Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Mwenye mpira ana mamlaka kumtoa anaepiga sana mashuti
Kuna wale walikuwa na mtindo wa kukanyaga mpira mpaka duara linapotea, dah nilikuaga nabeba mpira wangu kwa leo au kama bado mapema basi jamaa anaambiwa atoke
 
Kichwa cha mwendawazimu kilianzia hapo.
 
Hapo umenena kweli mkuu,, kwa iyo suluhisho watoto wameona wajikalie nyumbani tu kuangalia TV. Hii ni changamoto kwa serikali yetu, inatakiwa hili ilifanyie kazi ili watoto wapate muda wa kucheza.
Tulicheza hata barabarani
 
Hapo umenena kweli mkuu,, kwa iyo suluhisho watoto wameona wajikalie nyumbani tu kuangalia TV. Hii ni changamoto kwa serikali yetu, inatakiwa hili ilifanyie kazi ili watoto wapate muda wa kucheza.
Kabisaaa lkn sio rahisi kutatua hili
 
Kuna wakati sisi kukiwa na mbalamwezi tulikuwa tuna cheza usiku, hapo sio kung'oana kucha sasa!!!! Kurubasi zilikuwa zinaruhusiwa kuvaliwa
 
Mwenye mpira ana haki ya kucheza na viatu wengine wote peku peku labda rafiki zake wa karibu ambao wako upande wake. Anayefunga magoli dhidi ya timu ya mwenye mpira mwenye mpira anaweza kuamua kumtoa nje ili kuipa nafasi timu yake ishinde.

 
Sijui watoto wetu wamepumbazwa na ma-TV? Yaani wanacheza kwa kusuasua sana, wakati enzi zile tulikuwa tunatoka mtaa kwenda kushindana na mtaa mwingine au kijiji kimoja na kingine! Mkitoka suluhu zinapigwa ngumi angalau timu moja ionekane bingwa!!
Ukweli ni kwamba watoto wa kizazi hiki... hawafahidi kitu kabisa... utoto wetu ulikuwa raha sana... mitoto ya sasa hiv..bkutwa tv.. simu
 
Ha ha ha haaaaaaa, mkuu kweli we kijana wa zamani
 
HAUKUNA KUCHEZA NA VIATU MANA UTAUMIZA WENGINE.....
KILA MCHEZAJI NI KOCHA.....
HAKUNA IDADI YA WACHEZAJI HATA WATATU MNAUNDA TIMU...
HAKUNA MAPUMZIKO...
TIMU A WATAVUA MASHAT TIM B WATABAK NA MASHAT..
Mbambe hanyimwi no.
Hakuna no maalum beki a naweza kuwa mshambuliaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…