RC Adam Malima ashauri Serikali kuwa makini kwenye Mkataba wa DP World, ili tusipigwe kama kwenye Mikataba ya Madini

mkuu nadhani pia hujamwelewa, mheshimiwa sana Malima kakosoa kwa staha ( in your voice), shida kubwa ya ukosoaji wa kistaha ambao unapendwa sana na (supporters wa DPW), wanaunyumbulisha na kujifanya hawauelewi, ndio maana nawapenda pia wasiotumia staha (against DPW), maana wanaeleweka zaidi maana wako focused na nini.
 
Kifupi hofu aliyonayo ndio tulionao wengi, ila sababu ya ugali wake ame balance maneno.
 
Vipi Afya yako mkuu nasikia umepata ajali.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa Ruvuma ndugu Oddo K. Mwisho - Maoni ya WaTanzania yazingatiwe ili uwe wa manufaa


Mwenyekiti wa mkoa ndugu Oddo Killini Mwisho pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa NEC CCM azungumzia maoni mbalimbali kuhusu suala la bandari na ikiwa Mikataba ifuatayo mkataba-mama itarudi bungeni basi jambo sahihi litafanywa kuhusu mikataba ifuatayo ya bandari.. hivyo maoni ya waTanzania yazingatiwe, yaboreshwe na kuwa rafiki kwa Tanzania... waTanzania wasiligeuze suala hili katika sura ya udini na namna hasi ... Watanzania tuendelee kutoa maoni ili mikataba iwe rafiki na ya tija kwa nchi yetu ...
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya : Unafiki unatutesa hatuzungumzi hadharani sisi viongozi wa chama na serikali


Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dkt. Stephen Mwakajumilo awalaumu viongozi wa serikali ya CCM kushindwa kujitokeza kusema wazi kweupe badala yake wanaongea kwa vificho vichakani .... ajenda kubwa kama hii inatakiwa kiongozi kusimama katika mstari unaouamini siyo kuwa wa msimamo wa kati kwa kunyamaza kimya kwa uonga kuhusu ajenda ya bandari ... semeni kwa uwazi ili tupate jibu kwa manufaa ya nchi kukosea siyo dhambi ila kurudia kosa ndiyo makosa na historia ni mwalimu mzuri hivyo wananchi wanahaki na ni kheri kurekebishana kwa nia nzuri ...
 
Unaelewa maana yake? Kama kuna makosa yarekebishwe? Ina maana raisi alisaini agreement yenye mapungufu, je alikua hajui?
Nilipokuwa mtoto niliamini baba yangu anaweza kila kitu.
Hata hivyo, baadaye nikapata ufahamu kuwa kuna wengine ikiwa ni pamoja na mimi tunaoweza vitu tofauti na yeye.
Tuwe wakweli na kwa haki, viongozi (hasa wa kisiasa) hutegemea wasaidizi kwa asilimia kubwa.
Wanachotakiwa kufanya, ni kutafuta watu wenye weledi na werevu, watumike katika kufanya mambo sahihi kwa wakati sahihi.
Changamoto iliyopo ni kwamba, siasa zina fitina, upendeleo, kujuana, fadhila na yanayofanana na hayo. Hivyo kupata watu sahihi kwa usaidizi wenye tija na usalama ni shughuli pevu.
Kwa hiyo, viongozi wengi wa kisiasa huogelea kufuata uelekeo wa mawimbi na upepo.
 
..mbona serikali nzima, chama, na chawa wa Mama Samia, wameshupaza shingo, na wanasisitiza kwamba mkataba uko sawa?
Hii ndiyo changamoto ya siasa zetu. Yawezekana pia ni uthibitisho wa umasikini wa fikra.
Maoni na mitazamo tofauti juu ya jambo fulani ni kawaida, ila mwisho wa siku mamlaka halali zitatoa muelekeo.
 
Ni wachache walio serikalini na Mteule kusema wazi wazi kama Adam Malima, wengine wanaofia matumbo yao...
 
Hapa Mayalla naona amechemka..!!
 
Mama ananiambia sisi hatuna ndugu wa kiarabu
Hilo tatizo kubbwa sana.


Pole sana.

Mimi nna ndugu wa takriban kila taifa dunani. Wahindi, Wachina, Waarabu, Wamarekani, Ulaya, Japa.

Tanzania ndiyo usiseme.
 
Huyu U-RC wake uko shakani. Sisi tunataka tuwape bandari wajomba zetu, waarabu wa dpw , yeye anatoa ushauri feki
 
2025 inakuja na umri nao unapenda, mengine jiongeze mwenyewe .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…