Serikali yatoa kibali kuagiza mchele nje ya nchi
Best move kwa serikali,sasa subirini sasa muwaone wale madalali walio shikilia chakula ambao nia yao kulangua bei watakavyo lalamika.
 
Kama mbona una emotional trauma. So unataka na wafanyabiashara waachiwe huru mafuta ya petrol wauze wanavyotaka, pia na sukari.kama vile una chuki na wasiolima. Kuna utaratibu wa kila kitu katika nchi yenye utawala
emotional trauma.?😂😂 Unaelewa maana yake au ni neno umeliona tu unaanza kuliandika popote ili uonekane unalijua

Wafanyabishara wa mafuta wana profit margin yao ambayo ipo guaranteed na serikali, mafuta yapande au yashuke, ndio maana matuta yalivyopanda bei sana mwaka jana serikali haikuwalazimisha washushe bei ili wananchi wapate nafuu ila ilitoa ruzuku kugharamikia kupanda huko

Ila kwa vyakula ni tofauti, mchele na mahindi kuna kipindi yanashuka sana kiasi kwamba hayamlipi mkulima, serikali haiwapi ruzuku, yakipanda ndio mnataka serikali iingilie ili yashuke?

Leo hii nyie ndio mnaoshangaa kwa nini watu wengi wenye mitaji mikubwa wanawekeza kwenye vituo vya mafuta badala ya kilimo
 
Kwani lile agizo la kuuza nje lilishasitishwa? sikumbuki hilo kufanyika.

Tunaongozwa na serikali kama ya wendawazimu, hawajielewi, mawaziri wa viwanda na kilimo wanakanyagana, huku inaruhusu kuuza nje, wakiambiwa kufanya hivyo scarcity inazidi kuongeza mfumuko wa bei nchini, wanajibu kwa dharau ni zamu ya wakulima kufaidi.

Sasa huku wakulima wakiendelea "kufaidi" nashangaa tena wanaagiza mchele toka nje, hii maana yake nini? wamejua scarcity ipo, kama tulichonacho tunapeleka nje, halafu tunaruhusu cha nje kiingie ndani kwa bei ya juu ile ile, hapa wamesaidia nini kupunguza tatizo la mfumuko wa bei? na quality je?!
 
Asante serikali maana tulikuwa tunauziwa machenga ya vitumbua kwa 3000+ ,...mawe kibao, kijiko cha kwanza cha pili penalty! Yani mpaka unamaliza sahani kidole tumbo kimejaa
 
Ngoja sasa muanze kuletewa ma michele yenye sumu, nakumbuka miaka ya 90s kampuni ya kina Mo Dewji ilileta mchele hatarishi kwa watu, serikali ya mzee Mwinyi ikajikoroga ikaupiga marufuku, ila sakata lake liliua watu wote walioshughulika na huo mchele kuanzia Long room hadi kwa wakemia wa nchi walioshughulikia.

Waliuawa vifo vya utata sana. Kwahio kuruhusu mchele toka nje ni fursa ya kuwaletea wananchi makanjanja na faida kwa wafanyabiashara na wala sio eti njia ya kupunguza makali ya bei ya mchele. Time will tell.
Eenyi kizazi chanyoka msaidiweje mbona rangi zenu hazieleweki?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwa Dar es salaam leo amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais Dkt.Samia “Tunatarajia kuanzia mwisho wa mwezi huu wa pili zao la mchele litapungua bei”

Lengo la Serikali mchele ushuke bei.

======

Serikali yatangaza matazamio kushuka bei ya mchele

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa zao hilo kwa Taifa na pia Serikali imeondoa baadhi ya kodi ili zao hilo liweze kuongezeka kwenye soko.

Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “Tunatarajia kuanzia mwisho mwezi huu wa pili, wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu zao la mchele litapungua bei na Watanzania waweze kufikia zao hilo na kununua katika bei inayohimilika"

Tanzania Web
Sasa wapinzani wananyanganywa hoja, ndio shida ya kukosa ajenda za kudumu, na kudakia matukio, viva Samia
 
Tunapigwa na vitu vizito.
Mchele wetu, mahindi, maharage vimeenda wapi?

Njaa ni kali imefikia watoto wanaiba mandaz huko mbeya mkoa wenye chakula.

Nchi imekuwa ngumu
Ni jukumu la kila mtanzania kuweka akiba ya chakula chake
 
Ngoja sasa muanze kuletewa ma michele yenye sumu, nakumbuka miaka ya 90s kampuni ya kina Mo Dewji ilileta mchele hatarishi kwa watu, serikali ya mzee Mwinyi ikajikoroga ikaupiga marufuku, ila sakata lake liliua watu wote walioshughulika na huo mchele kuanzia Long room hadi kwa wakemia wa nchi walioshughulikia.

Waliuawa vifo vya utata sana. Kwahio kuruhusu mchele toka nje ni fursa ya kuwaletea wananchi makanjanja na faida kwa wafanyabiashara na wala sio eti njia ya kupunguza makali ya bei ya mchele. Time will tell.
Mkuu naomba hii habar vizur
 
Bwasheee anasema anaruhusu chakula kisombwe holela kwenda nje ili wakulima wanufaike wakati kiuhalisia wanaonufaika ni madalali na walanguzi ambao sasa anawapa shavu jingine la kuagiza chakula kilekile walichopeleka nje kukirudisha nchini kuwauzia wakulima wasio na chakula kwa sasa........eti hizo ndo akili za jiniaz.​
 
Back
Top Bottom