Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

Rais Samia Suluhu anakwenda kuzoa kura zote uchaguzi ujao

Naomba uwe mwelewa. Ajira zinatengenezwa sio nafasi za kazi serikalini. Magufuli alitengeneza ajira kiasi kwa kujenga miundo mbinu nchi nzima. Mama Angekuja na akili mpya ya namna ya kutengeneza ajira.
Basi wewe sio mfatiliaji mzuri Rais Samia ametoa ajira nyingi sana za serikali ukiachana na izo pia ameleta fursa kwa vijana mikopo inatolewa kwa mashart nafuu pia anawekeza katika kilimo lakini vijana wengi wa sasa ni wavivu kila kitu kupinga tu
 
Kuna ajira katika secta ya umma na secta binafsi, ifahamike kuwa serikali peke yake haiwezi kuajiri vijana wote wanao maliza vyuo vikuu na vyuo vya kati,

Sasa Basi kwa kulitambua Hilo ndio maana unaona serikali ya mh Rais wetu ikihakikisha secta binafsi inakuwa imara, hii inafanyika kwa kuweka Sera nzuri na Sheria rafiki ili kuvutia wawekezaji katika nyanja mbalimbali, maana wakina wawekezaji wakawekeza mf katika viwanda wataajiri vijana wa kitanzania, ambapo hapa faida take Ni kuwa licha ya kijana kupata mshahara na kulipa Kodi serikalini itamsaidia pia kijana kupata ujuzi na uzoefu,

Sanjari na Hilo pia miradi mingi tu imekuwa ikijengwa na serikali ambapo imekuwa pia ikitoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja,

Mh Rais wetu pia amekuwa akiimarisha mahusiano yetu ya kimataifa Jambo ambalo linasaidia kuwavuta wawekezaji hapa nchini kwetu kuweza kuwekeza, kwa ufupi. Mama Anastahili pongezi kutoka kwetu watanzania
 
Naomba uwe mwelewa. Ajira zinatengenezwa sio nafasi za kazi serikalini. Magufuli alitengeneza ajira kiasi kwa kujenga miundo mbinu nchi nzima. Mama Angekuja na akili mpya ya namna ya kutengeneza ajira.
Wewe ni taahira kiukweli,nikikwambia Lete Takwimu za ajira zilizotengenezwa na Magufuli kama unavyodai huna..

Labda kama mlitengeneza hizo ajira kwenye vile viwanda vyenu vya vyerehani..

Mwisho,kwani miundombinu imeacha kujengwa? In fact saizi ajira za kwenye miundombinu zinazotengenezwa ni nyingi kuliko hapo awali..

Unavyozungumzia bajeti ya barabara za Tarura kutoka bil.257 hadi bil 752 ni ajira zaidi na zaidi..

Unavyozungumzia bajeti ya Wizara ya maji kutoka bil.302 hadi bil.767 ni miradi mingi zaidi na ajira zaidi..

Unavyozungumzia bil.954 kutoka bil.205 za irrigation unazungumzia ajira zaidi na zaidi.

Unavyozungumzia ujenzi wa mashule,vituo vya afya nk ni ajira zaidi na zaidi..
 
Punguza dhihaka. Mama mwenyewe anawaogopa upinzani ndio maana amekataa wasifanye mikutano ya siasa. Wafuasi wa upinzani Tanzania ni wengi kuliko ccm. Sema system hairuhusu kufurahia Uhuru wa vyama vya upinzani ndio maana wengi wanajificha.
Mama Samia suluhu Hassani hawaogopi wapinzani Bali anawaheshimu Kama ilivyo hulka yake ya kuheshimu kila mtu, Anawaheshimu hata wapinzani kwa kuwa anajuwa kuwa Taifa Hili litajengwa na sisi sote watanzania, lakini pia anaona haipendezi tukajenga Taifa ambalo limegawanyika mapande mapande,

Anataka kuona kuwa kila mtu anajivunia kuwa mtanzania, anataka kuona Kama kikijengwa kituo Cha Afya Basi kila mtu afurahi na kuona kuwa Ni chetu sote, anataka kuona mradi wa maji ukipelekwa mahali fulani unapokelewa na watu wote na kulindwa na watu wote

Anajuwa kuwa ili Hili lifanikiwe hatuna budi kujenga umoja wa kitaifa, anaona kuwa Ni lazima tuheshimiane na kupendana, anaona kuwa Ni lazima Basi ikitokea tunakosoana Basi Tukosoane kwa staha bila kuvunjiana utu wetu, anaona kuwa tunaweza tukaijenga Tanzania Yetu iliyo Bora pamoja na kuwa tunatofautiana katika baadhi ya misimamo yetu ya kisiasa

Ndio maana unaona akitoa fursa ya kuweza kukutana na kufanya mazungumzo na hata viongozi wa vyama vya upinzani ili kuzungumza nao na kukubaliana katika yanayowezekana na kutafuta muafaka katika yanayohitaji mjadala mpana
 
Basi wewe sio mfatiliaji mzuri Rais Samia ametoa ajira nyingi sana za serikali ukiachana na izo pia ameleta fursa kwa vijana mikopo inatolewa kwa mashart nafuu pia anawekeza katika kilimo lakini vijana wengi wa sasa ni wavivu kila kitu kupinga tu
Hao Wana chuki binafsi,hata usihangaike Sana kujichosha,hata dakika hii tunaongea,mwambie aingie ajira portal ya serikali kuna ajira lundo huko za Tawa na taasisi zingine kibao..

Hivyo hivyo ukienda private sector saizi ajira zinamwagika..

Just imagine kwa Takwimu hizi hapa chini just kwa mda mfupi tuu 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220817-174037.png
    Screenshot_20220817-174037.png
    89.4 KB · Views: 2
Nchi ngum Sana hii,nimejikuta nikicheka kijinga Sana, Sasa SSH ndo anajenga au Serikali ndo inajenga? yeye ni msimamizi katika ngazi ya juu ya serikali KWa niaba ya wenye nchi, Sasa mkisema anajenga hizo pesa anatoa mfukoni mwake?,
Alafu ni serikali ipi ambayo haikujenga shule,hospitali, reli, mabwawa ya umeme, stendi,n.k, nchi haijawahi simama ,vilevile hata yeye akiondoka 2025, serikali ijayo bado itaendelea kujenga tu,
Sasa sijui huwa mnasifia KWa kujua au kutojua ,acheni Mambo haya, kwani serikali yake kurudisha maendeleo KWa wananchi ambao ndo walipa kodi ni hisani au niwajibu ? Kama ndivyo sifa za ajabu za nini, badilikeni
Jamaa amelogwaa ila hajastuka, akistuka itakua too late.
 
SAMIA ana kazi sana,kwanza wapiga kura wengi ni wanawakewa ambapo hawapendi kuongozwa na Mwanamke mwenzao-Wanaume vilevile hawapendi kabisa ukijumuisha na Uzanzibar wake labda aibe tu kura lakini free and fair hawezi kutoboa hata robo.

..vilevile ni mwanasiasa asiyeweza kujieleza, na asiyevutia kumsikiliza.

..labda abebwe na mapesa ya Ccm, vyombo vya habari, na vyombo vya dola.

..zaidi, hakuwahi kuwaza kugombea uraisi kabla ya huu uraisi wa kudura za Mungu.

..hata alipokuwa VP hakuna aliyekuwa akimfikiria kuwa kati ya warithi wa Jpm.
 
Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.

Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.

Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.

Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.
Kura za matajiri ambao huwa hawapigi kura? Mwananchi wa kawaida kwa Tanzania hii? Thubutu
 
Kura za matajiri ambao huwa hawapigi kura? Mwananchi wa kawaida kwa Tanzania hii? Thubutu
Ndio Tena mwananchi wa Hali ya chini ndio atakuwa wa kwanza kwenda kumpigia kura mh mama Samia kutokanaa na utendaji kazi wa mh Rais kuwekeza fedha nyingi katika miradi inayogusa maisha ya mwananchi wa kipato Cha chini,

Mwananchi yupi wa kipato Cha chini asiyejishughilisha na kilimo, Sasa huko mh Rais katoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini ili kupunguza Bei ya mbolea, Sasa kwa Hali hii huyu mwananchi atashindwaje kwenda kumpigia kura mh Rais

Katika Elimu ,Afya ,maji mh Rais kaweka fedha za kutosha ,miradi inayogusa maisha ya mwananchi wa chini kabisa, Sasa unafikiri utamwambia Nini mtu huyu ili asiende kumpigia kura mh Rais mama Samia suluhu Hassani wakati anaona namna mh Rais alivyo fanya kazi ya kutukuka
 
labda huyo mamayenu ajenge tanzania ya walamba asali lumumba lakin tanzania ya wananchi itampeleka zanzibar akale urojo na harua.
Mama ameijenga na anaijenga Tanzania yenye kutoa matunda kwa watu wote, hapo ulipo huoni Miundombinu ya shule, zahanati,vituo vya Afya, umeme, vipi huna mtoto au ndugu au jirani anayesoma shule ya serikali, je umesikia karudishwa nyumbani kukudai Ada? Kama hajaja Basi fahamu hiyo Ni kazi ya mama yetu mpendwa mama Samia suluhu ambaye anahitaji kuona watoto na vijana wanapata Elimu bila shida yoyote ile
 
..vilevile ni mwanasiasa asiyeweza kujieleza, na asiyevutia kumsikiliza.

..labda abebwe na mapesa ya Ccm, vyombo vya habari, na vyombo vya dola.

..zaidi, hakuwahi kuwaza kugombea uraisi kabla ya huu uraisi wa kudura za Mungu.

..hata alipokuwa VP hakuna aliyekuwa akimfikiria kuwa kati ya warithi wa Jpm.
Labda wewe uliyeamua kujipa upofu wa kazi kubwa ya kulitumikia nchi hii anayoifanya mh Rais ndio unaweza waza hivyo, hata hivyo watanzania wameona kazi za mama,mama anamvuto wa kipekeee kabisa kwa wananchi, ndio maana unaona wanakuwa na hamu ya kumsikiliza, ndio maana unaona mafuriko ya wananchi waliokuwa wakijitokeza kumlaki alipofanya ziara mikoa ya Mbeya,njombe na iringa
 
Ndugu zangu wahenga walishasema "nyota njema huonekana asubuhi", kwa kazi nzuri na ya kutukuka anayoifanya Mh. Rais katika kuijenga Tanzania mpya, ni dhahiri uchaguzi ujao utakuwa mwepesi Sana kwake kuweza kupita. Kwa Sasa hakuna mpinzani yeyote mwenye mwelekeo wala nguvu ya kuweza kuja kumtikisa Mh. Rais uchaguzi ujao.

Hii inatokana na ukweli kwamba upinzani ulikuwa unategemea makosa ya serikali ili upate ajenda na kujijenga, lakini Mama Samia Suluhu Hassani, punde tu baada ya kuapishwa ni Kama alikuwa analijua hilo. Kwa sasa ndani ya mwaka mmoja na miez kadhaa ameziba mianya yote na kuunyima upinzani ajenda na sera kwa serikali yake, kwa hiyo sasa hivi wapinzani wanashindwa wawaeleze nini wananchi, maana kila kitu kimeguswa na kufanyiwa kazi na Mh. Rais.

Ndio maana unaona wapinzani wengi sana wanamuunga mkono Mh. Rais kwa kazi kubwa anazofanya katika kuijenga nchi yetu. Hakika siasa ni sayansi na mama ameumaliza upinzani kisayansi kwa kufanya kazi wanayohitaji wananchi. Maana wananchi walichokuwa wanahitaji ni mtumishi wao, na kwa sasa Mama Samia Suluhu Hassani amepatikana, hivyo hawana muda tena na habari za vurugu, maandamano, makelele wala matusi kwa serikali.

Mama anaupiga mwingi, ni Mama hadi 2030 hapo ndiyo tutaanza mazungumzo baada ya kufika kituo hicho. Kikubwa ni maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu ili amlinde na kumpigania Mh. Rais wetu, ampatie na kumjalia uzima na afya njema.
Tunajua kuwa miaka yote CCM inazoa kura kwa mitutu ya bunduki na siyo kuchaguliwa kwenye sanduku la kura.
 
Labda wewe uliyeamua kujipa upofu wa kazi kubwa ya kulitumikia nchi hii anayoifanya mh Rais ndio unaweza waza hivyo, hata hivyo watanzania wameona kazi za mama,mama anamvuto wa kipekeee kabisa kwa wananchi, ndio maana unaona wanakuwa na hamu ya kumsikiliza, ndio maana unaona mafuriko ya wananchi waliokuwa wakijitokeza kumlaki alipofanya ziara mikoa ya Mbeya,njombe na iringa

..anabebwa na cheo cha raisi.

..hakuna raisi wa tz ambaye alitembelea mji au kijiji chochote hapa nchini halafu akapokelewa na umati mdogo.

..Ssh bila uraisi hana mvuto wowote ule.
 
..anabebwa na cheo cha raisi.

..hakuna raisi wa tz ambaye alitembelea mji au kijiji chochote hapa nchini halafu akapokelewa na umati mdogo.

..Ssh bila uraisi hana mvuto wowote ule.
Hajafika hapo kwa bahati mbaya, mh Rais Ni kiongozi kwa kuzaliwa, Ndio maana unaona alivyo ituliza nchi na Sasa inasonga vizuri kabisa bila shida
 
Wewe ni taahira kiukweli,nikikwambia Lete Takwimu za ajira zilizotengenezwa na Magufuli kama unavyodai huna..

Labda kama mlitengeneza hizo ajira kwenye vile viwanda vyenu vya vyerehani..

Mwisho,kwani miundombinu imeacha kujengwa? In fact saizi ajira za kwenye miundombinu zinazotengenezwa ni nyingi kuliko hapo awali..

Unavyozungumzia bajeti ya barabara za Tarura kutoka bil.257 hadi bil 752 ni ajira zaidi na zaidi..

Unavyozungumzia bajeti ya Wizara ya maji kutoka bil.302 hadi bil.767 ni miradi mingi zaidi na ajira zaidi..

Unavyozungumzia bil.954 kutoka bil.205 za irrigation unazungumzia ajira zaidi na zaidi.

Unavyozungumzia ujenzi wa mashule,vituo vya afya nk ni ajira zaidi na zaidi..

Taahira mwenyewe. Unajiona wa maana kumbe boys tu. Unatukana wengine kiss mama Samiah. Siwezi kubishana na wewe uelewa wako mdogo Kama panzi.
 
Back
Top Bottom