Serikali yatoa kibali kuagiza mchele nje ya nchi
Mchele wetu, mahindi, maharage vimeenda wapi?

Njaa ni kali
Mchele wenu? Hahaha.

Hii nchi hii ujamaa umetuharibu sana, huko tunapoelekea hope watoto watakuwa na akili mbadala ya kuelewa mfumo wa dunia na kwenda sawa na teknolojia otherwise watatawaliwa kisasa kuliko sisi au mababu zetu enzi za ukoloni.
 
Ngoja sasa muanze kuletewa ma mchele yenye sumu, nakumbuka miaka ya 90s kampuni ya kina Mo Dewji ilileta mchele hatarishi kwa watu, serikali ya mzee Mwinyi ikajikoroga ikaupiga marufuku, lile sakata lake liliua watu wote walioshughulika na huo mchele kuanzia Long room hadi kwa wakemia wa nchi walioshughulikia.

Waliuawa vifo vya utata sana. Kwahio kuruhusu mchele toka nje ni fursa ya kuwaletea wananchi makanjanja na faida kwa wafanyabiashara na wala sio eti njia ya kupunguza makali ya bei ya mchele. Time will tell.
Acha porojo za vibanda vya kahawa
 
Nimewasiliana na ndugu zangu kutoka China, nimeona endapo Serikali itatupatia clearance tunaweza kumletea mraji wa mwisho mchele grade one kwa thamani ya Pesa isiyozidi 2000. Naomba tutumie mfumo kuruhusu Biashara uria.

Pia sukari kutoka Brazil ni bei rahisi sana hivyo hakuna haja Tena ya kuumizana mbona Zanzibar wanatumia hiyo sukari ya bei nafuu na wanaishi vizuri tu.
 
Aiseee watoe tu vibali kwakweli hali si nzuri mtaani. Kuna familia nimekwenda juzi kati nimekuta wananunua vitu nusu nusu dukani nikajiskia vibaya sana.

Leo mtu kununua chakula cha jumla imekuwa ni mtihani. Imagine, mchele 3,500 kilo, Maharage 4,000, ina maana kwa milo miwili kwa siku familia ambayo inatumia zaidi ya kilo mbili inakuwa katika hali mbaya sana kumudu chakula tu tukiacha expenses nyingine.

Hawa mabwanyenye wapo busy kukimbizana na Ma land cruiser humo barabarani wakichoma hela zetu za kodi badala ya kudeal na hii emergency. Kama yule Mwigulu me namuombea dua mbaya kila uchao maana si kwa uhaini anaotufanyia raia tusio na hatia.

Inapofikia hatua raia wanahangaika na chakula kwasababu za kipumbavu nje ya ukame au mafuriko au tukio la kiasili ina maanisha serikali iliyopo kwenye uongozi ina uwezo mdogo sana kusimamia maisha ya wananchi.

Ni sawa na baba una mali ila watoto wanashinda na kulala njaa, wewe ni irresponsible father kupita maelezo na hauna akili sawa sawa.

Hii hali ni jambo la dharula na pale bungeni wanatakiwa kujadili kushusha bei ya mazao haraka sana na kuondoa huu mfumuko wa bei unaowatesa raia kushindwa kuishi vizuri na akili ziweze kutafakari maendeleo.

Inapofikia hatua serikali inacheka cheka na watu wanaficha chakula kwa sababu za kipuuzi kama kufanya bei zipande bila kuchukua hatua ni wazi wanashiriki dhambi ya uhujumu wa uchumi.

Kwann isitoe ruzuku tuagize sukari, mchele na mafuta kutoka nje kwa kiwango kikubwa ili raia wapate ahuweni ya haraka na kuwashikisha adabu hawa wapumbavu wachache wanaocheza na bei za mazao.
 
Vibali vitolewe,

Bt ubora uzingatiwe, Mchele wa PLASTIC usiingie nchini tafadhali.

NB: Utumishi ktk KAZI ofisi za Umma ni KAZI takatifu kama kuhudumia madhabahu HEKALUNI.

Tangulizeni maslah ya umma mbele mtabarikiwa.

Aaamen
 
Tunapigwa na vitu vizito.
Mchele wetu, mahindi, maharage vimeenda wapi?

Njaa ni kali imefikia watoto wanaiba mandaz huko mbeya mkoa wenye chakula.

Nchi imekuwa ngumu
Aliye saidia kutufikisha hapo ni Waziri Bashe. Watu tulipiga kelele sana humu tangu mwaka jana kuwa chakula kisivushwe mipaka kiholela. Yeye na ma- boss wake waka tuona pro- Magu. Wa kulima wetu wengi ni maskini sana. Hawezi kumkatalia Mkenya anapokuja na sh million moja ana mwachia heka 2 akavune mwenyewe, atakachopata halali yake. Kesho yake mkulima ana a za kuhemea chakula, tumewaona sana huku. Samia awe makini na baadhi ya mawaziri wake kwani kuvaa capero (kofia) yenye herufi 'SSH' si uzalendo tosha.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Fear of unknown
It's not fear man, maana mchele mwingi unatoka Pakistan, India na Far East huko i.e Thailand. Sasa uwaga top quality ya vitu vingi inapelekwa ulaya na US/Canada ila yale makapi ndio yanakwenda Africa. Hata nguo, magari ndio hivyo hivyo kwahio tutegemee bongo wakiagiza mchele watauziwa hayo makapi ambayo mengi yamepita muda yenye sumu-tuombe yasitokee hayo. Hilo suala la akina Mo Dewji la mchele wenye sumu hukuwahi kulisikia mbona lilikuwaga front pages kwenye magazeti ya bongo?? Na wote waliohusika walidedishwa ki utata nalo hukusikia?? Labda ulikua kiunoni kwa m sure bado kuzaliwa, maana humu JF siku hizi kuna vitoto vingi sana vya dotcom 🤣 🤣 🤣 🤣 .
 
Yani tumeuza nje mchele wetu mtamu, sasa tunaagiza mchele kitumbo kama sio mchele wa mapembe unaopatikana Zanzibar. Lakini wakulima walinufaika, waliuza sana nafaka nje.

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Hakuna mkulima wa chini aliyenufaika jamani acheni hizi ngonjera sema dalali ndo hunufaika zaidi ila sio mkulima.
 
Back
Top Bottom