Ruble ya Urusi inazidi kuchanja mbuga kwa kuongezeka thamani

Ni mkubwa ukilinganisha na nchi yako ila ni mdogo ukilinganisha na California, Texas, Ufaransa, Italia n.k
Kwenye uchumi wake upi Mkuu??,au unataka kusema kwamba uchumi wake ni mdogo??
 
Uchumi hauimariki kupitia fedha, uchumi unaimarika kwa kuongeza uzalishaji na biashara. Kama uzalishaji wako na biashara vinapungua pesa yako hata iwe na thamani ya aina gani haina maana kwako.
Mbona hata yetu hatuitumii popote nje ya bongo. Kikubwa uchumi wa warusi uimarike kupitia fedha yao
 
Poundi ya UK inatumika sana kwa sababu UK inauza sana nje bidhaa za thamani kubwa na wafanyabiashara wa UK hupenda kutumuia paundi yao kuliko dolar.
paundi ya muingereza haitumiki sana nje Zaidi ya palepale UK lakini inathamani kubwa kuliko dollar au euro...hii kitaalamu kwani imekaaje?
 
Kwacha ya Zambia inapaa lakini mataifa mengi hayajaanza kuihitaji kuitumia.

Biashara ya kimataifa inapendelea pesa ambayo ni tulivu "stable" sio pesa inayoyumba kama mlevi wa gongo au iliyo kama maji kupwa na kujaa.

Pesa ikiwa ina tabia ya kupanda thamani sana tofauti na uhalisia wa uchumi wake ni tatizo na ikishuka sana ni tatizo pia katia biashara na kuweka akiba kupitia hiyo pesa.
Ungekuwa unafahamu financial markets zinavyofanya kazi usingeuliza swali kamma hili. Maana Kama ruble itazidi kupaa Ina maanaa mataifa mengi yataaanza kuitaji kuitumia ..
 
China akihamia kununua mafuta ya bei rahisi Russia ina maana atapunguza manunuzi Uarabuni na Africa, hiyo ni hasara kwa Africa, hiyo inamaanisha Uarabuni na Africa inabidi wauze Ulaya.

China anahitaji dollar zaidi kuliko ruble kwa sababu biashara yake kubwa iko US, Ulaya, Japan, Australia na nchi nyingine nyingi kabla ya Russia. Fahamu Russia hayuko hata top ten ya washirika wakubwa wa biashara wa China. Hiyo inamaanisha rubles anazohitaji China ni za kununua mafuta na gesi tu ya Russia, hakuna kitu kingine kikubwa anaweza kupata kutoka huko. Hiyo inamaanisha China atahitaji Russia anunue kwa Dollar au Yuan.

 
Njia pekee ya kupambana kutoka ni kuzalisha na kuuza nje vitu vya thamani zaidi ya Marekani na Ulaya, tofauti na hapo ni porojo tu.
 
Uchumi wa Russia ni mdogo kuliko majimbo ya California au Texas, malighafi zote alizo nazo Russia Marekani wanazo na wana uwezo wa kuzipata nyingine Canada, Mexico, South America, Australia na Africa.

Hakuna marriage made in heaven or hell ya maana itakayotokea kati ya China na Russia kwa siku za karibuni kwa sababu ya maono yao tofauti kabisa na pia hata kama hiyo marriage itatokea itakuwa ni ya Tajiri kumuoa maskini amsaidie.
 
Growth huwa inafika peak, ukiona chumi za Ulaya na Marekani zinakuwa kwa asilimia 2 au 3 kwa miongo ni kwa sababu zimefika peak yao, na China itafikia huko. Ni suala la muda tu
 
Itafika mahali uchumi wa China utaelekeza wafanyakazi wa China wapate malipo sawa na wenzao wa Ulaya na Marekani. Siku cheap labour ikikata China watu wataibukia kwingine duniani kuweka viwanda vyao.
 
Itafika mahali uchumi wa China utaelekeza wafanyakazi wa China wapate malipo sawa na wenzao wa Ulaya na Marekani. Siku cheap labour ikikata China watu wataibukia kwingine duniani kuweka viwanda vyao.
Mkuu china inawekeza kwenye robots na AI hii itafanya production cost iwe chini..... Bila kujali kuongezeka kwa GDP
 
1.Raia wa Urusi wamewahi kuandamana mara nyingi tu dhidi ya Putin kabla hata ya huu uvamizi na vikwazo.

2.Maisha ya Raia wa Russia yatakuwa magumu tu hata Ruble ikilingana na dola, kwa sababu urahisi wa maisha huletwa na upatikanaji wa bidhaa na huduma. Kama bidhaa hazipatikani hata ukiwa matrilioni ya dolla ndani haisaidii.

3.Vikwazo vinawalenga zaidi "Oligarchs" na inner circle ya Putin ambao wamezoea bata za magharibi kwa sababu hao ndio wanaoweza kumpa Putin presha amalize uvamizi wake. Marekani na Ulaya wanafahamu vyema Putin hajali maisha wanayopitia raia wake wengi wa kawaida na wala raia wa kawaida hawawezi kumtoa madarakani kwa maandamano. Kila walipojaribu kufanya hivyo wameishia jela.
 
Pamoja na udikteta wote huo China bado iko kwenye joto kali la Covid mpaka sasa na baadhi ya miji wameanza lockdowns tena wakati wenzao wa magharibi wanaendelea na maisha kama kawaida.

Usisahau kwamba China huwa ina tabia ya kuficha taarifa, kuna uwezekano mkubwa ndilo taifa lililoathirika na Covid kuliko mengi ya Ulaya au Marekani.
 
Jack Ma alifanya nini hadi wakamuweka detention?
 
Hawakujiondoa, Russia haijawahi kuwa na biashara kubwa na Africa. Hiyo biashara kubwa na Africa walikuwa wanatuuzia nini?

Hata sasa hivi biashara kubwa ya Russia kwetu Africa na sehemu nyingine ni Ngano na Silaha tu wakati wenzao US, Ulaya, Japan na China wanauza karibia kila kitu hapa kwetu na kwingine duniani. Hakuna cha maana wanachonunua kutoa Africa.
 
1.JF Kuna wajinga wengi sana na huwa wana like posti za kijinga kwa sababu ni wajinga. Usipime hoja kwa likes.

2.BRICS ni umoja kituko ni kama AU tu hata haihitaji kuongelewa hapa.

3.Marekani ianazalisha mbolea yake na kiasi inachoagiza nje asilimia 83 ni kutoka Canada, msipende kulisha watu matangopori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…