PreGE2025 Rais Samia: Tusi-gwajimanize chama chetu, Magwajima tuyaache huko nje. Ukicheza ngoma si yako lazima utaharibu

PreGE2025 Rais Samia: Tusi-gwajimanize chama chetu, Magwajima tuyaache huko nje. Ukicheza ngoma si yako lazima utaharibu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa maneno mengine Gwajima asithubutu kuchukua fomu ya Ubunge!
 
mlimtukana sana kwa kumuita mpole,mara sijui awe kama magufuli acheki na kima, mara sijui mahijabu,


Acha awanyooshe muwe na heshima next time..mama wa watu alianza kuongoza nchi kwakuwa muungwana kabisa, lakini mlivyo wapuuzi mkawa mnatukana mkisaidiana na watu wa team Jiwe
Alinde wanae,ukimya wa watu asiupuuze mkuu
 
Wapinzani ndani ya Chama hawewezi isha kwa kupiga biti.
Kumbe sio chura kizuei tena
 
Angalia Samia alivyofura kwa hasira!View attachment 3351087
UVCCM TUNAKWAMA WAPI SAGA YA GWAJIMA?
Na Bollen Ngetti
+255748092092
KUNA baadhi ya kauli nyingine huwa mtu mwenye akili kama wewe msomaji ukizisikia ni lazima utajiuliza maswali kadhaa juu ya mtu au taasisi inayozitoa:

Huyu mtu ni tahira kwa kuzaliwa au ametorokwa na akili ukubwani? Huyu mtu anatumia kiungo gani kufikiri kabla ya kutamka? Au je, hii ndiyo kamusi halisi ya neno chawa na uchawa? Au ni kuloa utamu na uhondo wa madaraka toka uwayo hadi utosini? Au pengine ni yote kwa pamoja?

Tunahoji maswali haya maana ukiwatazama usoni hawafanani na kauli zao. Usoni ukiwatazama ni kama watu walioshiba weledi, uelewa na maarifa lakini wakitoa tamko ndio unasema loh! Mwenye hekima Nabii Sulemani anasema, "ukimya huficha upumbavu wa mtu". Maneno haya yanasadifu uongozi wa jumuiya ya UVCCM mkoa wa Dar es salaam.

Kada wa CCM, M-Neki, Mbunge, Askofu maarufu duniani na raia mwema wa Tanzania Josephat Gwajima ameguswa na matukio ya kishetani yanayoendelea nchini ya utekaji, uteswaji, uuaji, uokotwaji au kupotea mazima kwa watu. Hakuna Mtanzania asiyeguswa na matukio haya ya kiberedhuli!

Gwajima akatoa maoni yake kama Gwajiboy akilindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Ibara ya 18(3) akivinyooshea vidole vyombo vya usalama akihoji ni kwa nini wasiweze kunusa na kuwabaini waliosilimishwa jina la "wasiojulikana"?

Gwajima anahoji iko wapi ulinzi wa uhai wa raia maana hatimaye umma utazoea maisha ya Haiti kulikosheheni magenge ya kihalifu yasiyojulikana. Gwajima ametolea mifano kwa watoto (binadamu) wa viongozi wa juu akiwemo Rais na Waziri Mkuu.

Gwajima pia kwa maoni yake ameona kuajiri na kuondoa mara kwa mara ma-DGS kwamba halina afya akapendekeza mfumo mwingine. Gwajiboy alisema mengi.

Sijaona. Narudia sijaona hoja hata MOJA ya Gwajima isiyoweza kujibiwa kwa hoja kwa vijana wa CCM walioiva itikadi na maarifa ya siasa za hoja. UVCCM ninayoijua iliyokuwa imejaa maarifa na itikadi hoja za Gwajima zingeyeyuka hewani kwa hoja mbadala!

Badala yake eti UVCCM Woodcote wa Dar es salaam wameitana, wakaketi kitako, wakatafakari na kujadili wakaona kujibu hoja za Askofu ni "akamatwe, asichukue fomu ya kugombea Ubunge popote, avuliwe uanachama". You guys are you mad? Hatua hiyo itafuta vipi hoja za Gwajima? Mbona tunadhalilisha jumuiya hii iliyowahi kuheshimiwa?

Badala yake eti Gwajima anajibiwa na comedians Mwijaku, Steve Nyerere, Baba Levo, semaji la Yanga mstaafu Jerry Muro. Sitoshangaa Kingwendu naye akitumwa kujibu hoja za Askofu. You guys huku ndiko kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kiuongozi au ndio niliyosema parandesi ya pili hapo juu?

Mjinga mwingine akakumbusha kwamba Gwajima 2020 alikuwa wa 3 ndani ya chama. Eti hiyo nayo ni hoja, "idiot" kabisa. Hivi walioteuliwa nje ya namba 1 ni Gwajima tu? Vipi na wale waliopita bila kupingwa baada ya kuwateka wapinzani huko Kusini? Nao wakamatwe na wasichukue fomu popote? Kwa nini uongozi ndani ya CCM uonekane kama hisani?

Kwa nini leo mawazo ya wana-CCM yashikiliwe na mtu mmoja. Kwamba hutakiwi kufikiri tofauti? Nijuavyo viumbe wanaofikiri sawa ni "zero brain" tukiwaita nyumbu wa mbugani ambao huwaza kula nyasi na kujamiiana tu, basi. Si binadamu wenye utashi. Gwajima ajibiwe kwa hoja tuache uvivu kufikiri! Period!
 
Hapana ..mi sifagilii mauaji na kudhuru watu...Mungu amekataza umwagaji wa damu katika ardhi....bali nimeongea ukweli mlidharau mama wa watu amehamua kuwa mkali nayeye...alitaka kuwatendea fair mkamtukana
Asante
 
Hiyo kauli haikupaswa itoke kwa rais wa nchi yaani ni kama ametia muhuri rasimi wa KIFO Cha Gwajima.
Mungu Linda watetezi wa taifa hili dhidi ya kiongozi huyu dhalimu.
HANA UWEZO WA KUMUUA JASUSI LA MBINGUNI SN SN ATATANGULIA YY
 
Hofu yangu ni kwamba isije kuwa ni mipango watu wako kazini wanacheza shoo za kikubwa... Wapinzani kuweni makini na msisahau ya Lowassa na Ukawa 2015
 
Back
Top Bottom