Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

Nani amekwambia hawachunguzi kwani jarada limefungwa? Mrudisheni dereva aje ayatambue magari yale yaliyokamatwa. Uchunguzi unaanza na maelezo ya watu wazima muhimu waliokuwepo eneo la tukio. Hata ao wachunguzi wa nje wataanza na hao.
Jarada - jalada
 
Sasa itajulikanaje kama baada ya jamaa kuwa mzima hao walioshindwa kumuua hamkuwachukulia hatua?pia hivi kinacho ua ni MTU au risasi?maana kama risasi zilimpata na amekuwa mzima hamuoni kuwa ni mkono waMungu?Acheni kujifau jambo hili lingekupata wewe mama sijui ingekuwaje
 
..kuna comment alitoa kuhusu wabunge wa vyama vya upinzani wakati wa bunge maalum.

..nadhani kulitokea mzozo na wabunge hao wakaamua kutoka nje ya ukumbi, sasa kuna kauli aliitoa ndio ilinifanya nijue kwamba iko siku tabia zake zitakuja kujulikana/kujitokeza waziwazi.

..Mama Samia alimtembelea Tundu Lissu akiwa hospitali Nairobi na alimkuta katika hali mbaya sana akiwa bado kitandani.

..Na waTz wengi tulimpongeza kuwa amefanya jambo la kiungwana. Sasa imekuwaje mtu ambaye alimuona TL akiwa kitandani ni mgonjwa, leo aanze kumtolea maneno ya kashfa? Kwa maoni yangu ni afadhali maneno hayo yangesemwa na mtu ambaye hakumuona TL kule hospitali.

..Na kibaya zaidi yamesemwa na mwanamke ambaye tunajua ana uchungu wa kuzaa,na anajua machungu ya kuuguza kwani kwa mila zetu wanawake ndiyo wanaouguza na wafariji ktk familia zetu.
Na yeye ni mhuni kama wanaccm wengine tu bunge la katiba walivuruga na mzee Sita
 
Hapo kasema ukweli mtupu Maana yeye ndo miongoni mwa maboss wa Askari wao wa CCM hivyo anawajua vizuri weredi wao. Kwahiyo Mimi naamini alichokisema na ndo uhalisia.

Zitto aliutaka uenyekit wa chadema akafukuzwa Chama.
Ben sanane aliutaka uenyekit wa Chama akapotea mpaka leo.
Tundu lissu aliutaka uenyekiti wa Chama akapigwa na vitu vinavyosadikika ni risasi.
F. SUMAYE aliutaka uenyekiti wa Chama akaambiwa kuwa Sumu haionjwi kwa usalama wa maisha yake akaamua kujiweka pembeni na kuchomoka kwenye himaya za mtia Sumu.

Swali; kwanini Kila anaeutaka uenyekiti wa Chama CDM anapatwa na matatizo Ni ipi Siri iliyopo Hapo nyuma?

Je nikweli Mbowe Ni kibaraka wa serikali kwamba hawezi kutoka kwenye kile kiti kwa masilahi ya Taifa?
Mkuu nafikiri umesahau kujiuliza maswali ya aliyewatoa walinzi wote wa kwenye nyumba za viongozi.
Pili hebu jiulize hata aliyetoa CCTV cameras.
Tatu jiulize kwanini interejensia ya polisi haikupata taarifa kama wanavyopatataga taarifa kwenye vikao au mikutano ya ndani ya chadema?
 
Huyo mama ni mafia toka zamani huwa nashangaa watu wanaompamba humu.

Yeye na mzee Sita walishiriki kuvuruga mchakato wa katiba mpya ndiyo maana akazawaidiwa umakamu wa rais


Hii binafsi nakumbuka aiseee hafai
 
Huyu mama namtaka ndani ya masaa 24 aombe radhi umma kwa kumtusi mkombozi wa wanyonge kwa kejeli, la si hivyo tutamvua heshima yake aliyojijengea kwa miaka mingi.
 



Mama Samia Suluhu Hassani ambaye ni Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) amesema kuwa anawaomba wafanye kampeni kwa amani wakipita wawasikilize wala wasigombane nao.

Amesema kuwa wapo wagombea watakwenda kuwaambia kuwa walivunjwa miguu na mwingine alimsikia akisema kuwa alipigwa risasi 16.

''Watakuja kuwaambieni wamevunjwa miguu lakini waulizeni ilikuwaje wakavunjwa miguu, wengine jana nilisikia mmoja anasema amemimiwa risasi 16 nataka niwaambie huyo sio askari wetu wa serikali ya chama cha Mapinduzi, askari wetu akipiga mtu tatu akamkosa atawajibika sikwambii askari aliefundishwa akapiga 16 huyo mtu atoke mzima".
tutawa jua wengi sana
 
Keshalipata, kigogo Keshafungua file lake huko twitter 😂😂😂😂

Daaah!! Ila kigogo 2014 mwanaharamu yule jamaa. Kujua teknolojia kunafanya awanyanyase sana Lumumba 😂😂😂
Duh! Kasemaje? Imenipita!😀
 
Back
Top Bottom