RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Kwanini wasihamishiwe Dodoma lile soko lenye jina la mnajisi katiba halina watu lipolipo tu. Na wengine wakaanzishe mkoa mpya wa Chato.
 
Ongezeko kubwa la wamachinga lilisababishwa na biashara nyingi na miradi mbalimbali kufa.Kwa mfano Manji kufunga baadhi ya miradi yake kulisababisha rate kubwa ya unemployment
 
RC Makala amesema wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar es salaam wamekaa bila utaratibu maalumu na barabara zimezibwa na sasa wanalikaribia geti la Ikulu.

Makala amesema hali hii haikubaliki na ni lazima wafanyabiashara hao wapangwe upya katika utaratibu rasmi kwenye maeneo yote ya mkoa na waliopo barabarani na mbele ya maduka au ofisi za watu wengine wataondolewa.

Chanzo: ITV habari!
Enzi za dikteta asingethubutu kutamka hivyo
 
Njia pekee ya kupunguza tatizo la machinga mijini ni kuchochea uzalishaji vijijini,mfano fungua mipaka mtu alime auze popote hata kama ni mbinguni SAwa,usiingilie biashara ya mazao.Ruhusu wageni wasake mazao hadi uchochoronj vijijini huko.Korosho, mbaazi ufuta ukilipa nani atakubali kuunguzwa na jua mjini akiiuza kanadamili.Umachinga ni suluba sema tu njaa haizoeleki.
 
mim nauliza sheria ya mazingira inataka EIA kwa kila mradi.je mwendokas wa phase 3 mbagala mbona kunaendelea biashara pemben na katikat ya barabara pale rang 3.je kwa nn wale wasiiondolewe wapelekww mahali salama ilinkupisha mrad.? nimepita pale ujenz unaendelea mabanda kila sehem sheria inataka kuwe na noise reduction,air polltuion control na kila kitu je wale wmachibga rang 3 wapo juu ya sheria au ?
 
Tunatakiwa kwenda mbali zaidi mtaa wa congo ni machinga wamejaa mule wanazuia gari kupita na wenye maduka kufanya biashara. Wale wote watengewe maeneo mengine.
 
Mara nyingi huwa nasema humu kwamba mambo mengi ya humu mitandaoni huwa si picha halisi ya huko mitaani ila watu huwa wananikatalia.
Nadhani wengi ni watoto wa shule za kati au watu wanajitoa uelewa.
Kuna vitu huwa ni automatic vinaji create.
Mfano mfumo wa nchi ni rushwa unyanyasaji na uonezi tegemea vurugu, maandamano. Uporaji na aina zake.
Hawa chinga wameletwa na mfumo i.e umaskini, kukosa ajira, kukosa motisha kwa wakulima lkn zaidi usimamizi mbovu wa serkali.
Jiulize mtu kituo cha mafuta katikati ya makazi tena eneo sqm za high density mika 20 baadae unataka kumvunjia huku ulikuwa unachukua kodi zake.
Ni uhuni tu.
Kiki za kisiasa , na kutafuta temporal popularity
 
Back
Top Bottom