Ukiamua kutotaka kunielewa ni ruksa tu Mkuu.
Ila hoja zangu zina msingi wa kihistoria na ushahidi wa kisheria ambao uko wazi, dhahiri na hata mamlaka za kanisa zinakiri kuhusu uwepo wake. Katika miaka yake 2000 kanisa katoliki limetenda madhambi mengi sana kwa jamii ambazo sizo za wakatoliki. Limefanya mauaji, utekaji na kutoa miongozi mingi ya kikuhani ambayo imelichafua kanisa mpaka leo hii kulazimisha hadi Mapapa waombe msamaha mbele za dunia nzima.
Hata Yesu Kristo aliuwawa na viongozi wa dini ya Kiyahudi chini ya usimamizi wa dola ya Kirumi..
Hili la dini (dini zote) kushiriki uovu ikiwemo mauaji na ufisadi, haliko kwa Wakatoliki tu. Ni dini zote. Wakatoliki wanakuwa front page kwa kuwa, ndiyo mama na baba wa asili ya dini ya u-kristo. Madhehebu mengine yote yametoka huko...
Na ndo kusema kuwa mizizi na mifumo ya Kanisa Katoliki ni very deeply rooted underneath na ni imara kwelikweli. Kuing'oa mizizi hii ni kazi kubwa sana na pengine haiwezekani. Hata mifumo mingi ya kiserikali duniani iko connected na mifumo ya kanisa hili...
Na kumbuka dini si utakatifu, sio Mungu. Ni mfumo tu wa serikali za kibinadamu wa kutambua makundi ya kumwabudu huyo Mungu na kuyapa haki ya kisheria...
Kama ulikuwa hujui ndugu
MALCOM LUMUMBA ni kuwa hata hizi dini za kilokole (imani kali), kuna uchafu na uovu mkubwa huendelea humo ndani
MASWALI YA MSINGI HAPA NI HAYA:
MOSI: Je, ni kweli kanisa katoliki halikuwahi kutenda mabaya dhidi ya watu ???
Ni dini ya Ukristo kwa ujumla (si kanisa Katoliki pekee).
Jibu ni kuwa limetenda sana. Nimesema hapo juu, hata Yesu Kristo na mitume wengine kina Petro, Yohana nk na manabii waliuwawa na mifumo dhalimu ya kidini...
THE BIG FACT NI KUWA: Roman Catholic ni kokoro kubwa lililobeba watu wa kila aina wabaya na wazuri. Bahati mbaya ni pale kanisa linapopata kiongozi mkuu mbaya. Hapo tegemea kanisa kushiriki kwenye mambo mabaya kwa mwavuli wa kanisa. Hii ni sawa na serikali tu. Yaweza kupata kiongozi mzuri au mbaya kabisa na serikali yote kuonekana hovyo kama ilivyo sasa...
PILI: Je, ni kweli kanisa katoliki halikuwahi kuunga mkono vitendo dhalimu vya watawala wakatoliki ambao walinyanyasa watu ???
Huwa linaunga. Yaweza kuwa kwa hiari au kwa bahati mbaya na kutojua..
Yesu Kristo aliuwawa na wanadini wa Kiyahudi chini ya utawala wa Kirumi kwa ujinga wa kutojua..
TATU: Je, ni sahihi kusema kanisa katoliki halina uhalali wowote kukemea maovu kwasababu ya vitendo hivi vya kihistoria ???
No, si halali. Mwanadamu (ambaye ndiye msingi wa dini) ni volatile. Ndiyo maana kuna toba. Ukitubu hubadili jina, unabadili mwenendo na tabia..
Inawezekana wakati fulani ktk kipindi cha uongozi fulani kanisa lilifanya makosa kama haya. Lakini linapogundua na kujirudi, Mungu husamehe. Umetoa mifano hiyo ktk andiko lako hapo juu...
NNE: Je, ni sahihi kusema kanisa katoliki lote ni taasisi ovu kisa matendo ya viongozi wake wachache tu ndani ya Kanisa ??? (Hapa zingatia muktadha wa Rwanda 1994)
Sio sahihi. Soma hoja hiyo hapo juu👆🏻
TANO: Je, ni sahihi kusema kanisa katoliki linafanya mabaya tu ilhali tunakataa kusema mazuri yake pia ambayo lilifanya kama kusaidia harakati za ukombozi barani Afria na America kwa kusomesha maelfu ya wasomi ???
Sio sahihi. Soma majibu yangu ya hoja yako ya 3...
SITA: Je, Kanisa Katoliki linampinga Samia kwasababu ya Uislamu wake tu ???
Sio kweli.
Ni kwa sababu hafai kuwa Rais au kiongozi mkuu wa nchi hii. Uislamu wake haujawahi kuhusishwa na kupingwa au kukosolewa kwake. Ni insecurity yake tu inamsumbua kwa sbb ya udhaifu wake...
Anajificha kwenye kichaka cha "KWA SABABU NI MWISLAMU" ni kuficha au watu wasione udhaifu au mapungufu yake...
SABA: Je, Kanisa Katoliki halijawahi kuwapinga viongozi wa Kikristo ???
Limewahi katika awamu zote, kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Mahufuli. Tena wakati wa Magufuli vita yake na kanisa lake ilikuwa kubwa mno kwa sbb hakupenda kanisa likosoe sera na matendo yake mabaya..
Magufuli Mkatoliki, alifikia hatua kuhoji uraia wa baadhi ya maaskofu wakristo mfano Niwemugizi, Zachary Kakobe nk walikiona cha moto toka kwa mkristo mwenzao mkatoliki ili mradi anaitwa "Rais.."
NANE: Je, uovu unapofanyika dhidi ya raia, ni sahihi Kanisa Katoliki kunyamaza na kufumba macho kuwafurahisha watawala ilhali lina uzoefu wa miaka zaidi ya 2000 ya kuona nini huwa madhara ya kutokemea uovu ???
Sio sahihi hata kidogo..
Kanisa kawaida ni chombo cha Mungu mwenyewe kueneza na kutekelezea agenda zake hapa kwa watu wake. Agenda ya maadili mema, upendo, kuthamini uhai wa mwanadamu, nk
Kuikemea serikali inapokwenda kinyume na agenda za Mungu kwa watu wake, ni kufanya au kutenda wajibu wa ki - Mungu. Yesu Kristo aliuwawa kwa sbb hii. Alikuwa kinyume na viongozi wa serikali na wa dini waliokuwa watenda kinyume na agenda za Mungu. Kuona hivyo, kwa sababu wao walikuwa na hela, bunduki na jeshi wakamshughulikia mpaka kumuua kifo kitakatifu kikawa ukombozi wa dunia yote na vilivyomo tukiwemo sisi binadamu...
SABA: Je, ni kweli kwamba hapa Tanzania viongozi wa Kanisa Katoliki hawajawahi kufanya makosa na kutetewa na watu kwasababu tu ni viongozi wa kanisa ??? (Unakumbuka sakata la fedha za TEGETA ESCROW, MKOMBOZI BANK, RUGEMALILA, KADINALI PENGO na FATHER KILAINI ???)
Wengi wamefanya makosa, wanafanya na wataendelea kufanya....
Mtu kuwa kiongozi wa dini hakuondoi ubinadamu wake. Anabaki na ubinadamu wake akiishi hapa hapa duniani. Anaweza kukosea na kukengeuka wakati fulani na baadaye kujirudi anapogundua kosa lake na kuacha (kutubu)..
Ndio maana Yesu Kristo alikuja duniani. Ni ili kutuwezesha kushinda majaribu haya. Alisema, hata mtu akikosea mara 7 × 70 namba ya Mungu, akikumbuka kuwa amekosea, akatubu basi yeye humsamehe na kuwa mtu mpya..
Hata Samia Suluhu Hassan, pamoja na kushiriki direct or inderectly kuua raia wake mwezi uliopita, akigundua kuwa alifanya kosa, akitubu na kukiri ATASAMEHEWA BILA MASHARTI...
Kinachotusumbua wanadamu (akiwemo Samia na wenzake) ni kiburi na jeuri inayosababishwa na factors nyingi: Uzima, mali, fedha, bunduki na wakati mwungine ujinga tu wa kutojua..