Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

Siasa za kindugu, umwagaji damu na Ukatoliki nchini Ufilipino

Kuwasema TEC kuhusu nini?
Soma hapo chini
Nashangaa sana mnaoona Wakatoliki ndio dini kubwa sana duniani, wakati ukubwa wake upo kwenye nchi masikini na za dunia ya tatu
Unadhani kwanini US, UK na Europe idadi ya wakatoliki ni ndogo?
Sababu huwa wanakiherehere sana cha kujifanya wana mamlaka, ndio maana King James aliaanzisha Bibilia yake, na kufanya UK kuwa Anglicans, na US wamewekwa kando kabisa, yaani walokole kule ndio wengi kuliko wakatoliki
Mpaka leo hii kuna vita nchini Ireland kati ya Wakatoliki na Protestant, na sababu kubwa ni kujifanya wao ndio wenye mamlaka kuliko dini zingine.

UKWELI USIOPINGIKA: Viongozi wa KANISA KATOLIKI huwa wana matatizo ya UDINI ULIOPITILIZA wa kuamini kwamba hii nchi ni mali yao na wao ndiyo wana haki ya kusema kama MIUNGU-WATU. Hii tabia ndiyo ilisababisha wakatoliki wachinjane na waprotestanti kule ULAYA kwa miaka zaidi ya 30 na kusababisha dola la rumi (The Holy Roman Empire) kuporomoka.
 
MALCOM LUMUMBA nimekuwa nikifuatilia nyuzi zako, na nimekuwa nikikuhusudu sana kwa jinsi unavyo elezea mambo, ila kwa leo hapo mwisho uliposema kuhusu mapadre ”hata wenyewe hawaelewi kwanini huwa wanatetea mengi wanayoyatetea”, niko a bit disappointed.
Nimefuatilia sana nyuzi zako, maswali nayo jiuliza:

1. uwa unatoa na mifano, ila kwnye hili hujatoa mfano, je ni jambo lipi wanalotetea ambayo hawaelewi kwanini wanatetea?

2. Kwanini hauja balance kwa kuongelea pia dhehebu lolote la kiislamu, je msheikh wa BAKWATA hawana udini?, kauli za baadhi ya watu wao kuhusu kuchinjana ni nafuu kuliko matamko/ waraka ya wakatoriki?

3. Je unatoa maoni gani juu ya kauli za mama, anaposema anakosolewa sababu ya dini yake?, je dosari zinazotolewa, iwe na wakatoriki au sio na wakatoriki, zina chembe ya udini anausema? au ni uhalisia?

4. Je wanayooengea wakatoriki yanagusa maslahi ya wakatoriki tu au ni watanzania wote?, kama ni wote kwanini ionekane wanayosema hawaelewi kwanini wanatetea?
 
Nimeona kwenye uzi wako sehemu nyingi unasema waislamu wa Tanganyika ni wavumilivu ndio maana hakuna ugaidi kwenye huu ukanda. Kwa nini unauhusisha uislamu na ugaidi??

Umerudia mara nyingi sana kuonyesha kuwa siku waislamu wakiishiwa uvumilivu basi ugaidi utaingia nchini. Kwa nn unauweka ugaidi na uislamu pamoja?

mjingamimi msome MALCOM LUMUMBA , anaamini ugaidi haupo nchini sababu waislamu wa hapa kwetu ni wavumilivu, siku wakiacha uvumilivu basi ugaidi utaingia. Anauweka uislam na ugaidi pamoja
Ugaidi ni biashara za watu.wanajificha tu kwenye uislam.ila wale jamaa Wana nguvu za ushwawishi mpaka unaona ugaidi ni sahemu ya uislam
 
Hapa ndio tunatofautisha akili zilizojaa tope na kamasi na wenye akili kubwa
Kuwasema TEC kuhusu nini?
Huyu ndiyo zero kabisa bora hata ya mleta mada unaweza ukajilazimisha kumuelewa lakini huyu!!!

Utapoteza muda wako tu na nimekuwa surprised hapo juu amejiweka kundi la wenye akili wakati humu inaaminika ndiye member mwenye akili ndogo kuliko wote.
 
Soma hapo chini
Nashangaa sana mnaoona Wakatoliki ndio dini kubwa sana duniani, wakati ukubwa wake upo kwenye nchi masikini na za dunia ya tatu
Unadhani kwanini US, UK na Europe idadi ya wakatoliki ni ndogo?
Wewe ndio unajadili wakatoliki.

Sisi tunajadili HOJA zao.

US na UK hakuna MTAWALA MWIZI , Wala anayeua na kuteka watu wake OVYO OVYO.

Kule watu wengi hawaamini dini, lakini wanatokea familia za kidini.

Nchi kama US Republican mpaka leo wanaamini DINI.
Sababu huwa wanakiherehere sana cha kujifanya wana mamlaka,
Hii ni sababu yako ya kipumbavu tu.

US na UK mwenye mamlaka ni nani sasa?

Maana hata watawala wa US na UK hawana mamlaka.
ndio maana King James aliaanzisha Bibilia yake, na kufanya UK kuwa Anglicans, na US wamewekwa kando kabisa, yaani walokole kule ndio wengi kuliko wakatoliki
Mpaka leo hii kuna vita nchini Ireland kati ya Wakatoliki na Protestant, na sababu kubwa ni kujifanya wao ndio wenye mamlaka kuliko dini zingine.
Jambo la msingi hiyo biblia yake haijahalalisha MAUAJI, UFIRAJI, UTEKAJI, IMPUNITY, WIZI, UFISADI, UTAPELI na RUSHWA.
 
Yeye anaamini waislamu wote wanakubaliana na ugaidi. Nimetoka kumuuliza ingekua hivyo basi Somalia wote wangejiunga Al shabab
Changamoto ya mfumo wa Uislam, hauna mzizi ya kitaasisi.

Unajiendesha kama makanisa ya kina Kakobe, Mwingira.

Mtu akiwa na vijisenti au akipata mfadhili wa kumjengea msikiti, basi anamiliki wale waumini na mafundisho husika.

Ndio maana kuna msikiti na waumini chini ya BAKWATA, Al Hikhma Foundation, Sheikh Ponda.

Ndio naama ni cheap sana kutumika.
 
Ni JUHA.

Anaandika kama njia ya kutishia fulani, ionekane wasio waislam watulie kwasababu waislam wakikasirika kutakuwa na UGAIDI.

Anashindwa kujua UGAIDI ni TAARIFA na RECRUITMENT.

Huko Afrika ya Kati waliokuwa wanaua waislam mpaka wanakimbilia makanisani ni ANTI BARAKA.

Anadhani vita ya kidini, basi waathirika watakuwa ni wakristo pekee na wao ndio watashindwa.

Ni JUHA, TAAHIRA kwenye kazi maalum.
Ni kazi maalum hii.
 
Alafu uwakute wakijisifia ujinga.

Eti sisi ndo idara bora ya usalama Afrika na wale wagonga nyundo JWTZ. Muda wote kujisifia ujinga tu wakati Taifa linaibiwa linafirisiwa huku wao wapo tu.

Miaka 64 ya uhuru eti kuna mgao Dar na mikoa mingine kwa sababu ya tu ya ukosefu wa mvua.

Intelejensia wanayoijua ni kuiba matokeo ya uchaguzi hadi wa madiwani kuisaidia ccm kushinda. Kuteka, kuwafira na kuua viongozi na wanachama wa nyama vya upinzani wakati Katiba tu wanayoapa kuilinda inatambua nchi kuwa ya kidemokrasia.
Nilipochoka ni aliposema kuwa EA I a waislamu wasomi na wavumilivu sana .
 
Nakubaliana kabisa na wewe, asilimia 10000% dini zimeleta umasikini Afrika.

Huu mgawanyiko kwa minajili ya kidini haitakiwi kuwepo ili tuweze kuvuka kama nchi. Tanzania ni nchi changa sana ina miaka 64 tu, hata Marekani na Uingereza ambako wewe unaishi leo na kupata kipato kuna miaka yalikuwa mataifa yanayosumbuliwa na UJINGA MTUPU wa kidini.

Baada ya kuchinjana sana kwenye Civil Wars kukawa na adabu Marekani ikaingia kwenye The Gilded Age 1872 na kuwa taifa tajiri ambalo hata wewe leo unaweza kwenda kutafuta kipato kwa amani. Hivyo hata Tanzania haiwezi kuruka hatua ambazo wakubwa wa dunia walizipitia.

Ndiyo maisha yalivyo
​
Si kweli kwamba Tanzania haiwezi kuruka, inaweza, ila tunajilemaza wenyewe kufikiri haiwezi kuruka.
 
Ukishaona watu wanasoma kimafungu kwa kuji-group kimafungu kwamba wao Waislam wanamesoma kama waislam ujue hakuna USOMI hapo.
Kumbe Malcolm ni Islam,

Anyway, thread zake nyingi huwa ana hoja,

Hii ya Leo ameegemea kwenye dini yake.
 
Nakubaliana kabisa na wewe, asilimia 10000% dini zimeleta umasikini Afrika.

Huu mgawanyiko kwa minajili ya kidini haitakiwi kuwepo ili tuweze kuvuka kama nchi. Tanzania ni nchi changa sana ina miaka 64 tu, hata Marekani na Uingereza ambako wewe unaishi leo na kupata kipato kuna miaka yalikuwa mataifa yanayosumbuliwa na UJINGA MTUPU wa kidini.

Baada ya kuchinjana sana kwenye Civil Wars kukawa na adabu Marekani ikaingia kwenye The Gilded Age 1872 na kuwa taifa tajiri ambalo hata wewe leo unaweza kwenda kutafuta kipato kwa amani. Hivyo hata Tanzania haiwezi kuruka hatua ambazo wakubwa wa dunia walizipitia.

Ndiyo maisha yalivyo
​
Watakatifu walioko duniani,

Wana wa Mungu ndio hasa sababu ya kuwepo kwa Amani hii ndogo iliyopo.
 
watekaji, wauaji na wezi wa kura ndio tatizo letu na tunawajua wanaofanya ni shetani Samia na genge lake la wahuni, uchunguzi ICC umeshaanza na list wanayo, wakatoliki sio wadini na hawajafanya kosa kukemea mauaji na wizi wa uchaguzi uliofanywa na Samia na CCM
 
Wanachokisema TEC hata sisi RAIA wema mawazo yetu ni hayo hayo.

TEC wanasema kwasababu wana nguvu.

Sisi tunakaa kimya kwasababu wana tumudu, watatuua.

So, issue siyo TEC bali ni kile wanachosema.

Kuhusu Udini, ndio maana tumemwambia aweke ushidi hapa, hana.

Anatapika tapika tu.
Una madin sana ndugu yangu
 
Umemsoma harakaharaka. Kwenye thread yake jaweka vitu vingi vya uongo ambavyo lazima vitakanushwa kwanza.

Anasema ukanda huu hakuna ugaidi sababu waislamu ni wavumilivu. Hii ni hoja nzito lakini ya uongo, wanaoaua kufanya ugaidi wana sababu zao ni kwa sababu waislamu ni wavumilivu. Pia ameunasibisha uislamu na ugaidi

Pili anasema katoliki wana udini wanaamini nchi ni yao, huu pia ni uongo. Thread yake inaelezea namna kabisa huko Philippines linavyopinga serikali, hii maana yake ni kuwa dunia nzima kanisa huikosoa serikali. Hapa majirani zetu tu kila leo wanakosolewa na kanisa.

Kenya katoliki wanamkosoa sana Rutto Hadi wamekataa pesa zake za michango, je huko napo wana udini?
Zambia kila leo wanamkosoa hichilema, je napo wana udini na kuona nchi yao?
Congokila Leo wanamkosoa raisi, je napo wana udini?

Katoliki ni wakosoaji kwenye serikali zote, si hapa nchini tu
Kwahiyo unataka kusema kwamba maada yake haina tofaut na spinning za yoga?
 
Naomba tu niwakumbushe kuwa mleta mada huwa anajaribu kuficha hisia zake kwa kalamu ila kiujumla ni:

1. Anti-Catholic
2. Pro-Chinese & Pro-Russian
3. Pro-Communist
4. Anti-Western
5. Politically ni Mhafidhina

Ukishamuelewa hivyo popote pale atakapoitaja mfano NATO, chunga sana ataisingizia. Atakapoutaja ujamaa chunga sana ataupamba au atachagua sifa yake nzuri. Ni kama utazame Al Jazeera ikiizungumzia Saudi Arabia usitegemee mazuri sana.
 
Back
Top Bottom