Siku Rais Samia akigundua wanawake ndio wanaompinga zaidi, atawapigia magoti wanaume

Siku Rais Samia akigundua wanawake ndio wanaompinga zaidi, atawapigia magoti wanaume

Umetumia kipimo gani kutambua wanawake wengi ni CCM, research au zile sare zao za kijani ambazo hata mashabiki wa Yanga wakivaa wanaonekana kama CCM?
Sinawahi kupiga kura, ila nimeshiriki kwenye chaguzi za 2010 nikiwa Ilemela na Nyamagana, 2015 nikiwa Mikumi kwa Prof Jay na 2020 nikiwa Temeke.

Wanawake wengi na wazee n8 wapoga kura wa CCM.

Vijana wengi hawana misimamo, wanachoweza ni ushabikibtu wa oya oya kama wakiwq huru. Wakitishiwa kidogo huoni mtu, kila mmoja anaenda kwenye mishe zake. Ndio maana hata uchaguzi wa 2020 wa Magu wapiga kura walikuwa wachache sana tena wanawake
 
Wanawake wepi hao unaowaongelea hapa?

Mimi na wengine wengi tunaamini kwenye wanawake wenye uwezo katika kazi na SSH anao uwezo, hata waliompokea kwenye siasa na aliyekua kiongozi wake JPM aliliona hilo
Wanawake huwa mnakuwa waongo mara nyingi.Alimteua awe mgombea mwenza ili awachote akili na mumpigie kura.Ina maana haujui hadi leo?
 
Kwani uchaguzi hapa una amliwa na idadi ya kura, au na CC (Central Committee) ya chama tawala, la muhimu yeye kupita ni kueweka chama vizuri na kuondoa wanao mpiga chawa) kama polepole na wezie, ila la muhimu asiache kambi Msoga.....huyu baba ndo architecture wa siasa za CCm, na anapendwa sanaa na wa Tz, hizo kura zawanawake hazina lolote
JK mtu sana aise. JK kawawezesha wengi kimaisha kiasi hata wanafikiria namna gani wamshukuru.
Alitoa ajira nyingi sana na alipandisha mishahara ikafika figure ambazo watu wanasema alhamdulilah" Hata biashara zilishamiri sana na uchumi ulikua, ukiacha uchumi ule wa kubumba record kutoka 7.5 kuporomoka hadi 2.kadhaa ndani ya mwezi mmoja.

JK ni mtu[emoji122][emoji122]
 
Mwanaume hutembea na wanawake akisambaza upendo na hupewa shukrani
ila
Mwanamke hutembezwa na Mwanaume!
 
Si kweli bana acheni kumpinga Rais kisa jinsia yake na kusingizia eti tuna amini wanaume kimaamuzi si kweli.
Samia akosolewe kiuomgozi na sio kumshambulia mara dhaifu kisa jinsia yake.
 
Wanawake wengi hawataki kuona wanaongozwa na mwanamke mwezao
Hilo liko wazi mtaani tunaona
 
Kufa kwa jiwe kwake ni kudra , sasa naanza kuelewa kwanini Mabula Mchembe alikua hataki mama awe Rais , sukuma gang walikua wanaelewa
 
Yaani kuna dada hapa tokea Samia anayoapishwa alianza kumponda nikawa simuelewi. Zilivyokuja tozo sasa! Yaani Samia labda apore uchaguzi kama mwendazake....wanawake ndio wa kwanza kumpinga asijidanganye na wale aa ukumbini wanaosaka vyeo saaa hivi.
 
Si kweli bana acheni kumpinga Rais kisa jinsia yake na kusingizia eti tuna amini wanaume kimaamuzi si kweli.
Samia akosolewe kiuomgozi na sio kumshambulia mara dhaifu kisa jinsia yake.
Tatizo na yeye anatumia jinsia yake Kama Kinga. Hivyo acha ashambuliwe tu kijinsia
 
Wanawake wepi hao unaowaongelea hapa?

Mimi na wengine wengi tunaamini kwenye wanawake wenye uwezo katika kazi na SSH anao uwezo, hata waliompokea kwenye siasa na aliyekua kiongozi wake JPM aliliona hilo
Itakuwa kuna jinsi unafaidika naye
 
Umeandika ukweli sana......kama kweli watampitisha kuwa mgombea wataiba sana....
Watu wengi walimpa sifa eti ni msikivu.....nafsi yangu ilisita sana kwake....sasa walewale waliokuwa wanampamba wamepigwa na butwaa.....
In short hakuna kitu.
 
Kuna jambo moja ambalo Rais Samia huenda bado hajaligundua ni kuhusu nafasi yake ya kisiasa kuwa imetengenezwa na nguvu ya siasa za vyama kuwatumia wanawake kama mtaji wa kisiasa ili kupata madaraka au kuendelea kuwa madarakani na kamwe sio kuwapa wanawake madaraka ili wawatale wanaume.

Pili mama Samia asahau kabisa kuwa wanawake wa Tanzania wanaweza kujipanga kumpa madaraka au kulinda madaraka yake, kwa sababu ya tabia za kisiasa za wanawake wa Tanzania walivyo. Kwa mfano....

1. Wanawake wengi wa Tanzania husukumwa na wanaume kimaamuzi.

2. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini kufanikiwa kwao kimaisha kunategemea kuwezeshwa na wanaume.

3. Wanawake wengi wa Tanzania hawapendi kuongozwa na mwanamke mwenzao.

4. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini adui mkubwa wa mwanamke kwenye maisha ni mwanamke mwenzake.

5. Wanawake wengi wa Tanzania wanaamini uanamke mbele ya wanaume ni ishara ya udhaifu na sio ujasiri au ufahari.

Mwisho kabisa ninapenda kuandika kuwa, Siku Rais Samia akigundua kuwa mateso ya kimaisha wanayopata wanawake yanaletwa na mwenendo mbovu wa seikali yake, hakika ataogopa kuwaambia wanawake wamuunge mkono kwenye mbio zake za urais 2025.
In short Mama kwa sasa hapendwi!!! Yaani ajikite kuleta impact kwa jamii. Akumbuke Dkt Magufuli alijengwa na kuandaliwa na TISS kwa miaka zaidi ya 10. Ktk hicho kipindi Dkt Magufuli alijipambanua na kila mtanzania hata wapinzani walitamani awe rais ili anyooshe nchi na kuleta maendeleo, ila kila mtu walijua asingepenya kwa sababu hana hela za kuhonga NEC ya CCM. Ila mfumo ulifanya yake na hatimaye akawa rais.

Mama muda aliokaa kwenye kiti ni mfupi mno, watu bado hawajamuelewa kabisa! Falsafa za uwepo wa Dkt Magufuli bado zimetawala kwenye akili za watanzania wanyonge. Ina maana Dkt Magufuli alijengwa na alipopata madaraka alifanya yale watanzania waliowerevu walitamani yafanywe na viongozi waliopita.

Ningekuwa mimi Mama Samia, ningefanya kama Obama. Aachane na kujiona ni minority! Yaani uanauke wake isiwe kigezo cha yeye kuwa rais. Na asifurahie/kusema ni baraka za Mungu yeye kuwa rais baada ya mtangulizi kufa.

Ajijenge na kutengeneza falsafa zake. Awe busy kuijua Tanzania. Ajipambanue yeye kama yeye na maono yake. Yaani ajikite kwenye kile anachotaka nchi ikifikie.

Mama ni kiongozi mzuri sana tena mwenye maono mazuri mno. Pamoja na kupokea ushauri, afanye maamuzi yake kama nafsi inavyomtuma juu ya Tanzania mpya.

Mama arudi kwenye utu wake na ajitamkie juu ya anataka Tanzania iweje.
 
In short Mama kwa sasa hapendwi!!! Yaani ajikite kuleta impact kwa jamii. Akumbuke Dkt Magufuli alijengwa na kuandaliwa na TISS kwa miaka zaidi ya 10. Ktk hicho kipindi Dkt Magufuli alijipambanua na kila mtanzania hata wapinzani walitamani awe rais ili anyooshe nchi na kuleta maendeleo, ila kila mtu walijua asingeoenya kwa sababu hana hela za kuhonga. Ila mfumo ulifanya yake na hatimaye akawa rais.

Mama muda aliokaa kwenye kiti ni mfupi mno, watu bado hawajamuelewa kabisa! Falsafa za uwepo wa Dkt Magufuli limetawala kwenye akili za watanzania wanyonge.

Ningekuwa mimi Mama Samia, ningefanya kama Obama. Ashughulikie chagamoto, awe busy kuijua Tanzania. Ajipambanue yeye kama yeye na maono yake. Yaani ajikite kwenye kile anachotaka nchi ikifikie.

Mama ni kiongozi mzuri sana tena mwenye maono mazuri mno. Pamoja na kupokea ushauri, afanye maamuzi yake kama nafsi inavyomtuma.

Mama arudi kwenye utu wake na ajitamkie juu ya anataka Tanzania iweje.
Nimependa sana ulivyoandika kuhusu JPM.
Ila kwa Rais wa sasa naomba nikupinge sio kiongozi mzuri na hana maono yoyote hivi nikiuliza yeye kama yeye uelekeo wake ni upi?....miezi sita imepita lakini so far hakuna direction iliyo clear zaidi ya maneno tu.
Miradi iliyoachwa na JPM inasuasua vibaya hili lipo wazi....huduma za Afya zimerudi nyuma sana na mengine mengi tu.
 
Tatizo na yeye anatumia jinsia yake Kama Kinga. Hivyo acha ashambuliwe tu kijinsia
Sasa na mimi naomba na 2025 aendelee kuwa Rais Ili mkome kumshambulia kwa jinsia yake na Mungu akiniweka hai nitampigia kura ya Urais ccm mkuu. Wanaume madarakani mumekuwa mkitumia wanawake kupata ulaji wakipata wanawake inakuwa nongwa
 
Uongozi usitolewe kwa sababu ya jinsia bali uwezo
 
Itakuwa Sawa kusema kuwa cheo ulichokipata baada ya aliyekuwa nacho kufa ni rehema ya mwenyezi Mungu kwako!?
Hapa ndo kuna walakini, kumbe yale machozi ya kutangaza kifo cha mtangulizi wake ilikuwa ni geresha tu. Ila kwa ndani alikuwa anashangilia ushindi wa urais wa ngekewa...........
 
Wako wanawake na waume zao ambao ni wamiliki maduka na wapangishaji wa "FREMU" za barabarani......WALIUMIA SANA KIUCHUMI KUTOKANA NA UWEPO WA MACHINGA "WANAOZAGAA" mbele ya "FREMU ZA MADUKA YAO"......

#SiempreChifuMkuuHangaya
#NchiKwanza
 
Hapa ndo kuna walakini, kumbe yale machozi ya kutangaza kifo cha mtangulizi wake ilikuwa ni geresha tu. Ila kwa ndani alikuwa anashangilia ushindi wa urais wa ngekewa...........
Kwani kuna mtu anayetamani kuzikwa na kipenzi chake?!!!

MAISHA inabidi yaendelee.....

#NchiKwanza
 
Back
Top Bottom