Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Pia.Ule mtazamo kuwa taaluma ya ualimu ni chaguo la mwisho baada ya kukosa fursa nyingine unakaribia ukingoni, baada ya Serikali kutangaza utaratibu mpya katika ajira za taaluma hiyo.
Utaratibu huo, kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda utahusisha, ili uajiriwe kuwa mwalimu utapaswa kufanya mtihani wa kupima uwezo wako.
Kwa sasa, ajira ya ualimu inahusisha kutuma maombi katika tovuti maalum ya maombi ya ajira, kisha anayepata nafasi hufanyiwa usaili kisha kupangiwa eneo la kazi.
Mwananchi
-Wasajiliwe na kupewa Leseni kama taaluma zingine( Kabla ya huu mchakato ndio wapimwe kwanza kupitia mitihani)
-Maslahi yao yaboreshwe ili waweze kumudu kuhuisha leseni zao.
Hili la Walimu kupimwa uwezo wao tumelijadili sana humu, naona kilio chetu kinaenda kupata majibu.