much know
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 11,461
- 17,183
Ndio maana ya solo huriaMchele wa nje hauliki kwa mapishi ya tz,labda kwa ajili ya vitumbua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio maana ya solo huriaMchele wa nje hauliki kwa mapishi ya tz,labda kwa ajili ya vitumbua
Anavyotoaga macho unafikiri anajiandaa kulamba ndimuBwasheee anasema anaruhusu chakula kisombwe holela kwenda nje ili wakulima wanufaike wakati kiuhalisia wanaonufaika ni madalali na walanguzi ambao sasa anawapa shavu jingine la kuagiza chakula kilekile walichopeleka nje kukirudisha nchini kuwauzia wakulima wasio na chakula kwa sasa........eti hizo ndo akili za jiniaz.
Jamaa anavyotoaga macho sijui huwa anatumia akili ganiSiku zote njia ya mwongo ni fupi tulimwambia Bashe nchi haina chakula stop export ya mazao kwa muda mpaka hali ikawe vizuri, tukapewa majibu kwamba hatumsaidii mkulima shmbani. Leo tena tumeamua kufanya importation ni nini tunafanya??
Viongozi wetu wanatambua wanachofanya??
Wamegundua mkulima mwenyewe hainulikiSi walisema wanamwinua mkulima?
huyu mtu hajitambui,food security ni suala nyeti sana,yule waziri mjinga anayesema wakulima wanauza nje kwa bei nzuri aje atuambie kwanini sasa hivi tununue nje wakati chakula kipo ndani?,Kama mbona una emotional trauma. So unataka na wafanyabiashara waachiwe huru mafuta ya petrol wauze wanavyotaka, pia na sukari.kama vile una chuki na wasiolima. Kuna utaratibu wa kila kitu katika nchi yenye utawala
Fear of unknownNgoja sasa muanze kuletewa ma mchele yenye sumu, nakumbuka miaka ya 90s kampuni ya kina Mo Dewji ilileta mchele hatarishi kwa watu, serikali ya mzee Mwinyi ikajikoroga ikaupiga marufuku, lile sakata lake liliua watu wote walioshughulika na huo mchele kuanzia Long room hadi kwa wakemia wa nchi walioshughulikia.
Waliuawa vifo vya utata sana. Kwahio kuruhusu mchele toka nje ni fursa ya kuwaletea wananchi makanjanja na faida kwa wafanyabiashara na wala sio eti njia ya kupunguza makali ya bei ya mchele. Time will tell.
Ni kitu gani hamkielewi hapa?Hizi ndio akili za mwafrika, tena mtanzania. Mchele umeuzwa nje leo tunaenda kununua mchele nje.
Acha uje tukishindwa kuupika kwa mapishi yetu tutakula kwenye vitumbua maana hata vitumbua bado ni mapishi yetuMchele wa nje hauliki kwa mapishi ya tz,labda kwa ajili ya vitumbua
Muda ukifika mtavijua,hata sisi watu wa Mjini mwanzo hatukuvijua,ila sasa tunavijua! Ukija Mjini nileetee Kuku moja la Kienyeji nitafune pls ndg wa shambani!!mnakula nyie mjini huku shambani hatuvijui
Hizi ndio akili za mwafrika, tena mtanzania. Mchele umeuzwa nje leo tunaenda kununua mchele nje.
lakini tujue kabisa huo (UBWECHE)sio kama huu tuliouzoea wa kwetu hata bila mboga tu unakula!!ule bnana ni kama ugali bila mboga ya maana huuliiii!!!hauna ladha!!lakini potelea mbali uje tu,kwani ni hatari yaani familia zimerudi kwenye ile miaka ya 90 ya kula wali ni anasa!!!Mzigo utakuwa mwingi sana na watataka wauuze kwa wingi
Mkuu sio kweli kwa sasa nchini hakuna mchele wa kutosha kabisa!!yaani huko mikoani maghara mengi yako tupu kabisa!!kwani mavuno ya msimu 2021/22 yalikuwa ni madogo sana,hivyo kupelekea bei ya mchele kupanda toka mwezi sita hivyo wakulima wengi walianza kuuza mazao yao muda huo.Kwa taarifa yako hadi sasa kongo mchele hauendi kutokana na ugumu wa kuupata hapa nchini,wengi waliokuwa wanapeleka ZAMBIA,DRC,BURUNDI NA RWANDA.wameshindwa kupeleka kutokana na upatikanaji wake na bei ziko juu sana.Serikali ni ya ajabu sana, unatoa vibali vya kuuza mchele nje ya nchi, na baadae unatoa vibali vya kwenda kuunua huo mchele nje ya nchi, kwanini hiyo pesa na bei inayonunulia nje wasipewe wakulima wa ndani. Na uhakika mchele kwa wakulima upo wa kutosha, tengeneza sera nzuri kwa hao wafanyabiashara wanaotaka vibali kwenda kununua kwa wakulima ili mchele uingie sokoni kwa wingi , supply ikiwa kubwa, demand itashuka tu hivyo bei itashuka pia.
Kwa kilimo cha nchi hii,mito,maziwa havijawahi kuwa msaada kwetu tofauti na mvua tu.Kuyatoa maji kwenye hivyo vyanzo na kuyatumia kwenye kilimo ni inshu nyingine kabisa.Tutumie akili zetu kutatua tatizo la chakula na si kufikiria kuagiza tu kutoka nje kwamba ndo last resort.
Nguvu kazi ipo, ardhi yenye rutuba ipo na ya kutosha, maji ya mito, vijito na vyanzo vingine pamoja na maziwa yapo, mvua za kutosha zipo.
Nchi yetu haina tatizo la ukame ni nchi safi kabisa kwa kilimo cha mazao yote khasa ya chakula.
Unapenda ubwabwa eehAfadhali waruhusiwe bei inaweza kushuka tukaweza kula Basmati siku moja moja.