Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa ule ni mpira au vikatuni,Wanacheza mpira kwa play stiations, kwa Tv au smartphone.
Kuna wale walikuwa na mtindo wa kukanyaga mpira mpaka duara linapotea, dah nilikuaga nabeba mpira wangu kwa leo au kama bado mapema basi jamaa anaambiwa atokeMwenye mpira ana mamlaka kumtoa anaepiga sana mashuti
Kichwa cha mwendawazimu kilianzia hapo.SHERIA 15 ZA MPIRA ZA KIPINDI CHA UTOTONI
1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza Mnaingia Wawili.
2.Mwenye Mpira Hatolewi Hata Akicheza Vibaya.
3.Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama Penati Imetokea Na Baada Ya Penati Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.
4.Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi Namba Hata Siku Moja.
5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.
6.Mwenye Mpira Ataamua Nani Asicheze.
7.Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.
8.Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.
9. Hakuna Free Kick,refa Wala Offside.
10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote Uwanjani.
11.Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndo Mwende Kucheza.
12.Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.
13.Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.
14. Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Ni Kufata Mipira Ikitoka.
15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi Ndo Inakuwa Imeisha
Enzi hizo kumiliki mia tano siyo mchezo. Donation sh 20 au 50 inausika.Mmenikumbusha ule mpira unaoitwa nyuzi mbanano ulikuwa unauzwa pale kinondoni mosko tsh 500 tu! View attachment 447836
Tulicheza hata barabaraniHapo umenena kweli mkuu,, kwa iyo suluhisho watoto wameona wajikalie nyumbani tu kuangalia TV. Hii ni changamoto kwa serikali yetu, inatakiwa hili ilifanyie kazi ili watoto wapate muda wa kucheza.
Kabisaaa lkn sio rahisi kutatua hiliHapo umenena kweli mkuu,, kwa iyo suluhisho watoto wameona wajikalie nyumbani tu kuangalia TV. Hii ni changamoto kwa serikali yetu, inatakiwa hili ilifanyie kazi ili watoto wapate muda wa kucheza.
Kuna wakati sisi kukiwa na mbalamwezi tulikuwa tuna cheza usiku, hapo sio kung'oana kucha sasa!!!! Kurubasi zilikuwa zinaruhusiwa kuvaliwaSisi tulikuwa na sheria chache.
1.faulo pekee hata penati ni kushika
2.mpira ukitoka anaewahi ndio anarusha
3.hamna kona
4.hamna half time
5.giza ndio linaamua mpira uishe
6.mwenye mpira lazima acheze
7.mnyonge ndio kipa
8.hamna jezi,mwendo ni kuvaa au kuvua shati
9.hamna kucheza na viatu
10.anaejua yaani fundi lazima acheze mara nyingi huwa wanaringa sana
huo mpira tulikuwa tunafuma wenyewe enzi hizo tuliuita kisambiMmenikumbusha ule mpira unaoitwa nyuzi mbanano ulikuwa unauzwa pale kinondoni mosko tsh 500 tu! View attachment 447836
SHERIA 15 ZA MPIRA ZA KIPINDI CHA UTOTONI
1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza Mnaingia Wawili.
2.Mwenye Mpira Hatolewi Hata Akicheza Vibaya.
3.Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama Penati Imetokea Na Baada Ya Penati Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.
4.Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi Namba Hata Siku Moja.
5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.
6.Mwenye Mpira Ataamua Nani Asicheze.
7.Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.
8.Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.
9. Hakuna Free Kick,refa Wala Offside.
10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote Uwanjani.
11.Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndo Mwende Kucheza.
12.Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.
13.Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.
14. Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Ni Kufata Mipira Ikitoka.
15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi Ndo Inakuwa Imeisha
Ukweli ni kwamba watoto wa kizazi hiki... hawafahidi kitu kabisa... utoto wetu ulikuwa raha sana... mitoto ya sasa hiv..bkutwa tv.. simuSijui watoto wetu wamepumbazwa na ma-TV? Yaani wanacheza kwa kusuasua sana, wakati enzi zile tulikuwa tunatoka mtaa kwenda kushindana na mtaa mwingine au kijiji kimoja na kingine! Mkitoka suluhu zinapigwa ngumi angalau timu moja ionekane bingwa!!
kisambi kilugha au kiswahil?huo mpira tulikuwa tunafuma wenyewe enzi hizo tuliuita kisambi
kihehe hicho mkuukisambi kilugha au kiswahil?