#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Uchumi tayari ulikuwa umeshashuka miaka mingi tu. Kulinda afya na uhai wa raia kwa kuwaambia ukweli ili wajilinde na kuepuka misongamano ni muhimu sana kuliko kusema uongo eti unalinda uchumi, uchumi ambao tayari ulishatetereka hata kabla ya COVID-19 ndiyo sababu wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara wote wanalia kuhusu uchumi mbovu uliosababishwa na sera za KUKURUPUKA kuingia gharama kubwa za mambo yasiyo na kipaumbele kwa Watanzania.
All good ideas. Lakini angalia biashara zitazokufa. Watu wengi kupoteza ajira. Uchumi kushuka sana.
 
"Binadamu ana uwezo wa ku-adapt and survive?"

Takwimu za kuonyesha uelekeo huo waja ziko wapi?

Kwa nini jitihada kubwa mno ya kuhalalisha kutokuchukua hatua yoyote dhidi ya ugonjwa huu ni option bora zaidi kwa mijamaa ya chama fulani?
Ziko hapa, kwako, wewe ni mzima unaweza kupost JF.

Nafikiri ni muhimu wote tuchukue tahadhari.
 
How do you expect any prosperity, progress where all people are dead. Maskini wa kutupwa. Kisa wamefungiwa kufanya biashara halali.

Nani kasema watu wafungiwe kufanya biashara milele?

Nani kasema kuchukua hatua dhidi ya corona "it means all people are dead that you then lack prosperity and progress?"

Hivi uhalali wa hata kuwakamua kodi zaidi wananchi hohe hahe hawa wanaokabiliwa na janga la ugonjwa huu maana yake nini?

Miradi kwenye dharura za majanga kama haya husimamishwa na vipaumbele hubadilika kutegemeana na hali halisi. Mwuungwana huwezi kuukana ubinadamu.

Maisha yana changamoto zake na mojawapo ni kama hizi za huu ugonjwa. Changamoto hukabiliwa.
 
Uchumi tayari ulikuwa umeshashuka miaka mingi tu. Kulinda afya na uhai wa raia kwa kuwaambia ukweli ili wajilinde na kuepuka misongamano ni muhimu sana kuliko kusema uongo eti unalinda uchumi, uchumi ambao tayari ulishatetereka hata kabla ya COVID-19 ndiyo sababu wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara wote wanalia kuhusu uchumi mbovu uliosababishwa na sera za KUKURUPUKA kuingia gharama kubwa za mambo yasiyo na kipaumbele kwa Watanzania.
Bak kuna vitu Magufuli amezifanya, kama tuko fair tumpe credit. Amekosea sehemu fulani.

Amewasaidia wakulima, kuimairisha nidhamu serikalini, kuwasaidia maskini, kukusanya mapato.
 
Ziko hapa, kwako, ni mzima unaweza kupost JF.

Nafikiri ni muhimu wote tuchukue tahadhari.

Hivi na waliokwisha tangulia mbele za haki kwa ugonjwa huu na familia zao nao ulichoandika kinawahusu?

Au kwa kuwa tu wewe haujakusibu basi na ndiyo sasa dunia nzima iko salama na haipo haja ya takwimu sahihi?

Dalili za ubinafsi uliopitiliza!

Mbona mawazo duni namna hiyo jombi?
 
Sioni chochote alichokifanya zaidi ya kuwadhulumu wakulima, wafanyabiashara na wafanyakazi haki zao za mabilioni kama siyo matrilioni, kauwa Watanzania wengi wasio na hatia yoyote ile pia kawabambikia kesi Watanzania chungu nzima na kuwapora vijisenti vyao kwa kisingizio cha kuwatoza faini za kesi FAKE. Ni janga la Taifa huyo na ndiyo sababu Watanzania wengi wanamchukia sana hata kumuombea mabaya.
Bak kuna vitu Magufuli amezifanya, kama tuko fair tumpe credit. Amekosea sehemu fulani.

Amewasaidia wakulima, kuimairsha nidhamu serikalini, kuwasaidia maskini, kukusanya mapato.
 
Brazaj taratibu!

Taratibu? Pana dharura panapo maamuzi sahihi pana maisha mengi ya kuokolewa. Wajibu nambari moja wa serikali ni kulinda maisha ya watu.

Kushindwa au kutoonyesha jitihada za kutosha katika kuyalinda maisha ya watu kwa sababu yoyote ile ni kujikosesha uhalali wa kuwapo madarakani wewe mwenyewe.

Tuna ugonjwa unauwa. Tukubali hilo na tukubaliane kuukabili. Wataalamu wa afya wapo. Hakuna aliye bora kuwazidi wataalamu wa afya katika hilo.

Tatizo liko wapi hapo?
 
Hivi ninyi mmeweka mkataba wa kibiashara na huyu jamaa anaitwa korona, au!??? Mbona HIV hamsemi!??? Tokeni huko na unafiki wenu!
 
Labda unashindwa kutofautisha Kati ya Tanzania na Zimbabwe kuwa Ni nchi mbili tofauti.
KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE.
kwa anavyojua mwenyewe
 
Labda unashindwa kutofautisha Kati ya Tanzania na Zimbabwe kuwa Ni nchi mbili tofauti.
KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE.
kwa anavyojua mwenyewe

Pamekuwapo na angalizo pia, "Tanzania si makao mkuu ya Mungu."

Mwenye masikio na asikie.
 
Inahitajika elimu.
Sio kila anayewekewa ventilator basi ANAUMWA CORONA..
Kwani kabla ya Corona hakukuwa na matumizi ya ventilator?.
Ukiingia ICU AU EMERGENCY hakuna ventilator? Je wale wote waliowekewa Wana Corona?
MABEBERU wanatuonea wivu na uchumi wetu na wanawatumia wapinzani.

HAKUNA CORONa ILA tu ugonjwa wa NEMONIA UPO.
 
Inahitajika elimu.
Sio kila anayewekewa ventilator basi ANAUMWA CORONA..
Kwani kabla ya Corona hakukuwa na matumizi ya ventilator?.²
Kulihitajika elimu au takwimu?

Elimu ipi unayoitaka wewe?
 
Sio kila anayekufa kwa kushindwa kupumua basi kafa na Corona.
Kama NI hivyo wale wote waliopo ICU na emergency ROOM WOTE WANA CORONA .
Maana wanashindwa kupumua ndo maana wanawekewa ventilator

Si unajua pia kuwa si kila mtu anayekufa kwa kushindwa kupumua kuwa hajafa kwa Corona?

Mwarobaini kwenye hilo si ilikuwa takwimu sahihi za nani kafa na nini?

Kwanini nguvu kubwa kuhakikisha takwimu kuhusiana na corona pekee hazipo? Yote hii haikufikirishi?
 
Pia mungu anasema "NIOMBENI NITAWAJIBU".
CHAGUO NI LAKO

Kwa hiyo suala la ugonjwa huu sisi kama nchi mwenye kutujibia ni Mungu?

Huyu Mungu anatujibia Corona tu au kuna mengine pia?

Jambo lipi jingine analotujibia ili tuwe na list kamili ya mambo ambayo tumeyakabidhi kwa Mungu ili tusiwahoji tena wasiohusika?

Ushauri wa bure tukabidhi magonjwa yote kwa Mungu ili tufunge kabisa mahospitali. Tukabidhi mambo ya ulinzi na usalama kwa Mungu ili polisi, na wote katika sekta hii wapewe mjukuu mengine.

Tukabidhi utawala wa nchi hii kwa Mungu ili sote tuishi katika mazingira sawa na ya amani.

Tukabidhi miradi ya maSGR, Stiggler's Gorge na mingine mikubwa mikubwa kwa Mungu ili kwa miujiza ikamilike mara moja.

Zaidi zaidi tukabidhi nchi kwa Mungu ili uchumi upae mara moja tokea tulipo na kuwa uchumi wa kwanza.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
kwanini kila siku unataka upewe takwimu za Corona na sio malaria?
Lini utakuja kuulizia takwimu za wagonjwa wa Kansa?.
una agenda gani na CORONA?
Si unajua pia kuwa si kila mtu anayekufa kwa kushindwa kupumua kuwa hajafa kwa Corona?

Mwarobaini kwenye hilo si ilikuwa takwimu sahihi za nani kafa na nini?

Kwanini nguvu kubwa kuhakikisha takwimu kuhusiana na corona pekee hazipo? Yote hii haikufikirishi?
 
Anajibu yote.ni wewe na Imani yako tu kwake binafsi Sina Shaka nae
 
Back
Top Bottom