Kuna sheria zilitungwa mwishoni mwa mkwa 2014 na kuendelea zilikuwa sheria za hovyo sana ambazo wala hazina afya kwa taifa.

Hao Usalama wa taifa wana sheria zainazowaelekeza utendaji wao kazi. Tatizo ni kukosa uhuru unaotokana na kwamba Anayemteua boss wa TISS ni mwenyekiti wa chama na anahakikisha anamteua mtu wa chama pia
 
Hii bhagosha, wamejitathimini na wakakiri kuwa kuna watu waliwabambikia kesi na sasa wamefuta 147 !
Isiishie hapo tu itapendeza wakieleza uma wa watanzania nani alikuwa anawatuma na kwa minajili gani, pia warudishe zile pesa alizokuwa anapokea DPP ili kuwafutia kesi za kubambikiana watuhumiwa wote akiwemo Kabendera
 
Hiyo ya kumtafuta nani alikuwa anawatuma itakuwa sio kuliponya taifa. ni Visasi. itoshe kuzifuta kesi waliziaababisha watapata aibu tu. wanajijua na tunawajua.
 
Wamefuta au wameingia mitini hawahudhurii mahakamani!!
 
PAMOJA NAJUHUDI ZOTE HIZO ZA RAIS WETU, AMINI NA WAAMBIA MALIPO ATAKAYO YAPATA MAMA KWENYE SERIKALI YAKE JUU YA UVUNJIVU WA AMANI NA RUSHWA HAUTA SAHAULIKA, SABABU WATANZANIA HATUPO HIVYO NA HUWA TUNATAFUTA WEAK POINT
 
Well said Mama President!! Nakupa πŸ‘πŸ‘Œ

Ila tunaomba uangazie vyombo vingine vya kutoa haki sio Jeshi la Polisi na Mahakama tuu!!!

Kuna chombo kama TUME YA UTUMISHI WA UMMA. Hii taasisi imekuwa ni kero sana kwa watumishi wa Umma ambao wanakata rufaa au wanapeleka malalamiko yao.

Kama unavyoona Mahakama au Jeshi la Polisi zinavyopora haki za watu vivyo hivyo hii inatokea kwa TUME YA UTUMISHI WA UMMA.

Tume ya Utumishi wa Umma wamekuwa ni wababaishaji sana katika kushughulikia matatizo au kero zinazopelekwa na watumishi wa umma kwa njia ya rufaa au malalamiko dhidi ya waajiri wao.

Tume ya Utumishi wa Umma imekuwa; haifanyi critical review ya malalamiko na rufaa za watumishi na mara nyingi hulalia upande wa mwajiri

Tume ya Utumishi wa Umma imekuwa na tabia ya ucheleweshaji wa rufaa na malalamiko yanayopelekwa na watumishi wa umma, na mara nyingi wamekuwa too defensive!!

Ukienda kuulizia hatma ya jambo lako wanakuwa wakali na hawawi cooperative at all, customer care ni zeero kabisa ktk hii ofisi.

Nafikili hata technical know how jinsi ya kufanya kazi ni tatizo, inaonekana hata ujuzi waliokuwa nao wafanyakazi wa hii Tume ya Utumishi wa Umma ni questionable na ndio maana wanaishia kuvurunda case za watu huku zikiwa zimekaa muda mrefu.

Mama President, hii ofisi ya TUME YA UTUMISHI WA UMMA ni mojawapo ya taasisi inayoharibu na kuwanyima haki watumishi wa umma, imekuwa ni mojawapo ya vichochoro vinavyotumiwa na waajiri waliokosa maadili na kuwaharibia utumishi watumishi wa umma.

Inaonekana hii tume inatumika na waajiri kuwakandamiza watumishi wa umma. How comes, rufaa au malalamiko ya mtumishi yanakaa mwaka au hata zaidi ya mwaka bila kupata muafaka au kulikamilisha. Tume ya Utumishi wa Umma imekuwa ni mojawapo ya taasisi zinazokiuka sheria badala ya kuzisimamia na kuzifuata ipasavyo.

Tunaomba mamlaka husika ziingalie hii ofisi ya TUME YA UTUMISHI WA UMMA jinsi inavyofanya kazi ili kudhibiti upotevu wa haki za watumishi wa umma.

Asante!
 
Bongo hii askari wa usalama barabarani anaweza akague gari yako na kukuta ritisi ya bima inaisha kesho asikukumbushe ili keshokutwa akudake kuwa bima imeisha. Yaani maisha flani hivi ya kuviziana. Hiyo elimu ni ngumu kutolewa. Watu wanajificha kwenye vichaka na vitochi maeneo ambayo wanajua watu watakuwa washajisahau, lazima wakupate.
 
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====

Rais Samia Suluhu amesema Takukuru wamefuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu. Awataka Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.
Kinachotafutwa hapo ni kufuta kesi za mafisadi. Mama kashauriwa ila wenzake wanajua lengo lao nini πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mh.RAIS Mama SAMIA kwa kuwa NAFSI yako imekutuma kuamini kuwa Kuna Watanzania Wasio na HATIA lakini Wamebambikiziwa KESI na Vyombo Vyetu vya Ulinzi Tunakuomba sana Tumia MAMLAKA yako KUSHAURIANA na Vyombo Vyako ili Kuzifuta Kesi hizo kwani WATU Wanateseka MAGEREZANI na UPELELEZI Haufanyiki ili Mradi KUWAUMIZA Wapinzani. KESI
nyingi za WAPINZANI Zilikuwa Kabla ya UCHAGUZI Mkuu wa 2020 zilikuwa na LENGO la KUWAKOMOA na KUWAUMIZA.Tunakuomba Utumie HEKIMA na Na BUSARA uliyojaliwa na MUNGU KUZIONDOA.
 
Asante kwa taarifa zitafika tuendelee kupaza sauti
 
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====

Rais Samia Suluhu amesema Takukuru wamefuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu. Awataka Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.
... kumbe hii issue ya kubambika kesi nikajua ni polisi kumbe hadi TAKUKURU ipo? Dah; kwanini hao waliofungua hayo mafaili ya kubambika raia wema kesi wasitimuliwe na kushitakiwa? Huu ujinga utaendelea kutamalaki hadi lini!
 
... kumbe hii issue ya kubambika kesi nikajua ni polisi kumbe hadi TAKUKURU ipo? Dah; kwanini hao waliofungua hayo mafaili ya kubambika raia wema kesi wasitimuliwe na kushitakiwa? Huu ujinga utaendelea kutamalaki hadi lini!
Kwakweli inasikitisha na hizo ni Takukuru tu. Pata picha huko polisi ziko ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…