Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

KABISA,
Hapa Inabidi wazazi waingilie Kati.

This is not fair, tunaharibu Watoto wetu kwa kuendekeza upuuzi wa watanionaje Mimi.
Tunaendeshwa sana na Mentality.

Mtu anaishi Tabata anataka kumpeleka Mwanaye shule iko Mbezi Beach, kisa workmates wake wamepeleka watoto wao kule.

Kiufupi kuna ujinga mwingi sana unaendelea kwa habari ya haya mashule na Wazazi tumeupokea kama Mazombie.

Pia kuna hili suala la watoto Wa Madarasa ya mitihani kulazimishwa kukaa Bweni.
 
Kwani mmelazimishwa kupeleka watoto kwenye hizo shule?

Wabongo mnapenda kulalama sana, peleka mtoto shule ya jirani, au ww hamia jirani na shule husika.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au vinafikia kwenye tv vinakutana na vikatuni vya Tom and Jerry! Mbona ndiyo vitakodoa macho hadi saa 12 jioni ndiyo kanaanza kusinzia huku homework ikimsubiria!!!
Si heri Tom & Jerry

Sikuizi kuna makatuni ya hovyo hovyo!

yani watoto wanaharibiwa sana.
 
Reactions: nao
Wee naona tunaogea vitu viwili tofauti.
 
Swala hapa ni kuangalia ni kwanini watoto wanasoma hiyo shule ya mbali, kama sababu ni ubora wa viwango na serikali haiwezi kuvitoa katika shule za kata basi waruhusu wawekezaji waongeze shule ili watoto wasiteseke.
Hivi kwani wawekezaji hawaruhusiwi kuongeza shule?
 
hii inashangaza sana, nakaa eneo A
kuna siku niliamka saa 10 alfajiri kuwahi basi Ubungo
kituo cha daladala nakutana na wanafunzi (O-Level) wa Zanaki na Jangwani, ni mwendo wa 35 km mpaka uko Zanaki
ilihali eneo hilo kuna shule za sekondari kadhaa,
Kwann Zanaki na Jangwani wasiweke boarding kwa level zote? Maana ni shule kongwe, ambazo za level ile ni bweni kwa level zote,
 
Hilo ndio tatizo kubwa , sijui Hao wazazi hawana huruma kwa watoto wao. Shule nzuri ziko karibu kila sehemu siku hizi, hakuna ulazima wa mtoto kupelekwa shule za mbali.
 
Au vinafikia kwenye tv vinakutana na vikatuni vya Tom and Jerry! Mbona ndiyo vitakodoa macho hadi saa 12 jioni ndiyo kanaanza kusinzia huku homework ikimsubiria!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…