Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ametangaza utaratibu mpya wa ajira za Ualimu unaoelekeza Walimu kufanya Mtihani wa Kuwapima uwezo kabla ya Kuajiriwa, lengo likiwa ni kurudisha hadhi ya taaluma ya ualimu, isitazamwe kuwa chaguo la mwisho baada ya kukosa nyingine

Utaratibu wa ajira hizo kwa sasa unahusisha kutuma maombi katika tovuti maalum ya maombi ya ajira, kisha anayepata nafasi hufanyiwa usaili kisha kupangiwa eneo la kazi.

Kwa mujibu wa Profesa Mkenda, utaratibu huo utaanza kufanyika katika ajira mpya za taaluma hiyo, na hautafuta mchakato wa usaili, akisisitiza utaendelea kama kawaida ili kupata walimu

Amesema, "Wakati wa kutangaza nafasi mpya za ualimu, wakitaka kupata kazi, watafanya mtihani haijalishi tayari umesoma, kwanza itatuondolea matatizo. Kuajiriwa kuwa Mwalimu utafanya mtihani, utaona matokeo, tutaangalia idadi inayohitajika tutachukua waliofaulu tutawaajiri,"

Chanzo: Mwananchi
Wizara ya Afya nayo iige huu utaratibu sio mnaajiri watu wanabaka wagonjwa Wetu.
 
Unanifanyisha usaili kwa mshahara upi wa ualimu?
Huwa nashangaa Sana nikiona hizi comments Huwa naamini utoto Bado upo kichwani!! Na kujifanya mmefanikiwa Sana kinaisha!!! Wakati loooooh!!! Mara nyingi watu ambao hujifanya wanazo pesa Hali Huwa ni kinyume!! Tungekuwa tunaoneshana Mali na akiba humu tungekimbiana!? Jamii forum inatusitiri sana
 
kwa hio Mkenda haamini vyuo vyao vilivyofundisha waalimu?
hata elimu yake inabidi tuwe na wasi wasi nao kama anaanza kuleta figisu tu ili watoto wa maskini wasipate ajira
kiufupiu hii mitihani ni ulaji wao , wanatafuta kila mbinu ya kula pesa ya mlala hoi
 
Haamini vipi? Mbona kada zingine wanafanya Usaili?
 
Back
Top Bottom