Shule zaandikiwa Barua kutoa takwimu za Idadi ya wanafunzi wa Kiislamu shuleni


Mbona hakuna shida mkuu!

  • Je kama wanataka wanunue vitabu vya elimu ya dini!?
  • Au ni research, wanaevaluate idadi ya waislamu waliopo shule.
 
Barua ipo Sawa kabisa Ila itategemea msomaji anaitafsiri vipi hiyo barua.
Kama ni hivyo huo ni uandishi mbaya wa barua. Barua inapaswa kujieleza yenyewe isiache nafasi ya mtu kuielewa tofauti na mwingine, vinginevyo utekelezaji unaweza kuwa tofauti
 
Kuna watu waajabu sana,mtu anasema hilo halina shida kweli?lazima watoe sababu hata kama jambo ni dogo kiasi gani,vitu vidogo vidogo vikiungana vinakuwa bomu kabisa,shule ni moja ya sehemu tunaungana na wamoja na sio sensa ya kidini,kama wamechinja ngamia wao wapeleke tu hapo hapo wote wale,kama ni juzuu wawasubiri misikitini na madrasa wawape.
 
Hii ilikuwa ni kweli na baada ya kelele wameandika barua nyingine kusitisha ruhusa waliyotoa
 
Mawazo huru!

Kama linafanyika wakati huu wa karibia na uchaguzi!ni dhahiri shahiri kura za mchongo zinatafutwa Kwa vyovyote vile!!

Hata Kwa hongo na ahadi za kazi,ufadhili wa masomo na n.k!

Tunaenda kugawanyika kiimani kabisa kuelekea uchaguzi mkuu!!yaani waarabu vs wazungu dhidi ya rasilimali zetu!!

Nilifundishwa utotoni muislamu ndugu yake ni muislam!
 
Mengine tuwe positive. Nadhani kwanza ni shirika binafsi limeomba kibali. Mambo mengine tunayakuza bila sababu.
Kama ni shirika binafsi wakafanye wao sensa kwanini wahusishwe walimu?
 
Huwa wanaanza hivi hivi.. awamu zingine mambo haya hayakuepo
ni movement ya udini isiyo na afya kwa taifa lisiloongozwa kwa misingi ya dini. Siku hizi hakuna anayekemea udini kama zamani. Udini unashadidiwa kwa nguvu mpaka kwenye taasisi za umma. Wakijiona wako wengi ataibuka mwehu wa kidini kuanzisha hoja bungeni kuwa lianzishwe jambo fulani kwa waumini wa dini hiyo kwa kuwa ni wengi na wana haki ya kufanya mambo ya dini yao kwa uhuru
 
Mengine tuwe positive. Nadhani kwanza ni shirika binafsi limeomba kibali. Mambo mengine tunayakuza bila sababu.
Kwanini udhani? Hilo shirika limeomba kibali cha kuhesabu waislam kwa lengo gani? BTW hicho kibali baada ya kelele kelele hizi kimefutwa, kwanini? If nothing fishy is going on nyuma ya pazia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…