Ruble ya Urusi inazidi kuchanja mbuga kwa kuongezeka thamani

Ruble ya Urusi inazidi kuchanja mbuga kwa kuongezeka thamani

Uchumi hauimariki kupitia fedha, uchumi unaimarika kwa kuongeza uzalishaji na biashara. Kama uzalishaji wako na biashara vinapungua pesa yako hata iwe na thamani ya aina gani haina maana kwako.
Mbona hata yetu hatuitumii popote nje ya bongo. Kikubwa uchumi wa warusi uimarike kupitia fedha yao
 
Poundi ya UK inatumika sana kwa sababu UK inauza sana nje bidhaa za thamani kubwa na wafanyabiashara wa UK hupenda kutumuia paundi yao kuliko dolar.
paundi ya muingereza haitumiki sana nje Zaidi ya palepale UK lakini inathamani kubwa kuliko dollar au euro...hii kitaalamu kwani imekaaje?
 
Kwacha ya Zambia inapaa lakini mataifa mengi hayajaanza kuihitaji kuitumia.

Biashara ya kimataifa inapendelea pesa ambayo ni tulivu "stable" sio pesa inayoyumba kama mlevi wa gongo au iliyo kama maji kupwa na kujaa.

Pesa ikiwa ina tabia ya kupanda thamani sana tofauti na uhalisia wa uchumi wake ni tatizo na ikishuka sana ni tatizo pia katia biashara na kuweka akiba kupitia hiyo pesa.
Ungekuwa unafahamu financial markets zinavyofanya kazi usingeuliza swali kamma hili. Maana Kama ruble itazidi kupaa Ina maanaa mataifa mengi yataaanza kuitaji kuitumia ..
 
China akihamia kununua mafuta ya bei rahisi Russia ina maana atapunguza manunuzi Uarabuni na Africa, hiyo ni hasara kwa Africa, hiyo inamaanisha Uarabuni na Africa inabidi wauze Ulaya.

China anahitaji dollar zaidi kuliko ruble kwa sababu biashara yake kubwa iko US, Ulaya, Japan, Australia na nchi nyingine nyingi kabla ya Russia. Fahamu Russia hayuko hata top ten ya washirika wakubwa wa biashara wa China. Hiyo inamaanisha rubles anazohitaji China ni za kununua mafuta na gesi tu ya Russia, hakuna kitu kingine kikubwa anaweza kupata kutoka huko. Hiyo inamaanisha China atahitaji Russia anunue kwa Dollar au Yuan.

China is the Industry of the World.., pale production ya ulimwengu ndipo inapofanyika..., Production needs Energy / Nishati and cheap energy will lower production costs....,

Wewe ukienda pale kununua vitu vyako watachukua dollar yako na rubble yako pia kama unayo (sababu it means cheap energy) na hio dollar yako wataendelea kuwa nayo deposit (ukizingatia hata sasa wanayo ya kumwaga)...,

Kama pesa yako inamaanisha cheaper products kwako basi watu wataitafuta tu pesa yako..., ndio maana mchina haya mambo ya currency yake kuwa na gharama sana aliachana nayo na alishalaumiwa kwa makusudi ku-devalue currency yake ili always iwe cheaper than dollar which means cheaper products....
 
Njia pekee ya kupambana kutoka ni kuzalisha na kuuza nje vitu vya thamani zaidi ya Marekani na Ulaya, tofauti na hapo ni porojo tu.
Mataifa yanapambana kutoka kwenye huo mfumo wa fedha sijui SWIFT Ina maaana fedha za Russia na mataifa mengine wataweza kufungua mipaka na kuifanya baisha hata Hadi huku Africa, labda USA na wenzake watumie mbinu chafu mfano kuanzisha vurugu, vikwazo ili kuua Izo movement .. otherwise kila kitu kinawezekana. Kwani wewe ukiwa na ruble saiv huwezi kuitumia?
 
Uchumi wa Russia ni mdogo kuliko majimbo ya California au Texas, malighafi zote alizo nazo Russia Marekani wanazo na wana uwezo wa kuzipata nyingine Canada, Mexico, South America, Australia na Africa.

Hakuna marriage made in heaven or hell ya maana itakayotokea kati ya China na Russia kwa siku za karibuni kwa sababu ya maono yao tofauti kabisa na pia hata kama hiyo marriage itatokea itakuwa ni ya Tajiri kumuoa maskini amsaidie.
Unajua unachokiongea !!!?????

Kwanini America hizo industry hasiziweke kwake au unadhani anamfanyia hisani China ?!!, In short walijaribu kurudisha Apple plant America ila ni kwamba haiwezekani, huwezi uka-beat production cost ya China..., China was once a Giant, who slept and now the Sleeping Giant is awakening, there has been a slow but gradual shift of economic power from west to east..., hata kabla ya hizi shenanigans, de-dolarization was already a thought.... Na hapa simaanishi Russia as the only Player ingawa yeye kwa malighafi zake akiwa bega kwa bega na hawa jamaa it will be a marriage made in heaven...
 
Growth huwa inafika peak, ukiona chumi za Ulaya na Marekani zinakuwa kwa asilimia 2 au 3 kwa miongo ni kwa sababu zimefika peak yao, na China itafikia huko. Ni suala la muda tu
Unaongea nini mkuu labor laws na unions zote duniani hazina meno kama zamani ndio system ya demand and supply..., tofauti ya China has a One Party State wanachoamua kinakwenda sio kama nchi nyingine watu kuanza kubishana Bungeni na wananchi kugoma na kuandama..., Hili China halipo..., Kule ndio msemo wa Kazi iendelee..., ni kweli inaendelea..., China being the World manufacturer haijaja kwa bahati mbaya..., many things zinachangia ikiwe cultural attitudes...
 
Itafika mahali uchumi wa China utaelekeza wafanyakazi wa China wapate malipo sawa na wenzao wa Ulaya na Marekani. Siku cheap labour ikikata China watu wataibukia kwingine duniani kuweka viwanda vyao.
Sasa naona tumehamia kwenye stories za Gahawa...., unadhani zile kazi ambazo zinaenda China au production kufanyika China America wanapenda ? Kunda industries nyingi ambayo America ilikuwa inaongeza ila mchina amechukua, na bado kufanya kwake biashara na Africa na kutoa misaada without question asked ni threat kwao...

Make no mistake urafiki wao ni wa convenience, na huwezi kushindana na mchina mtu ambaye wananchi wao wamezoea / wameishi kwenye maisha ya kawaida miaka na miaka, kwao shida ni kawaida tofauti na wala Bata (western countries) na hicho China ndio anachowashindia na atakachoendelea kuwashindia yaani kama America ni Prima Donna basi China ni Grafter....
 
Itafika mahali uchumi wa China utaelekeza wafanyakazi wa China wapate malipo sawa na wenzao wa Ulaya na Marekani. Siku cheap labour ikikata China watu wataibukia kwingine duniani kuweka viwanda vyao.
Mkuu china inawekeza kwenye robots na AI hii itafanya production cost iwe chini..... Bila kujali kuongezeka kwa GDP
 
1.Raia wa Urusi wamewahi kuandamana mara nyingi tu dhidi ya Putin kabla hata ya huu uvamizi na vikwazo.

2.Maisha ya Raia wa Russia yatakuwa magumu tu hata Ruble ikilingana na dola, kwa sababu urahisi wa maisha huletwa na upatikanaji wa bidhaa na huduma. Kama bidhaa hazipatikani hata ukiwa matrilioni ya dolla ndani haisaidii.

3.Vikwazo vinawalenga zaidi "Oligarchs" na inner circle ya Putin ambao wamezoea bata za magharibi kwa sababu hao ndio wanaoweza kumpa Putin presha amalize uvamizi wake. Marekani na Ulaya wanafahamu vyema Putin hajali maisha wanayopitia raia wake wengi wa kawaida na wala raia wa kawaida hawawezi kumtoa madarakani kwa maandamano. Kila walipojaribu kufanya hivyo wameishia jela.
Ww jamaa umejaa makamasi kichwani badala ya ubongo yaani watu wana kuelewesha lakini bado umekaza kichwa tu kwenye hamna.
Alafu aliye kwambia Urusi inataka pesa yake itumike dunia nzima ninani?lengo kuu la Urusi ni kulinda thamani ya sarafu yake kwa manufaa ya raia wake na sio ww.

Kwanza lengo la kwanza la nchi za magharibi lili kuwa ni kuyafanya maisha ya raia wa Urusi kuwa magumu na ili raia waichukie serikali yao ili kusababisha machafuko.

Na ili hilo lifanikiwe walilenga kuuwa thamani ya pesa ya Urusi ili kusababisha mfumuko mkubwa sana wa bei, lakini hilo limeferi vibaya sana badala yake mfumuko wa bei umehamia kwenye nchi zao.
 
Pamoja na udikteta wote huo China bado iko kwenye joto kali la Covid mpaka sasa na baadhi ya miji wameanza lockdowns tena wakati wenzao wa magharibi wanaendelea na maisha kama kawaida.

Usisahau kwamba China huwa ina tabia ya kuficha taarifa, kuna uwezekano mkubwa ndilo taifa lililoathirika na Covid kuliko mengi ya Ulaya au Marekani.
Aisee unachoongea ni ukweli mtupu Kuna channel inaitwa CGTN documentary inaonesha maisha halisi ya serikali ya china na raia wa China walivyo ni hivyo hivyo unavyoongea vijana nahisi hawafahamu ilo . Kule wakisema zero covid[emoji1] hakuna kuandamana hio tayari imeshapitishwa kinachobaki ukelezaji tofauti kubwa sana na zinazoitwa Democratic state Mara walumbane bungeni paka wakubaliane muda mwingi utakuwa umepita
 
Jack Ma alifanya nini hadi wakamuweka detention?
Unakumbuka walichomfanya jack ma [emoji1] hatorudia tena China[ CPC ] ni kubwa kuliko mtu yoyote pale china hata huyo Xi Jinping so lolote mbele ya china na chama cha CPC .labda mzimu wa Mao Zedong ndio mkubwa kuliko mtu yoyote pale china . Mtu yoyote atakaye jifanya mkubwa kuliko china na chama cha CPC lazima ale kibano. Huyo jack ma ni mtoto waliomlea wenyewe China[ CPC] hawezi kuwasumbua hata kidogo[emoji1] .kamsome yule tajiri fisadi bao xilai China[CPC ] walimfanya nini sembuse kidagaa jack ma ambaye Hana influence kubwa china[emoji1]
 
Hawakujiondoa, Russia haijawahi kuwa na biashara kubwa na Africa. Hiyo biashara kubwa na Africa walikuwa wanatuuzia nini?

Hata sasa hivi biashara kubwa ya Russia kwetu Africa na sehemu nyingine ni Ngano na Silaha tu wakati wenzao US, Ulaya, Japan na China wanauza karibia kila kitu hapa kwetu na kwingine duniani. Hakuna cha maana wanachonunua kutoa Africa.
Rubble unaipimia Tanzania [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] mbona hili ni jambo la kuchekesha.

Kumbuka 1991 baada ya kuanguka Soviet, walijiondoa au kupunguza kufanya biashara na nchi nyingi za kiafrika.
Ila kuanzia 2010 walianza comeback na uwekezaji mkubwa ulifanyika Misri.

Ila walikuwa na plan kuingia maeneo mbali mbali ya Afrika.

Nafikiri unafahamu kinachotokea afrika ya kati, Mali, Niger mpaka Tchad.
 
1.JF Kuna wajinga wengi sana na huwa wana like posti za kijinga kwa sababu ni wajinga. Usipime hoja kwa likes.

2.BRICS ni umoja kituko ni kama AU tu hata haihitaji kuongelewa hapa.

3.Marekani ianazalisha mbolea yake na kiasi inachoagiza nje asilimia 83 ni kutoka Canada, msipende kulisha watu matangopori.
Ukiona hata like Moja huna ujue ulichozungumza siyo kabisa. Ujue brics ilishaliweka hili jambo la kuitumia fedha mbadala katika vikao vyake vya mwanzo Kama unakumbukumbu za vikao vyao. Kwa hiyo hii ni utelezaji wa mpango huo. Kwa rasilimali ilizo nazo Urusi usitegemee fedha Yao ishuke. Licha ya mafuta na gesi ni wauzaji wakubwa wa mbolea duniani hata Amerika anategemea mbolea Yao. Ni wauzaji wakubwa wa mazao ya kilimo, mbao n.k. Vitu vyote hivyo haviepukiki duniani.
 
Back
Top Bottom