Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Hapa bongo kocha anayefungwa na mtani anaonekana hatoshi.
 
Nilitaka kuongelea hili, uko 100%. Mimi naamini kila team ina malengo yake ya msimu na hili lisipofikiwa kunaangaliwa nini tumekosea na watu wanawajibika. Sasa sijui kufungwa na mtani ni moja ya mambo ya malengo? Maana team inaweza kufungwa lakini kesho wakachukuwa ubingwa, CAF wakafika mbali na mafanikio nje ya uwanja. Mimi sisemi kocha mzuri au hapana hiyo ni issue nyingine na kama mbaya basi waliomuajiri inabidi wawajibike katika hili pia. Kwa hili Simba ni kama wamewapa lingine watani kuongelea, tano na kocha mmefukuza😉
Kwani malengo yenu yamebadilika? Msimu ulioisha hamkuchukua hata kombe moja baadae kiongozi wenu akaongea hadharani akisema moja wapo ya malengo ilikuwa kumfunga Yanga na mlimfunga.
 
Nilitoa ushauri kipindi nikatukanwa Sasa Leo wamekuja kumtimia aibu imeshawafika.
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

.... bado MED ALI...mpayukaji !!!!
 
Uongozi wa Simba waache Uhuni, inakuwaje wanauza mechi alafu lawama atupiwe kocha? Bado kocha alikuwa anatufaa huyu hakuwa na ubaya wowote

Kocha hafai, kapewa muda ila habadiliki. Ngoja aondoke. Simba tungebaki na Mgunda, shida Viongozi wetu bado Wana utoto mwingi.
 
Azam kama wana akili ndio muda wa kumchukua huyu kocha, kwanza ana uzoefu na soka la bongo, pili azam wana wachezaji wazuri kuliko simba lakini pia kocha anawajua makolo nje ndani kwa hiyo wakikutana ni mwendo wa kuwapasua tu.
 
Watu wanamtetea kocha lakini ukweli ni kwamba mbali na mechi hii na yanga mfumo wake tangu ashike timu ulishafeli,magoli tunayofunga ni papatu papatu hamna mfumo wa maana,hakuna mpira wa malengo ni kukimbia tu na pasi ndefu,hii is a failure
Ukiona mtu anatumia nguvu kutetea ujue alikuwa anafaidika na kufeli kwa simba
 
Shida ya mashabiki wa yanga ni wanafiki, na pia ni vigeu geu wakiona simba wameshinda wapo na jezi ya simba ng'we ukiona yanga wamefunga ng'wee halafu wengi ni wachawi
 
Ila watu ni vigeu geu hivi hata ndoa zenu zipo vzr kweli?? Si mlisema hatuna kocha mara ohoo sijui kocha hana anachofanya...so leo tena mmegeuka sasa kujifanya mpo side yake...
NB
Ila mimi nimeumia jamani khaaaa....
 
Back
Top Bottom