Siri niliyoipata katika kufunga siku 21 kila mwanzo wa mwaka

Siri niliyoipata katika kufunga siku 21 kila mwanzo wa mwaka

Wew sijui nikuite mtumishi ama nani, em tafakari kabla hujawaletea hawa izo mbinu zako za kiroho kama zina madhara ama la!.

Huwez kuingia huko kiholela namna hiyo, or otherwise uingie kupitia mind tricks kama vile Third eye opening, meditation and astral projection, accidentally unapokuwa umelala, vinginevyo haiwezekani acha kuwalisha watu watango pori
Acha kukatisha watu kiimani. Ila wewe ndio una uwezo wa kuingia?
 
JAMBO NI KUFANYA SIYO KUONGEA

Mambo haya siyo ya kuongea tu.
Mimi ninachokisema kipo kinafanyika. Wewe ni uchaguzi wako. Maarifa haya yapo na wengi huyatumia.

Kuna dini na madhehebu yapo yameandaa SALA na DUA katika maandishi. Wale watu wakikaa wiki au zaidi ya wiki wamejifungia kwa jambo hilo hilo huku wamefunga, hakika nakuambia litatokea.

Halafu haya mambo ninayoyaongelea hapa ni masuala ya IMANI. IMANI(Hisia) lazima ihusiane na MATAKWA(will)

FAITH AND WILL
vikiungana kwa pamoja lazima jambo litokee.

Wengine wanasema huwezi kumshawishi Mungu kupitia kufunga na kusali.
Watu hapa wanaongelea kitu tofauti kabisa. Hapa tunaongelea kuingia katika ulimwengu wa roho.
Uko vizuri. Nimekuelewa sana mkuu. Acha na hao wachawi wanaoogopa jinsi unavyofundisha wengine kuingia kwenye ulimwengu wa roho. Wanakatisha tamaa zisizo na maana. Mtu anakuja anaongea acha kuwafundisha.
 
Kwani kufunga lazima uache kula??.Mimi nafikiri kufunga inahusisha mambo mengi zaidi ya kujinyima kula, Nijuavyo Mimi unaweza kula tu kiasi kwaajili ya kuendeleza uhai,lkn ukajinyima vitu visivyo vya lazima,km vile unywaji wa bia au soda,ulaji wa Vyakula vizuri vizuri na vya gharama,n.k.Kisha pesa uliyoisevu kutokana na kujinyima kupeleka kwa wahitaji km vile kwenye nyumba za kulelea Wazee, watoto yatima, wagonjwa walioko mahospitalini au majumbani, watoto wa mitaani,n k.,Jambo jingine muhimu ni sala na kuomba toba na pia kutoa msamaha kwa waliokukosea au wewe kuomba radhi kwa wale uliowakosea.Ukiyafuata haya, naamini funga yako itakuwa na maana sana.
Kuna watu hamko serious . Yaani pesa uliojinyima kula upeleke kwa wahitaji?. Uko serious kweli?. Mfano ufunge siku 7. Ule kiasi tena. Katika hizo 7 ulizofunga kwa kula kiasi utakuwa ume-save kiasi gani cha kuwasaidia yatima?
 
Nimefuatulia bandiko lakini sijaona hitimisho la faida ambayo wewe uliipata baada ya kufanya hiyo meditation '

Yaani baada ya kumaliza huo mfungo ulinufaika kwakupata Nini ,

Let say uliamua kufunga kwaajili ya kuomba Kazi je ulipata (mfano tu )
Bado hujaelewa. Amekuambia ukifunga jua hitaji lako. Mfano unamdai mtu. Funga tamka lile hitaji lako. Baada ya zile siku za kufunga,hitaji lako litajibiwa au hata kabla ya kumaliza funga yako
 
SPELLS NA UCHAWI

Ulimwengu wa roho tunaouingia ni uleule. Wachawi nao wanaingia katika ulimwengu huo. Na unaweza ukaamua, kama unataka kuwa mchawi unaweza kufanya hivyo.

SPELLS
Hapa ni kutamka maneno kwa lengo la kumdhuru mwingine au kumlaani. Watu wadini wanaojua kutembea katika ulimwengu wa roho wanaweza kutumia njia hii kwaajili ya kuwadhuru wengine.

Tunaposema MANENO HUUMBA, hii ni kweli. Wakati MATAKWA NA HISIA vinapoungana katika jambo unalolitamka hutokea kweli kweli.

Soma Book of the Gospel of Thomas
(106) Jesus says:

(1) “When you make the two into one, you will become sons of man.
(2) And when you say ‘Mountain, move away,’ it will move away.”

Anaposema when you make two one, anamaanisha matakwa na hisia vifanye jambo moja.

SIWAFUNDISHI UCHAWI, lakini ndio ukweli ulivyo katika ulimwengu wa roho. Ni uamuzi wako kuamua kuwa mchawi au sio. Wengine ni wale wanaojiita watumishi wa Mungu hutumia njia hizi hizi kuweza kumlaani mtu.

Level ya kuweza kufanya hivi unaweza ukaifikia.
Mkuu #venus star habari ya majukumu kiongozi wangu..,?! Natumaini uko buheri wa afya., Swali langu ni kuhusisha hii maada yote kwa ujumla na namna mungu anavyotenda miujiza ndani yetu. Kumekua na mkangangiko sana hasa katika suala hili ulimwengu wa roho tumesikia namna nyingi za kuingia huko na namna mnavyoelezea nyinyi mliofanikiwa imekua kwa vitisho tena yaani mnaanza vyema na mnamaliza kwa vitisho tuu... Yanii kifupi uzi wako hauna tofauti na zile story za Meditations., we mtu uko ndani ya ulimwengu wa roho afu unawezaje ku mark kila linalotukia ndani yako?! [emoji848] Mfano mzuri tunaona mtu mwenye mashetan., Majini., Mapepo., Na hata wale wenye mizimu ya usaidiz katika uponyaji pindi anapopitia hali ya kupandwa na hayo mavitu ni anakua mtu aliyefumbwa nini kinachoendelea kwa wakati huo na pindi vikikuachia ni unakua kama mtu aliyepatwa na Mshangao na asiyejua nn kimetokea..., sasa nyinyi mnapokuja na hivi vistory vyenu vya kufikirishana in deep mtambue kuna watu wanawafuata kile mnachokisema na kukiandika maana hivi sasa mnafanya sifa kweli ili mfuatiliwe vizuri mnaweka vijipande kama seasons [emoji38]
 
Mnauwa watu na mtazidi kuuwa watu na hizi nafsi mtakuja kuzijibisha siku moja Endeleeni tu kufanya huu ukatili [emoji41]
 
Kuna watu hamko serious . Yaani pesa uliojinyima kula upeleke kwa wahitaji?. Uko serious kweli?. Mfano ufunge siku 7. Ule kiasi tena. Katika hizo 7 ulizofunga kwa kula kiasi utakuwa ume-save kiasi gani cha kuwasaidia yatima?
Ndio hivyo.Km hutaki saga chupa unywe.
 
Mnauwa watu na mtazidi kuuwa watu na hizi nafsi mtakuja kuzijibisha siku moja Endeleeni tu kufanya huu ukatili [emoji41]
Nadhani hii ni imani yako. Ulimwengu wa roho ni free world. Ni wewe tu kuijua njia.
 
Nasubiria funga aina nyingine.. nimewahi kuweka nia ya kufunga na nkafunga mwaka jana kipindi cha kwa resima.

Ila ilivyofika saa 9 ntapambana na njaa na hasira na myu naye qkaja akanivuruga end of the story nkashusha hasira na kitimoto
Pole Sana,hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu
 
Mleta huu Uzi siku ukifika kuzimu utaikuta hivi kazi unayoifanya...maana unayatumia maarifa vibaya ... Unafundisha mfungo wa siku 21 afu unawaambia watu wachague uchawi au (....) Mabano haujisemi wewe ni nani - mlokole au mpagani... Neno la msalaba ni upuzi kwao wanaopotea Bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu .. Siionei haya injili ni uwezo uletao wokovu..Kol 3;
16-17 Na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo fanyeni yote ktk Jina la Bw Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye...Mimi ni mlokole !
Safi kabisa
 
SPELLS NA UCHAWI

Ulimwengu wa roho tunaouingia ni uleule. Wachawi nao wanaingia katika ulimwengu huo. Na unaweza ukaamua, kama unataka kuwa mchawi unaweza kufanya hivyo.

SPELLS
Hapa ni kutamka maneno kwa lengo la kumdhuru mwingine au kumlaani. Watu wadini wanaojua kutembea katika ulimwengu wa roho wanaweza kutumia njia hii kwaajili ya kuwadhuru wengine.

Tunaposema MANENO HUUMBA, hii ni kweli. Wakati MATAKWA NA HISIA vinapoungana katika jambo unalolitamka hutokea kweli kweli.

Soma Book of the Gospel of Thomas
(106) Jesus says:

(1) “When you make the two into one, you will become sons of man.
(2) And when you say ‘Mountain, move away,’ it will move away.”

Anaposema when you make two one, anamaanisha matakwa na hisia vifanye jambo moja.

SIWAFUNDISHI UCHAWI, lakini ndio ukweli ulivyo katika ulimwengu wa roho. Ni uamuzi wako kuamua kuwa mchawi au sio. Wengine ni wale wanaojiita watumishi wa Mungu hutumia njia hizi hizi kuweza kumlaani mtu.

Level ya kuweza kufanya hivi unaweza ukaifikia.
Naweka kambia
 
Ni kweli usemavyo mkuu. Mimi niliwahi kufunga mda mrefu sana aise Mambo niliyokuwa nashuhudia mpaka nilikuwa naogopa. Hii dunia tunayoishi Ni hatari Sana.
 
Ngoja nianze kwa kusema.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

Kisha niongezee kwa kusema Andiko linaua bali Roho anahuisha.

Sasa hebu soma katika biblia upate kujua mzimu wa Samweli ulivyopandishwa.
11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
1 Samweli 28:11

13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13

14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14
SAULI ALIENDA KWA MCHAWI NDIO AKAPANDISHIWA HUO MZIMU WA SAMWELI, USITUMIE MAANDIKO KU PROVE UMIZIMU
 
Ngoja nianze kwa kusema.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

Kisha niongezee kwa kusema Andiko linaua bali Roho anahuisha.

Sasa hebu soma katika biblia upate kujua mzimu wa Samweli ulivyopandishwa.
11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.
1 Samweli 28:11

13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.
1 Samweli 28:13

14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14
Je ! Saul alikutana na Samweli kwa yule mchawi?

Ili kupata picha ya karibu, lazima tuwe na hoja...

1 Mambo ya nyakati 10: 13- 14
13 Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,
14 asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.
Hii habari inataja moja kwa moja kuwa Sauli alikosea kutaka msaada kwa Mchawi, hivyo Mungu akamuua.

1. Sauli ni mtu asie mtii Mungu, hivyo kama angejibiwa kupitia Mchawi, kiu yake ingetimia, kiu ya uasi juu ya Mungu.
Hata sasa wapo watu ambao kila wakimuomba Mungu, asipowajibu wanakimbilia kwa waganga au mizimu na andiko hili ndilo wanalishika.
2. Mungu amenyima watu wasiwaendeee waganga wala wachawi, hawezi vunja neno lake mwenyewe.
3. Taarifa za Samweli zinatia shaka, Samwel hakuwa Mtu wa kutaja laana kwa Sauli, ila Samweli alidumu katika kumuombea Sauli hadi Mungu alimuuliza, atadumu kumuombea Saul hadi lini? 1 samwel 16:1
4. Kutokana na Luka 16:18-31
Hakuna uwezekano wa mawasiliano kati ya wafu na watu walio hai...
Mtu akiwa hai anakuwa na uhuru wa kuchagua pa kwenda, ila akifa, habari yake imeisha, anaenda aliko chagua,... hakuna namna hata kwa maombi ya kumsaidia au kumuhamisha tena.
........26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu......
 
Utakapoanza kuona, unakutana waliokufa zamani na kuongea nao; USIOGOPE upo katika safari ya kuelekea ulimwengu wa roho level ya juu zaidi.
Kutokana na Luka 16:18-31

Back
Top Bottom