RC Adam Malima ashauri Serikali kuwa makini kwenye Mkataba wa DP World, ili tusipigwe kama kwenye Mikataba ya Madini

Good japo atang'olewa kwa kusema ukweli
 
Yupo sahihi, wapo wengi wataamua kujitoa muhanga na kufunguka. Hili swala la bandari ni mwanzo wa mambo mengi yajayo. Huu ni wakati wa watu kusimama ili wahesabiwe, huko tuendapo tusije kulaumiana tu.
Ataondolewa uRC soon, maza hataki kusikia kuhusu ndugu zake waarabu
 
Bonge la ushauri kutoka kwa RC wa awamu ya sita
 
Aaah, mie wajomba zangu na mashemeji zangu hao. Lakini kwenye biashara hakuna mjomba wala shangazi, ndiivyo nilivyomuelewa Malima.
We bibi huna akili sijui ni uzee, hakuna anayepinga waarabu kuwekeza Tanzania waje hata leo jioni kinachopingwa ni terms za mkabata ziwe wazi kwa pande zote 2 wala hakuna neno sisi tunahitaji wawekezaji hatubagui dini wala rangi
 

Well said,
Ni vema wakamwelewa mwenzao.
 
This shit is getting scary mpaka RC Anampiga spana boss wake. Hapa pana shida sasa
 
K
Msijibaraguwe, hakuna mahala Malima kapinga bandari isiendeshw na kampuni ya Dubai. Kasema tuwe makini kwenye mikataba. Ambacho ni kitu sahihi kabisa.
Kwani nani alipinga bandari kuwekeza la hasaha! Kinachopingwa na wengi akiwemo Malima ni masharti yaliyomo ktk kile mnachokiita makubaliano ambayo Ndiyo yanayo ashiria kuelekea kugawa bandari zetu.

Na ametumia neno "siyo wajomba zetu" kwa walio na ufahamu hili ni neno lenye maana kubwa Sana.
 
Prof Kighoma Alli Malima na Stephen Kibona ndio Mawaziri bora wa Fedha wa Nyakati Ngumu!
Mmh, labda kibona, huyo mwingine alikuwa mwizi kama mwanae. Kwani kilichomuua si kinahusiana na ufisadi alioifanyia Nchi.
 
Mmh, labda kibona, huyo mwingine alikuwa mwizi kama mwanae. Kwani kilichomuua si kinahusiana na ufisadi alioifanyia Nchi.
Prof Malima hakufanya Ufisadi wowote ilikuwa propaganda za kumkwamisha asigombee uRais

CAG alipomchunguza pale Hazina hakukutwa na kosa lolote sana Sana Naibu Katibu Mkuu mh Mkoma ndio alionekana kutoa misamaha ya kodi kinyemela bila idhini ya Waziri

Msikaririshwe vijimaneno vya Vijiweni!
 
kwanini atenguliwe na anatowa elimu kama walivyotakiwa serikali yote, wawaelimishe wasioelewa.
Ila kwenye hii issue ya bandari NIMEGUNDUA maafsa habari wa SERIKALI na taasis zake zikiwamo wizara, wanatakiwa wajitafakari sana sana... Hawakutoa elimu ya kutosha na kutoa taarifa sahihi kwa WANANCHI na ndo MAANA Kuna mkanganyiko namna hii

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Je naye ni mdini?
 
Na sisi tumemsikia. Sasa kila mtu abaki na lake. Wewe sio mfafanuzi wake.

Hii ndio inaitwa "kukosoa kwa staha".
 
Nyie kweli ni kima!! Sasa sisi tulikua tunapinga nini na nyinyi mnaongea nini sasa hivi? Loud and clear huu mkataba wa DP World ni mpumbavu peke ake anaweza kuukubali.
Ni mkataba wa kijinga kuwahi kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…