Bwana Utam
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 19,559
- 36,514
Marekani wangekua wanajali raia wao wasingekua wanalala nje kama maeneo fulani ya nchi fulani pale EA1.Raia wa Urusi wamewahi kuandamana mara nyingi tu dhidi ya Putin kabla hata ya huu uvamizi na vikwazo.
2.Maisha ya Raia wa Russia yatakuwa magumu tu hata Ruble ikilingana na dola, kwa sababu urahisi wa maisha huletwa na upatikanaji wa bidhaa na huduma. Kama bidhaa hazipatikani hata ukiwa matrilioni ya dolla ndani haisaidii.
3.Vikwazo vinawalenga zaidi "Oligarchs" na inner circle ya Putin ambao wamezoea bata za magharibi kwa sababu hao ndio wanaoweza kumpa Putin presha amalize uvamizi wake. Marekani na Ulaya wanafahamu vyema Putin hajali maisha wanayopitia raia wake wengi wa kawaida na wala raia wa kawaida hawawezi kumtoa madarakani kwa maandamano. Kila walipojaribu kufanya hivyo wameishia jela.
Sent using Jamii Forums mobile app