Wasalaam ndugu zangu Watanzania!
Bunge leo limekataa kupitisha mabadiliko ya sheria 2 ambazo zilikuwa zinakinzana mkataba tata kati ya Tanzania na Dubai.
Binafsi niliwasilisha maoni yangu kwa kupinga mabadiliko haya ya sheria kwa kamati ya Bunge kupitia email yao.
-
Nimewasilisha maoni yangu kupinga marekebisho ya sheria ya ulinzi wa rasimali za Taifa
Tukumbuke sheria hizi mbili zilitungwa 2017 baada ya migogoro mikubwa ya madini katika awamu ya 5.
Pia Kuna Rufaa inasubiliwa kusikilizwa rasmi na kutolewa uamuzi, ukiliangalia maamuzi ya Bunge leo unapata picha kabisa kuwa Mahakama Rufani itawapa ushindi mkubwa wananchi kwa kusema wazi kuwa Dubai haikuwa na hadhi ya kusaini IGA na Tanzania, pia itasisitiza kuwa mkataba ulikiuka sheria zetu na hivo mkataba huu batili na hivo kuipa nguvu Serikali ya kwenda kuvunja rasmi mkataba huu tata.
Watanzania wameshinda. Watanganyika tumeshinda.