Serikali yatoa kibali kuagiza mchele nje ya nchi
Labda wafanyabiashara washikiwe viboko ndiyo watapunguza bei au watatoboa mawe ya mizani ionekane wamepunguza bei.
Mchele ukishaingia mwingi sokoni bei inashuka bila kuambiwa labda waununue waende uficha
 
Yaani pamoja ukubwa wa ardhi yenye rutuba tuliyonayo, mito ya maji tiririka usiku na mchana mapori ya akiba kibao hivi 2023 hii inafikia hatua tunaangiza msosi nje? kweli?
Kalime
 
Wanaleta walionunua nje, Vietnam, India, China, Brazil
Wafanya biashara wa kaskazini wanachokifanya ni kuuchanga na wa huku nyumbani maana ukipikwa wenyewe hauna ladha au ndio maana wachina kule kwao wanakula kwa vijiti!
 
mkiambiwa mkasome ehhh mbona ambao hawajasoma wana hela zaidi. Haya sasa elimu ndogo tu ya uraia km hiyo unashindwa kuelewa. Bashe ni waziri wa nini. Uliambiwa tunaenda kulima mashamba nje ya nchi.
 
Serikali ni ya ajabu sana, unatoa vibali vya kuuza mchele nje ya nchi, na baadae unatoa vibali vya kwenda kuunua huo mchele nje ya nchi, kwanini hiyo pesa na bei inayonunulia nje wasipewe wakulima wa ndani. Na uhakika mchele kwa wakulima upo wa kutosha, tengeneza sera nzuri kwa hao wafanyabiashara wanaotaka vibali kwenda kununua kwa wakulima ili mchele uingie sokoni kwa wingi , supply ikiwa kubwa, demand itashuka tu hivyo bei itashuka pia.
 
Sasa nyie mnaolalamika mlitaka serikali ifanyeje kupunguza mfumuko wa bei?
 
Hii nchi Bado sana,sasa tulikuwa na nafaka nyingi,bei ilikuwa poa,mkazuia wakulima wasiuze nje,baadae mksruhusu,nafaka ikauzwa nyingi nje,sasa mahitaji yakawa makubwa,bei ikapanda,sasa hv nafska imekuwa haba,mmeruhusu tuagize nje!!
Swali langu kwenu nyie kenge maji,kwani haiwezekani tulime wenyewe,mkulima apate faida,na mnunuzi apate unafuu wa kununua?
Mchele uwe buku moja,mkulima apate faida hata ya 300 kwa kila kilo,kwanini mnatuhusu nafska iuzwe nje mpaka bei inapanda juu ndani ya nchi
Daah mi sijasoma uchumi ila hiki ulichoandika hapa ni kichekesho
 
Hii nchi Bado sana,sasa tulikuwa na nafaka nyingi,bei ilikuwa poa,mkazuia wakulima wasiuze nje,baadae mksruhusu,nafaka ikauzwa nyingi nje,sasa mahitaji yakawa makubwa,bei ikapanda,sasa hv nafska imekuwa haba,mmeruhusu tuagize nje!!
Swali langu kwenu nyie kenge maji,kwani haiwezekani tulime wenyewe,mkulima apate faida,na mnunuzi apate unafuu wa kununua?
Mchele uwe buku moja,mkulima apate faida hata ya 300 kwa kila kilo,kwanini mnatuhusu nafska iuzwe nje mpaka bei inapanda juu ndani ya nchi
Ukitaka bei poa nenda kalime.
 
vibali vinatolewa na wizara ya kilimo hata mimi nilishangaa sana kuona waziri wa uwekezaji ndio anatangaza kuruhusu mchele kuingia nchini
 
Hivi waziri wa Kilimo hastahili lawama katika hili?
 
Back
Top Bottom