuko katika kuponya majeraha na kuondoa migogoro na makovu yaloachwa na mwenda zake kwenye taasisi mashirika na nchi mbalimbali nyinyi hamuyaoni matunda ya Raisi zaidi sana nyinyi ndio mnaku viongozi wapinzani dhidi ya Raisi . Leo Yanga sports club mmeabisha kama mmeelewa Dr samia suluhu alilolizungumza haiwezekani suala la Katoto kamoja ata kasiko na madhara kwa timu mnalicha mpk raisi analiingilia na kutoa tamko .Uongozi wa yanga hii ni aibu kubwa kwenu maaana kwa sasa hata mkienda kulitolea maamuzi suala la Feisal salumu kwenye club mtaonekana mmefanya sababu ya shinikizo la raisi kuwaambia mlimalizi mlishindwa kumaliza suala hili kabla hata ya raisi kuliingilia? Maamuzi mtakaoyafanya kwa sasa ni kuonesha dhahiri kua mlishindwa kujismamia mpaka kiongozi wa nchi awaambia hapa mnafanya makosa hili liwaandee Taasisi ,mashirika na watu binafsi wote tekelezeni wajibu wenu sio kila kitu mpka mkuu wa nchi atoe maamuzi kwenye mambo madogomadogo nia aibu inapotokea suala kama la leo kwa yanga Africa
Kiukweli mwanangu una mwandiko mbaya.

Jaribu kuweka aya ili ueleleweke vizuri.

Samahani mkuu kama nitakua nimekukwaza.
 
Nchi isiyo na mafanikio yoyote yale yaliyo ya maana, kwenye nyanja yoyote ile, inaona timu kufikia fainali ya kakombe kaliko obscure duniani kuwa ni mafanikio?

Pity the fools.

Na wewe unachukua mda kujadili fools, very stupid
 
Waliokuwa wanasema Yanga ni ya kwanza kufika fainali Mama anewapa jibu safi kuwa Simba ilishafika hapo miaka 30 iliyopita!
Hivi unadhani huyu mama ni boya kama makolo?

Viongozi wa Simba wako pale amewapoza tu kwa kusema simba iliwahi kufika level ya Fainali na siyo Fainali ya Confederation cup.
 
Hivi unajuwa kama Sepp Blater alikamatwa na serikali kwa mambo ya mpira?

Wewe jizime data tu waulize kina Michael Wambura amenyooka sasa.
Serikali gani iliyomtia hatiani? FIFA inajiendesha yenyewe mambo yake , hata US na EU ilitia ngumu World Cup isifanyike Russia na bado ikafanyika. Sasa Super kama US pamoja na washirika wake EU,ila kwa FIFA waligonga mwamba. FIFA kwenye mpira maamuzi yake huwaga ya mwisho, labda turudi kwenye zile tabia zetu za kuoneana huruma tuongee ila kisheria Rais hana mamlaka kwenye mpira wa miguu.
 
Wakimaliza kula pilau hapo, wamepewa ndege iwapeleke mbeya leo kesho wanacheza kukamilisha mzunguko wa ligi halafu wanakabidhiwa kombe lao, baadae wataalikwa chamwino ikulu dodoma ili wakamuoneshe kombe la ubingwa yaani leo walienda kuonesha medali halafu chamwino ni kombe sasa
🤣🤣🤣🤣🤣🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻
 
Kiukweli mwanangu una mwandiko mbaya.

Jaribu kuweka aya ili ueleleweke vizuri.

Samahani mkuu kama nitakua nimekukwaza.
Umemkwaza vipi na ndio ukweli wenyewe.

Halafu hapo mwenyewe anaona ameshusha nondo kumbe ni ushuzi wa bata tu.
 
Back
Top Bottom