Serikali yafuta mapendekezo ya kuzifanyia Marekebisho ya Sheria zinazohusu Umiliki wa Maliasili

Yaani Kiongozi anayepèwa kila kitu anashadadia maliasili zisilindwe dhidi ya wavamizi wa kigeni...!

Hivi huyu nimwenzetu kweli ?
Lengo lake ninini haswa ?

Naomba majibu haraka.
 
Mwambukusi,dr slaa na wazalendo wengine washukuriwe kwa kutetea maliasili za Tanganyika hadi wauza maliasili wameona aibu kubadili sheria ili kurahisisha uuzwaji wa Nchi.
 
Ina impact gani juu ya huu Mkataba
 
Sheria mpya nyingi zimepitishwa bungeni leo, mbali ya kanuni za bunge sheria zilizo rekebishwa ni.

1) Tume ya mipango 2023.
2) Marekebisho idara ya Usalama wa Taifa " TISS Amendments Bill 2023".
3) Laws Amendment Revisions 2023.
4) Marekebisho sheria ya ubia "PPP Amendment Bill 2023"
5) Written Laws Amendment Bill 2023"
6) Matumizi ya fedha 2023 (Apropriation Bill 2023.
7) Finace acts 2023.

Hiyo miswada yote yote imeshapitishwa na Rais kuwa sheria kamili. Na ina majina yake kamili kisheria.
 
Ikiwa ni kweli basi Bunge limeanza kutambua kwa nini TANU na AFRO SHIRAZ walipigania uhuru kutoka kwa wakoloni. Binafsi nilikuwa mwanachama wa TANU kuanzia mwaka 1968, mwanzilishi wa CCM mwaka 1977 na sasa sina chama cha siasa.
 
Hakuna anayetaka kujua sheria zilizopitishwa leo, usikimbie hoja wacha utoto wako bibi.
 
Hatua muhimu sana imefikiwa leo, bunge na serikali wamejua kadri ambavyo wangezidi kuziba masikio ndio kelele za watanganyika zingezidi kuwasumbua masikioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…