Serikali yatoa kibali kuagiza mchele nje ya nchi
Hapa serekali ilaumiwe kwani vitabu vyao vya kubalansi chakula vinasemaje!!??
Leo hii Tz ni ya kununua mchele nje kweli!!??
 
Kwa hiyo huku bara tupo kama popo, upande mmoja tunauza nje, upande mwingine tunaagiza toka nje, halafu tunasema tuna serikali!

Tunajiendea zetu tu, kama kundi la wana kondoo.

Free Market Economy.
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwa Dar es salaam leo amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais Dkt.Samia “Tunatarajia kuanzia mwisho wa mwezi huu wa pili zao la mchele litapungua bei”

Lengo la Serikali mchele ushuke bei.

======

Serikali yatangaza matazamio kushuka bei ya mchele

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa zao hilo kwa Taifa na pia Serikali imeondoa baadhi ya kodi ili zao hilo liweze kuongezeka kwenye soko.

Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “Tunatarajia kuanzia mwisho mwezi huu wa pili, wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu zao la mchele litapungua bei na Watanzania waweze kufikia zao hilo na kununua katika bei inayohimilika".
Labda wafanyabiashara washikiwe viboko ndiyo watapunguza bei au watatoboa mawe ya mizani ionekane wamepunguza bei.
 
Hii nchi Bado sana,sasa tulikuwa na nafaka nyingi,bei ilikuwa poa,mkazuia wakulima wasiuze nje,baadae mksruhusu,nafaka ikauzwa nyingi nje,sasa mahitaji yakawa makubwa,bei ikapanda,sasa hv nafska imekuwa haba,mmeruhusu tuagize nje!!
Swali langu kwenu nyie kenge maji,kwani haiwezekani tulime wenyewe,mkulima apate faida,na mnunuzi apate unafuu wa kununua?
Mchele uwe buku moja,mkulima apate faida hata ya 300 kwa kila kilo,kwanini mnatuhusu nafska iuzwe nje mpaka bei inapanda juu ndani ya nchi
wewe nimpuuzi mmoja unaewaza ndani ya box

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
VIBALI vya kuingiza au kusafirisha ,mazao ya chakula ndani na nje vinatolewa na Wizara ya Kilimo, iweje leo tangazo la kuagiza mchele tani elf 90 litolewe na Waziri wa Uwekezaji na Viwanda, Dk. Ashatu Kijaji?

Kwanini Waziri mwenye dhamana ameshindwa kuita Press na kutangaza uamuzi huo?

Wajuzi wa mambo hebu tulijadilini hili lina maana gani?
 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwa Dar es salaam leo amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais Dkt.Samia “Tunatarajia kuanzia mwisho wa mwezi huu wa pili zao la mchele litapungua bei”

Lengo la Serikali mchele ushuke bei.

======

Serikali yatangaza matazamio kushuka bei ya mchele

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa zao hilo kwa Taifa na pia Serikali imeondoa baadhi ya kodi ili zao hilo liweze kuongezeka kwenye soko.

Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo Dar es salaam leo ambapo amenukuliwa akisema “Tunatarajia kuanzia mwisho mwezi huu wa pili, wiki ya kwanza ya mwezi wa tatu zao la mchele litapungua bei na Watanzania waweze kufikia zao hilo na kununua katika bei inayohimilika".
tatizo badala ya kuleta mchele wataleta makapi(kitumbo)
 
Bado hio ni aibu kuagiza chakula kutoka nje.

Pia yanyesha kiwango kikubwa cha tamaa ya kupata faida kubwa.

Tatu, kunaonyesha jinsi waagizaji walivyo na nguvu kubwa ya ushawishi.

Na nne kutowajali wakulima ambao ndo wazalishaji kule mashambani.
Tatizo ni Bashe kuruhusu watu wauze.

Watu walifurahia,
Walaji wakalia

Leo wanataka agiza wale wale wanaolia kila siku kuwa mchele bei ghali, hao hao leo wanalalamika kuwa serikali imekosea.
 
Haikupaswa kuagiza mchele nje,, italeta kelele kwa wazlishaji
 
Wanaagiza kwa ndege au meli?,, Kama ni kwa meli, huo mchele kama alivyoongea Bashe,, utakuja kuua bei ya mchele wa wakulima, mwezi may
Huu mchele tayari uko njiani ni wiki ijayo tu unakuja na bei yake kilo itakuwa 1700-2400
 
Nipo Holili hapa nashangaa ati mchele unatoka Kenya unaingia Tanzani na ni mwezi uliopita tu mchele ulikua unatoka huku unaenda kule, hivi Kenya wanakilimo gani cha mpunga?
Wanaleta walionunua nje, Vietnam, India, China, Brazil
 
VIBALI vya kuingiza au kusafirisha ,mazao ya chakula ndani na nje vinatolewa na Wizara ya Kilimo, iweje leo tangazo la kuagiza mchele tani elf 90 litolewe na Waziri wa Uwekezaji na Viwanda, Dk. Ashatu Kijaji?

Kwanini Waziri mwenye dhamana ameshindwa kuita Press na kutangaza uamuzi huo?

Wajuzi wa mambo hebu tulijadilini hili lina maana gani?
mkiambiwa mkasome ehhh mbona ambao hawajasoma wana hela zaidi. Haya sasa elimu ndogo tu ya uraia km hiyo unashindwa kuelewa. Bashe ni waziri wa nini. Uliambiwa tunaenda kulima mashamba nje ya nchi.
 
Ni mtizamo hasi tu mbona Zanzibar karibu 90% ya mchele wanaotumia miaka yote unatoka nje?!!ndio maana kule unakuta mchele siku zote unachezea 1200-.1500/kilo .labda mwaka huu tu.Kule mchele wa bara ni anasa!!wao kitu mapembe.
Naona kwa sasa kg 50 ni 92,000 ambayo ni kama 1800
 
Hilo ni jambo jema.
Sasa wajipange kwenye suala la kusimamia mara hizo tani za mchele zitakapo wasili.

Nashauri;
Vyombo vyote visimamie ili wafanyabiashara na wenye tamaa wasije kuhujumu lengo lililo kusudiwa.
Mzigo utakuwa mwingi sana na watataka wauuze kwa wingi
 
Yaani pamoja ukubwa wa ardhi yenye rutuba tuliyonayo, mito ya maji tiririka usiku na mchana mapori ya akiba kibao hivi 2023 hii inafikia hatua tunaangiza msosi nje? kweli?
 
Back
Top Bottom