Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Hapa bongo kocha anayefungwa na mtani anaonekana hatoshi.
 
Kwani malengo yenu yamebadilika? Msimu ulioisha hamkuchukua hata kombe moja baadae kiongozi wenu akaongea hadharani akisema moja wapo ya malengo ilikuwa kumfunga Yanga na mlimfunga.
 
Nilitoa ushauri kipindi nikatukanwa Sasa Leo wamekuja kumtimia aibu imeshawafika.
 
.... bado MED ALI...mpayukaji !!!!
 
Uongozi wa Simba waache Uhuni, inakuwaje wanauza mechi alafu lawama atupiwe kocha? Bado kocha alikuwa anatufaa huyu hakuwa na ubaya wowote

Kocha hafai, kapewa muda ila habadiliki. Ngoja aondoke. Simba tungebaki na Mgunda, shida Viongozi wetu bado Wana utoto mwingi.
 
Azam kama wana akili ndio muda wa kumchukua huyu kocha, kwanza ana uzoefu na soka la bongo, pili azam wana wachezaji wazuri kuliko simba lakini pia kocha anawajua makolo nje ndani kwa hiyo wakikutana ni mwendo wa kuwapasua tu.
 
Watu wanamtetea kocha lakini ukweli ni kwamba mbali na mechi hii na yanga mfumo wake tangu ashike timu ulishafeli,magoli tunayofunga ni papatu papatu hamna mfumo wa maana,hakuna mpira wa malengo ni kukimbia tu na pasi ndefu,hii is a failure
Ukiona mtu anatumia nguvu kutetea ujue alikuwa anafaidika na kufeli kwa simba
 
Shida ya mashabiki wa yanga ni wanafiki, na pia ni vigeu geu wakiona simba wameshinda wapo na jezi ya simba ng'we ukiona yanga wamefunga ng'wee halafu wengi ni wachawi
 
Ila watu ni vigeu geu hivi hata ndoa zenu zipo vzr kweli?? Si mlisema hatuna kocha mara ohoo sijui kocha hana anachofanya...so leo tena mmegeuka sasa kujifanya mpo side yake...
NB
Ila mimi nimeumia jamani khaaaa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…