Kwani lile agizo la kuuza nje lilishasitishwa? sikumbuki hilo kufanyika.
Tunaongozwa na serikali kama ya wendawazimu, hawajielewi, mawaziri wa viwanda na kilimo wanakanyagana, huku inaruhusu kuuza nje, wakiambiwa kufanya hivyo scarcity inazidi kuongeza mfumuko wa bei nchini, wanajibu kwa dharau ni zamu ya wakulima kufaidi.
Sasa huku wakulima wakiendelea "kufaidi" nashangaa tena wanaagiza mchele toka nje, hii maana yake nini? wamejua scarcity ipo, kama tulichonacho tunapeleka nje, halafu tunaruhusu cha nje kiingie ndani kwa bei ya juu ile ile, hapa wamesaidia nini kupunguza tatizo la mfumuko wa bei? na quality je?!