permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 12,484
- 15,297
Hii hoja inaweza kuwa na grains of truth katika historical perspective. Na kama sababu ya mwalimu ndio hiyo basi aliowatetea ndio wenye shida zaidi. Shule za Kikristu hupokea wanafunzi kutoka dini zote tofauti na shule za Waislam.Twenda taratibu kwa ushahidi.
Moja ya sababu kubwa kabisa ya Mzee Nyerere kutaifisha shule za kanisa haikuwa kutoa elimu peke yake, bali uhalisia uliokuwepo kwamba baadhi ya waislamu walitengwa kipindi cha ukolini kwenye kupata elimu. Kuna wasomi wa Tanganyika ili kupata elimu ilikuwa ni lazima wabadili dini na kuwa wakatoliki. Huu ulikuwa ni ubaguzi wa kimfumo (Systematic Discrimination) ambao uliligubika kanisa Katoliki duniani kote.
Ushahidi mwingine ni ule wa wazi, ambapo Ukatoliki uliunga mkono mauaji na unyanyasaji wa jamii zisizo za Kikatoliki duniani kote. Hili lina ukweli mchungu hata Papa Francis aliomba msamaha kwa jamii za WAHINDI WEKUNDU nchini CANADA kwa mamanyanyasao ambayo kanisa liliwafanyia kwenye maisha yao yote hadi kwenye mashule. Hili halikufanywa siku moja ni kwa miaka mingi mno.
Ushahidi upo na kanisa liliomba msamaha mbele ya dunia yote. Halikufanya hivyo kwa WAHINDI WEKUNDU, bali hata kwa WAYAHUDI ambapo Papa alienda mbali na KUWAOSHA MIGUU WAYAHUDI kwa makosa ya kibaguzi ambayo kanisa liliwafanyia kwa miaka zaidi ya elfu moja. Sasa kama kanisa lenyewe linawajibika utasemaje kwamba mimi nawatuhumu bure ???
=====================================================================
HOJA YA KISOMI HAPA NI HII:
MOSI: Je, ni kweli TEC wanamshambulia Samia kwasababu yeye ni Muislamu, Mwanamke na Mzanzibari ???
PILI: Je, ni kweli TEC hawajawahi kuwashambulia viongozi wa Kikristo, Wanaume na Watanganyika ???
TATU: Je, wanachokikema TEC ni kitu haramu au halali kwa serikali kukifanya ???