Mnaongea mambo kirahisi sana na huwa nawashangaa mno.
Tanganyika ni nchi ambayo katika huu ukanda wetu ina idadi kubwa sana ya Waislamu walioelimika kuliko sehemu nyingine za huu ukanda. Waislamu wa Tanganyika wana sifa kubwa za kipekee: UVUMILIVU WA HALI YA JUU.
Tunapenda kuwabagaza sana Waislamu wa Tanganyika ila ukweli ni kwamba ndugu zetu wana kiwango kikubwa cha Tolerance kuliko hata Zanzibar. Ukienda hata Nigeria huwezi kukuta ushirikiano mkubwa baina ya Wakristo na Waislamu kama ilivyo hapa nchini Tanganyika. Kule Zanzibar Wakristo wanabaguliwa mno na waislamu.
====================================================================
KIUSALAMA, Tanganyika imekuwa ndiyo kinara wa ulinzi ukanda huu kwasababu mitandao mingi ya kigaidi inafamika vizuri na vyombo vya usalama vya Tanzania. Waislamu wa Tanganyika ndiyo wanasadia kupambana na mitandao ya kigaidi kama Al Shabaab, Boko Haram, ISIS, Al Qaeda na Waislamu wenye misimo mikali kama The Muslim Brotherhood.
Miaka ya 2000's wakati ugaidi umeshamiri kwenye ukanda wetu TISS ilisaidia mno kuimarisha usalama kwasababu ilikuwa na taarifa nyeti kuhusu mitandao ya waislamu wenye msimamo mkali kwenye ukanda huu. Watu kama Balozi Adadi Rajabu ambaye ni Muislamu kindakindani ndiyo walikuwa vinara wa kupambana na magaidi. CIA na MI6 mpaka leo hii wanategemea taarifa kutoka TISS kuhusu mitandao ya kigaidi.
Marekani walipoanza kuvutana na Magufuli, aliwaambia TISS waache kuwapa CIA taarifa za kiintelijensia kuhusu makundi ya kigaidi ukanda huu. Huu ni ukweli ambao wengi hamuujui.
CCM iko madarakani mpaka leo hii siyo kwasababu wameshindwa kuitoa, ila kwasababu usalama wa Tanganyika is within the best interest of everyone. Kenya, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Uganda, Zanzibari, Somalia, Ethiopia na Congo zote zinategemea usalama wa Tanganyika. Waislamu wa Tanganyika mbali na madhaifu yao, wana uungwana mkubwa.
Siku hali ya siasa ikiwa mbaya hapa nchini na ukatokea mpasuko baina ya Wakristo na Waislamu, mitandao ya kigaidi itajipenyeza na kuvuruga ukanda wote huu. Marekani na Uingereza wanafahamu fika, ndiyo maana kuna ujinga wa CCM wamekuwa wakiuvumilia. Samia na genge lake wameanza kugawanya nchi na hili lina madhara. Wakristo wengi wameingia mkenge kwenye hii vita (They Took The Bait).
NIKUPE MIFANO HAI: Majasusi wa Tanzania wengi wamekufa sana Sudan, Nigeria na Somalia. Wengi wao ni vijana wa kiislamu waliokulia madrasa. Wamekufa wakilitumikia taifa kuhakikisha mimi na wewe tunaandika ujinga hapa mtandanoni. Siku unadhani mpasuko ukiwa mkubwa naina ya TEC na BAKWATA, hata hizo BARUA ZA KIKUHANI zitaandikwa kweli ????
================================================================
AU nawewe unaamini propaganda kwamba CATHOLIC CHURCH lina intelijensia kali ya kuweza kujipenyeza kwenye mitandao ya kigaidi bila msaada wa waislamu waungwana ???
-Mwisho wa haya yote utakuwa nini ???
-Hakuna njia nyingine za mazungumzo ambazo zinaweza kufanyika kuliko hii ya kutunisha misuli na kuzidi kutugawa ???